Thursday, August 14, 2014

Rais Kikwete afungua rasmi Kongamano la Kwanza la Diaspora nchini


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiingia Ukumbini kwa ajili ya ufunguzi  rasmi wa Kongamano la Kwanza la Diaspora hapa nchini lililoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Taasisi ya Tanzania Diaspora Initiative (TDI). Kongamano hilo lililofanyika kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam limewakutanisha Watanzania wanaoishi nje ya nchi  kutoka nchi zaidi ya 17 ikiwemo Marekani, Uingereza, Canada, Cambodia, Zambia, Ujerumani, Ufaransa, Poland, Saudi Arabia, Afrika Kusini, China, Tunisia, Comoro na Finland.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya pamoja na washiriki wengine wa mkutano wakimkaribisha Mhe. Rais Kikwete alipowasili kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kwanza la Diaspora hapa nchini.
Mkurugenzi wa Idara ya  Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki pamaja na Bi. Premi Kibanga, Mwandishi Msaidizi wa Rais  wakati wa mapokezi ya Mhe. Rais Kikwete kwenye Kongamano la Diaspora.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi Kongamano la Kwanza la Diaspora hapa nchini lililoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Taasisi ya Tanzania Diaspora Initiative (TDI). Kongamano hilo lililofanyika kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam limewakutanisha Watanzania wanaoishi nje ya nchi  kutoka nchi zaidi ya 17 ikiwemo Marekani, Uingereza, Canada, Cambodia, Zambia, Ujerumani, Ufaransa, Poland, Saudi Arabia, Afrika Kusini, China, Tunisia, Comoro na Finland.
Kaimu Wakurugenzi wa Idara za Afrika na Ulaya na Marekani  katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Victoria Mwakasege (kushoto) na Bi. Zuhura Bundala (wa pili kushoto) wakifuatilia hotuba ya Mhe. Rais Kikwete wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kwanza la Diaspora. Anayefuata ni Bw. Yusuph Mndolwa, Afisa Mambo ya Nje kutoka Ubalozi wa Tanzania Sweden.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Diaspora Initiative (TDI), Bw. Emmanuel Mwachullah nae akizungumza wakati wa Kongamano la Kwanza la Diaspora hapa nchini. Taasisi ya TDI imeshirikiana na Serikali katika kuandaa Kongamano hilo.
Bw. Caesar Waitara, Afisa Mambo ya Nje kutoka Ubalozi wa Tanzania Ujerumani akiwa na Bw. Peter Kazaura, Mwanadiaspora kutoka Ujerumani
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi. Rosemary Jairo akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa Kongamano hilo.
Maafisa Mambo ya Nje wakinukuu hotuba ya Mhe. Rais Kikwete. Kulia ni Bw. Celestine Kakele na Bw. Deogratius Dotto.
Mshereheshaji wakati wa Kongamano hilo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bi. Suzane Mzee akiwajibika.
Maafisa Mambo ya Nje wakifuatilia hotuba ya Mhe. Rais.


Mhe. Rais Kikwete akizindua rasmi Tovuti ya Diaspora wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kwanza la Diaspora. Wanaoshuhudia wengine ni Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda.
Mwonekano wa Tovuti hiyo inayoitwa www.tanzaniadiaspora.org   
Mhe. Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Mhe. Pinda, Mama Jairo, Mkurugenzi wa Tanzania Diaspora Initiative na Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) hapa nchini Bw. Damien Thuriaux
Mhe. Rais Kikwete na Mhe. Pinda katika picha ya pamoja na kundi la Wanadiaspora kutoka nchi za Ulaya
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa mara baada ya ufunguzi rasmi wa Kongamano la Kwanza la Diaspora nchini.

Picha  na Reginald Philip








No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.