Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga (kulia) akifuatilia kwa makini
hotuba kutoka kwa Waziri Membe.
|
Viongozi mbalimbali wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri Membe kwaniaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard K. Membe akiwapungia mkono wanafunzi wa Shule za Sekondari kutoka Tanzania bara (hawapo pichani). |
Waziri Membe akipiga Mpira kuashiria kufunguliwa kwa mashindano hayo rasmi |
Waziri Membe
akisalimiana na wachezaji wa mpira wa miguu kutoka Shule ya Sekondari ya
Makongo kabla ya kuanza mechi.
|
Waziri Membe akisalimiana pia na wachezaji wa shule ya Sekondari ya Mvara kutoka Uganda. |
Mechi ikiendelea |
Waziri Membe akishangilia baada ya Makongo Sekondari kufunga goli. |
Wachezaji wa Makongo Sekondari wakishangilia goli lao
Picha na Reginald Philip
|
-------------------------------------------------------------------------------------------
Mhe. Membe Amwakilisha Rais Michezo ya Shule A. Mashariki
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.),
alimwakilisha Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, kufungua Mashindano ya 13 ya Shirikisho la Vyama vya Michezo vya
Shule za Sekondari za Afrika Madhariki (FEASSSA), jijini Dar es Salaam Jana.
Mashindano hayo yanahisisha timu za michezo mbali mbali za Shule 205 kutoka Kenya, Uganda, Sudani Kusini, Rwanda, Burundi, Zanzibar na Tanzania Bara, zenye washiriki 3,000.
Mashindano
yatarindima kwenye Uwanja wa Taifa kwa siku 10.
Katika
hotuba iliyosomwa na Mhe. Membe, Rais Kikwete alisema michezo hiyo ni moja ya
mikakati ya utekelezaji wa itifaki ya utengamano wa Afrika Mashariki.
"Aidha,
michezo hii ni kiashiria tosha cha azma madhubuti tuliyo nayo ya kuimarisha
Umoja wetu," alisema.
Alizitaka
Nchi za Afrika Mashariki kushirikiana kuendeleza michezo, akashauri Mashindano
hayo yashirikishe pia Shule za msingi.
"Kwa
niaba ya Marais wa Nchi za Afrika Mashariki, na kwa niaba ya Nchi yangu,
napenda kuwahakikishia kuwa serikali za nchi zote zitaendelea kuwainga mkono na
kuwezesha michezo hii kufanyika kila mwaka," alisema.
"Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Mhe. Hawa Ghasia, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa); Mhe. Dkt. Shukururu Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi; Dkt. Abdullah Juma Abdullah, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mawaziri kutoka Sudani Kusini na Uganda.