Thursday, July 3, 2014

Mhe. Rais apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Romania hapa nchini


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa mHE. Julia Pataki, Balozi wa Romania hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi, Kenya. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Julai, 2014.
Balozi Pataki akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) mara baada ya Balozi huyo kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mhe. Rais Kikwete.
Balozi Pataki akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha aliyekuwepo wakati Balozi huyo anawasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais.
Balozi Pataki akisikiliza wimbo wa taifa wa Romania kutoka kwa Bendi ya Polisi (hawapo pichani). Wengine katika picha ni Balozi Mohammed Juma Maharage (kulia), Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki na Bw. Shaaban Gurumo, Mnikulu.
Bendi ya Polisi.

Mhe. Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Sri Lanka nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mhe. Kana V. Kananathan, Balozi wa Sri Lanka nchini mwenye makazi yake Kampala, Uganda. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 03 Julai, 2014.
Balozi Kananathan akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) mara baada ya kuwasilisha kwa Rais Hati zake za Utambulisho.
Balozi Kananathan akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha.
Balozi Kananathan akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mmabo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki.
Balozi Kananathan akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu
Balozi Kananathan akipigiwa wimbo wa taifa lake kwa heshima yake. Wengine ni Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Juma Maharage (kulia) na Mnikulu, Shaaban Gurumo (kushoto)
Bendi ya Polisi ikipiga wimbo wa taifa
Balozi Kananathan akipeana mkono na Kiongozi wa Bendi ya Polisi, ASP Mayala Kulwa
Maafisa Mambo ya Nje, Bw. James Bwana na Mercy Kitonga wakisikiliza wimbo wa taifa ulipopigwa wakati wa kumkaribisha Ikulu Balozi wa Sri Lanka hapa nchini (hayupo pichani)

Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Poland nchini


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mhe. Marek Ziolkowski  ambaye ni Balozi wa Poland nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 03 Julai, 2014.
Balozi Ziolkowski akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) mara baada ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mhe. Rais Kikwete.


Balozi Ziolkowski akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha huku Mhe. Membe na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Joseph Sokoine wakishuhudia.

Balozi Ziolkowski akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu.

Balozi Ziolkowski akisikiliza Wombo wa Taifa lake ukipigwa kwa heshima yake mara baada ya kuwasili Ikulu. Kulia ni Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Juma Maharage na kushoto ni Mnikulu, Bw. Shaaban Gurumo
Bendi ya Polisi ikiongozwa na ASP Mayala Kulwa wakipiga nyimbo za taiafa za Tanzania na Poland kwa heshima ya Balozi wa Poland hapa nchini

Mwanamfalme Akishino wa Japan awasili nchini kwa ziara rasmi

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akizungumza na Mwanamfalme Akishino wa Japan mara baada ya Mwanamfalme huyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza ziara yake ya siku tano hapa nchini.
Mhe. Mahadhi na Mwanamfalme Akishino wa Japan wakiendelea na mazungumzo huku Mke wa Mwanamfalme huyo (kulia) pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mhe. Salome Sijaona (kushoto) na Balozi wa Japan hapa nchini, Mhe.  Masaki Okada wakisikiliza.
Mazungumzo yakiendelea.

Vacancy Announcement


Kaimu Katibu Mkuu atembelea Banda la Wizara kwenye Maonesho ya Sabasaba

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili kwenye Banda la Maonesho la Wizara katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere ambako Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanafanyika. Wengine wanaoshuhudia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bw. Mkumbwa Ally (mwenye suti) na Bw. Mashaka Chikoli, Afisa kutoka Idara ya Sera na Mipango.
Balozi Gamaha akizungumza na Watangazaji  kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuhusu umuhimu wa ushiriki wa Wizara kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa kuwa ni pamoja na  kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi ambayo imejikita kwenye kukuza biashara, kuvutia watalii na kutangaza fursa za uwekezaji kupitia Balozi za Tanzania nje ya nchi.
 Bw. Chikoli akizungumza na mmoja wa wananchi waliofika kutembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Balozi Gamaha akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa kutoka Wizarani na Taasisi zilizo chini ya Wizara ambazo ni APRM, AICC na Chuo cha Diplomasia (CFR).

Picha na Reginald Philip


Wednesday, July 2, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa leo imepokea taarifa kutoka Ubalozi wa Libya hapa nchini kuwa aliyekuwa Kaimu Balozi wa Libya, Bwana Ismail Nwairat, amefariki dunia jana kwa kujipiga risasi.

Taarifa hiyo ya ubalozi imeeleza kuwa kifo hicho kimetokea majira ya saa Saba mchana ofisini kwa Kaimu Balozi huyo katika jengo la Ubalozi wa Lbya. 

Inataarifiwa kuwa Bwana Nwairat alijifungia ofisini na kujifyatulia risasi kifuani upande wa kushoto. Maafisa ubalozi walivunja mlango waliposikia mlipuko wa bunduki na kumkuta Kaimu Balozi Nwairat ameanguka chini. Walimkimbiza hospitali ya AMI Oysterbay ambako alitangazwa kuwa alikwisha kufariki na Polisi walithibitisha kifo hicho.

Maiti imehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Ubalozi unafanya maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu Nwairat kwenda Nyumbani kwa mazishi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeuhakikishia Ubalozi wa Libya Ushirikiano wake katika kipindi hiki kigumu.

