Friday, July 4, 2014

Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Malaysia na Cote d'Ivoire nchini


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Malaysia nchini mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Ismail Salem. Haf;la hiyo fupi ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 4 Julai, 2014.
Mhe. Rais akimtambulisha Balozi Salem kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule.
Mhe. Balozi Salem akisalimiana na Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Balozi Salem akisalimiana na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Khatib Makenga.
Mhe. Rais Kikwete akizungumza na Balozi Salem mara baada ya kupokea hati zake za utambulisho
Balozi Salem akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kukabidhi hati zake za Utambulisho.
Balozi Salem akisikiliza Wimbo wa Taifa lake mara baada ya kuwasili Ikulu. Wengine katika picha ni Balozi Mohammed Maharage Juma, Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki na Mnikulu, Bw. Shaaban Gurumo.
Bendi ya Polisi ikipiga wimbo wa taifa la Malaysia kwa heshima ya Balozi wake (hayupo pichani). 

....Balozi wa Cote d'Ivoire nae awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais

Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Maharage Juma (katikati) akimtambulisha Balozi wa Cote d'Ivoire nchini mwenye makazi yake mjini Nairobi, Kenya, Mhe. Georges Aboua kwa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla Balozi huyo hajawasilisha Hati za Utambulisho
Balozi Aboua akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais Kikwete.
Mhe. Rais Kikwete akimtambulisha kwa Balozi Aboua Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule.
Balozi Aboua akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Vincent Kibwana.
Balozi Aboua akisalimiana na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Selestine Kakele.
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Balozi Aboua (kushoto) na Afisa aliyefuatana na Balozi huyo.
Rais Kikwete akizungumza na Balozi Aboua.
Balozi Aboua akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu.
Balozi Aboua akisikiliza wimbo wa taifa lake mara baada ya kuwasili Ikulu. Wengine katika picha ni Balozi Mohammed Maharage Juma, Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki pamoja na Mnikulu, Bw. Shaaban Gurumo.
Bendi ya Polisi ikiongozwa na ASP Kulwa ikipiga wimbo wa taifa kwa heshima ya Balozi Aboua wa Cote d'Ivoire nchini (hayupo pichani)

Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.