Thursday, July 3, 2014

Mhe. Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Sri Lanka nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mhe. Kana V. Kananathan, Balozi wa Sri Lanka nchini mwenye makazi yake Kampala, Uganda. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 03 Julai, 2014.
Balozi Kananathan akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) mara baada ya kuwasilisha kwa Rais Hati zake za Utambulisho.
Balozi Kananathan akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha.
Balozi Kananathan akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mmabo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki.
Balozi Kananathan akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu
Balozi Kananathan akipigiwa wimbo wa taifa lake kwa heshima yake. Wengine ni Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Juma Maharage (kulia) na Mnikulu, Shaaban Gurumo (kushoto)
Bendi ya Polisi ikipiga wimbo wa taifa
Balozi Kananathan akipeana mkono na Kiongozi wa Bendi ya Polisi, ASP Mayala Kulwa
Maafisa Mambo ya Nje, Bw. James Bwana na Mercy Kitonga wakisikiliza wimbo wa taifa ulipopigwa wakati wa kumkaribisha Ikulu Balozi wa Sri Lanka hapa nchini (hayupo pichani)

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.