Thursday, July 3, 2014

Mhe. Rais apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Romania hapa nchini


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa mHE. Julia Pataki, Balozi wa Romania hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi, Kenya. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Julai, 2014.
Balozi Pataki akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) mara baada ya Balozi huyo kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mhe. Rais Kikwete.
Balozi Pataki akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha aliyekuwepo wakati Balozi huyo anawasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais.
Balozi Pataki akisikiliza wimbo wa taifa wa Romania kutoka kwa Bendi ya Polisi (hawapo pichani). Wengine katika picha ni Balozi Mohammed Juma Maharage (kulia), Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki na Bw. Shaaban Gurumo, Mnikulu.
Bendi ya Polisi.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.