Thursday, July 3, 2014

Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Poland nchini


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mhe. Marek Ziolkowski  ambaye ni Balozi wa Poland nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 03 Julai, 2014.
Balozi Ziolkowski akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) mara baada ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mhe. Rais Kikwete.


Balozi Ziolkowski akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha huku Mhe. Membe na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Joseph Sokoine wakishuhudia.

Balozi Ziolkowski akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu.

Balozi Ziolkowski akisikiliza Wombo wa Taifa lake ukipigwa kwa heshima yake mara baada ya kuwasili Ikulu. Kulia ni Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Juma Maharage na kushoto ni Mnikulu, Bw. Shaaban Gurumo
Bendi ya Polisi ikiongozwa na ASP Mayala Kulwa wakipiga nyimbo za taiafa za Tanzania na Poland kwa heshima ya Balozi wa Poland hapa nchini

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.