Mhe. Li akisalimiana na Mhe. Yusuph Mzee, Waziri wa Fedha wa Zanzibar pamoja na Viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliofika kumpokea. |
Mhe. Li akisalimiana na Balozi Silima Haji, Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar |
Mhe. Li pamoja na Mawaziri katika picha ya pamoja na Madaktari kutoka China wanaotoa huduma katika Hospitali za Zanzibar |
Mhe. Li na Mhe. Balozi Idd wakiwa wamewasili kwa ajili ya kuanza mazungumzo rasmi kuhusu ushirikiano kati ya Zanzibar na China. |
Mhe. Balozi Idd akiwa na baadhi ya Mawaziri waliohudhuria mazungumzo kati yake na Makamu wa Rais wa China (hayupo pichani) |
Mhe. Li na baadhi ya wajumbe alifuatana nao katika mazungumzo na Mhe. Balozi Idd (hayupo pichani) |
Mhe. Li na ujumbe wake wakati wa mazungumzo. |
Mhe. Balozi Idd na ujumbe wake wakati wa mazungumzo na Mhe. Li na ujumbe wake (hawapo pichani) |
Mhe. Li akiangalia moja ya kiuongo aina ya manjano au tumeric alipotembelea shamba la viungo vya chakula huko Kizimbani Zanzibar. Anayempatia kiungo hicho ni Bw. Fumu Ali Garo. |
Mhe. Li akiwaonesha kitu kwa mbali Wajumbe aliofuatana nao mara baada ya kutembelea eneo la kihistoria la Ngome Kongwe Zanzibar. Mwenye tai nyekundu ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Mhe. George Mkuchika. |
Mhe. Li akipata maelezo kuhusu historia ya watawala wa kiarabu waliowahi kuitawala Zanzibar zamani kutoka kwa Mkurugenzi wa Makumbusho na Mambo ya Kale, Bi Amina Ameir. |