Thursday, July 10, 2014

Mhe. Membe, Mhe. Sommonds na Mhe. Nyalandu wazungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ushirikiano kati ya Uingereza na Tanzania



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza wakati wa Mkutano wa pamoja kati yake Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Mark Simmonds (waliokaa kushoto), Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb.) (waliokaa katikati)  na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Julai, 2014. Wakati wa Mkutano huo Mawaziri hao waliwaeleza waandishi wa habari masuala mbalimbali ya ushirikiano  kati ya Tanzania na Uingereza ikiwemo Vita dhidi ya Ujangili wa Wanyamapori hususan Tembo na Faru na  namna ya kukomesha biashara ya meno ya tembo duniani, Uingereza kuendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta za Kilimo, Mafuta na Gesi, Nishati endelevu na kutengeneza mazingira mazuri ya biashara. Bw. Simmonds alifanya ziara ya siku mbili nchini kuanzia tarehe 8 hadi 9 Julai, 2014.
Mhe. Simmonds nae akiongea wakati wa mkutano huo na Waandishi wa Habari juu ya ziara yake 


Waziri Nyalandu akizungumza na waandishi wa

Sehemu ya Waandishi wa Habari wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mawaziri (hawapo pichani)

Baadhi ya Wawakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  na Ubalozi wa Uingereza akiwemo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizarani, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia) wakiwasikiliza Mawaziri (hawapo pichani)
Mmoja wa Waandishi wa Habari kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Ufaransa akiuliza swali kwa Waheshimiwa Mawaziri.
Mhe. Simmonds akijibu swali .
Waziri Membe akisisitiza jambo

Picha na Reginald Philip.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.