Thursday, July 17, 2014

Mhe. Rais apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Shelisheli nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hatiza Utambulisho za Mhe. Claude Morel, Balozi wa Shelisheli hapa nchini mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 15 Julai, 2014.
Balozi Morel akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu.
Mhe. Rais Kikwete akimtambulisha kwa Balozi Morel, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) huku Prof. Mark Mwandosya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi Maalum akishuhudia.
Mhe. Rais Kikwete akizungumza na Balozi Morel.
Mhe. Balozi Morel (katikati) akisikiliza wimbo wa taifa lake mara baada ya kuwasili Ikulu. Wengine katika picha ni Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohamed Maharage Juma (Kulia) naBw. Shaaban Gurumo, Mnikulu. 
Bendi ya Polisi ikiongozwa na ASP Kulwa wakiwa kazini

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.