Thursday, July 10, 2014

Mhe. Membe na Mhe. Simmonds wazungumzia kuimarisha ushirikiano

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.)  akisalimiana na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya  Afrika, Mhe. Mark Simmonds kabla ya kuanza kikao kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza kilichofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) tarehe 09 Julai, 2014. Mhe. Siimmonds alifanya ziara ya siku mbili nchini kwa lengo la kukuza na kuimarisha ushirikiano.
Mhe. Membe (kulia) na ujumbe wake pamoja na Mhe. Simmonds (kushoto) na ujumbe wake wakati wa mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.
Mhe. Membe ( katikati) na Mhe. Simmonds (wa nne kutoka kushoto) katika picha ya pamoja  na Mabalozi na baadhi ya Watendaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kushoto kwa Mhe. Simmonds ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kalaghe na kulia kwa Mhe. Membe ni Balozi Diana Melrose, Balozi wa Uingereza nchini. Wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Joseph Sokoine (wa tatu  kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Japhet Mwaisupule (kushoto), Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Ulaya na Amerika, Bibi Victoria Mwakasege (wa pili kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bw. Innocent Shiyo (kulia).

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.