Friday, July 4, 2014

Waziri Membe apokea Hati za Utambulisho za Mwakilishi mpya wa UNFPA nchini

Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akisalimiana na Mwakilishi mpya wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa unaoshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA) hapa nchini, Dkt. Natalia Kanem alipofika Ofisini kwake kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho.
Mhe. Membe akipokea Hati za Utambulisho za Dkt. Kanem.
Mhe. Membe akizungumza na Dkt. Natalia kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu idadi ya watu na maendeleo. Kwa upande wake Dkt. Kanem aliahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika masuala ya idadi ya watu ambapo pia aliipongeza Tanzania hususan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwa mstari wa mbele katika kutetea Afya ya Mama na Mtoto duniani. 
Picha ya pamoja kati ya Mhe. Membe na Dkt. Kanem. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa pili kutoka kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi Mindi Kasiga (wa pili kutoka kulia), Afisa Mambo ya Nje, Bibi Samira Diria (wa kwanza kulia) na Mtaalam wa Mawasiliano kutoka UNFPA, Bi. Sawiche Wamunza.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.