IMETOLEWA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Dar es Salaam
Julai 2,2014


Tuesday, July 1, 2014

Press Release

H.E. David Johnston

PRESS RELEASE

H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to His Excellency David Johnston, Governor General and Commander-in-Chief of Canada on the occasion of the National Day of Canada.

The message reads as follows.

“Your Excellency David Johnston,
  The Governor General and
  Commander-in-Chief of Canada,
  Ottawa,

  CANADA.


        Your Excellency,

On behalf of the people and the Government of the United Republic of Tanzania, and indeed on my own behalf, I wish to convey to you and through you to the Government and People of Canada, my heartfelt congratulations on the occasion of the National Day of Canada.

Canada and Tanzania have over the years enjoyed good bilateral relations. The celebration of your country’s National Day provides me with yet another opportunity to reiterate my personal commitment and that of my Government to working with You and Your Government much closer in strengthening further the long ties of friendship, co-operation and partnership that happily exist between our two countries and peoples for mutual benefit.

I wish you, Your Excellency, personal good health and prosperity for the people of Canada.

Please accept, Your Excellency, my personal regards and best wishes for your continued good health and success”.


Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam

1st July, 2014

Mwanamfalme Akishino wa Japan kutembelea Tanzania

Mwanamfalme Akishino
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mwanamfalme Akishino wa Japan na Mkewe wanatarajiwa kuwasili nchini tarehe 02 Julai, 2014 kwa ziara rasmi ya siku tano.

Akiwa hapa nchini Mwanamfalme Akishino atakutana kwa mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya kutembelea Kituo cha Mafunzo cha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO); Makumbusho ya Taifa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Akiendelea na ziara yake, Mwanamfalme Akishino atatembelea Visiwa vya Zanzibar na kufanya mazungumzo na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kabla ya kutembelea eneo la Mji Mkongwe na hatimaye kuelekea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro na Mbuga ya Wanyama ya Serengeti.

Aidha, katika siku ya mwisho ya ziara yake Mwanamfalme Akishino atatembelea Banda la Japan kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba.

Mwanamfalme Akishino ambae ni mtoto wa pili kati ya watoto watatu wa Mfalme Akihito anatarajiwa kumaliza ziara yake hapa nchini tarehe 06 Julai, 2014 na kuondoka siku hiyo hiyo kurejea nchini kwake.

IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.


01 JULAI, 2014



Mhe. Membe azungumza na Balozi wa Sweden hapa nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.)  akimkaribisha Ofisini kwake Balozi wa Sweden hapa nchini, Mhe. Lennarth Hjelmaker
alipofika kwa mazungumzo.
Mhe. Membe akimsikiliza Balozi Hjelmaker wakati wa mazungumzo yao ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia suala la ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden ambao unatimiza miaka 50 mwaka huu.
Balozi Hjelmaker akimwonesha Mhe. Membe picha mbalimbali ambazo zipo kwenye Kitabu kinachoelezea miaka 50 ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden. 


Mke wa Mfalme Mswati wa II wa Swaziland awasili nchini wa ziara

Ndege iliyombeba Mke wa kwanza wa Mfalme  Mswati ikiwasili katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Juliusa Nyerere jijini Dar es salaam.

Mke wa Kwanza wa Mfalme Mswati wa II wa Swaziland Malikia Nomsa La - Matsebula akiteremka katika ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kuwasili nchini kwa ziara.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akimpokea Malkia Nomsa La - Matsebula mara baada ya kuwasili nchini.
Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mtoto wa Mfalme Mswati II ambaye amefuatana na Malkia Nomsa kwenye ziara hapa nchini.
Malkia Nomsa La - Matsebula akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Raymond Mushi
Malkia Nomsa akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji anayewakilisha pia nchini Swaziland, Mhe. Shamim Nyanduga
Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi Bi. Hellen Kafumba akisalimiana na Malkia Nomsa
Picha na Reginald Philip

Monday, June 30, 2014

Mhe. Membe amuaga rasmi Balozi wa Afrika Kusini nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumuaga aliyekuwa Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini, Mhe. Thanduyise Henry Chiliza ambaye amemaliza muda wake wa kazi. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) Jijini Dar es  Salaam.
Balozi Chiliza (kulia) akiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha (katikati) pamoja na Balozi wa Nigeria hapa nchini, wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Chiliza.
Balozi Chiliza nae akizungumza 
Mhe. Membe na Balozi Chiliza wakigonganisha glasi kutakiana afya njema na ushirikiano imara kati ya Tanzania na Afrika Kusini
Mhe. Membe akimkabidhi Balozi Chiliza zawadi ya picha ya kuchora ya Mlima Kilimanjaro.
Picha ya pamoja

Picha na Reginald Philip

Mhe. Membe amuaga rasmi Balozi wa Somalia nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Balozi wa Somalia hapa nchini, Mhe. Abdihakim Ali Yasin ambaye alifika Ofisini kwake  kwa ajili ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
Mhe. Membe akimsikiliza Mhe. Balozi Yasin alipofika Ofisini kwake kwa lengo la kumuaga.
Mhe. Membe akiagana na Balozi Yasin
Mhe. Membe akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Yasin pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (kushoto), Bi. Faduma Abdullahi Mohamud (wa pili kutoka kulia), Afisa kutoka Ubalozi wa Somalia hapa nchini na Bw. Bujiku Sakila (kulia), Afisa Mambo ya Nje.