Friday, July 4, 2014

Waziri Membe apokea Hati za Utambulisho za Mwakilishi mpya wa IFAD nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akipokea Hati za Utambulisho za Mwakilishi mpya wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Chakula na Kilimo (IFAD) hapa nchini, Bw. Francisco Javier Pichou Angulo.  Hafla hiyo fupi ilifanyika Ofisini kwa Mhe. Membe tarehe 04 Julai, 2014.
Mhe. Membe akimsikiliza Bw. Angulo alipozungumza nae baada ya kupokea hati zake za Utambulisho. Miongoni mwa masuala aliyoahidi Mwakilishi huyo ni pamoja na kuendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali ya Tanzania katika Sekta ya Kilimo na Chakula.
Mhe. Membe nae akizungumza huku akisikilizwa na Mwakilishi huyo pamoja na Afisa aliyefuatana nae pamoja Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa kwanza kushoto)
Picha ya pamoja.


Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.