Thursday, July 17, 2014

Mhe. Rais apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Hungary nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho za Mhe. Sander Kocsis, Balozi wa Hungary nchini Tanzania mwenye makazi Nairobi, Kenya. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam hivi karibuni.
Balozi Kocsis akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu.
Balozi Kocsis akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) mara baada ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mhe. Rais.
Balozi Kocsis akisalimiana na Balozi Joseph Sokoine, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mhe. Rais Kikwete akizungumza na Balozi Kocsis.

Mhe. Rais katika picha ya pamoja na Balozi Kocsis, Waziri Membe na Mhe. Mark Mwandosya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi Maalum.
Balozi Kocsis akisikiliza wimbo wa taifa lake uliopigwa na bendi ya polisi (haipo pichani) kwa heshima yake. Wengine katika picha ni Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohhamed Maharage Juma (kulia) na Mnikulu, Bw. Shaaban Gurumo (kushoto)
ASP Kulwa akiongoza Bendi ya Polisi wakati wa mapokezi ya Balozi Kocsis (hayupo pichani)

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.