Monday, August 11, 2014

Watanzania waishio Visiwa vya Comoro waanzisha rasmi jumuiya yao.

Mhe. Balozi Kilumanga pamoja na watendaji wa Ubalozi wakifuatilia mkutano.

Sehemu ya Watanzania wanaoishi Comoro wakifuatilia hotuba ya Mhe. Balozi Kilumanga.

Viongozi wapya wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Kilumanga. Mwenye kanzu kushoto mwa Balozi, ni Bw. Salum Ali Abdallah (Mwenyekiti), wakulia kutoka alipo Balozi ni Bw. Khalfan Salum Khalifan (Makamu Mwenyekiti), anayefuatia kulia ni Bibi Rukia Selemani (Katibu).


Jana tarehe 10 Agost 2014, Watanzania wanaoishi katika Muungano wa Visiwa vya Comoro walianzisha rasmi Jumuiya yao. Lengo la kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ni kuwaunganisha wanachama wake, kuwawezesha kushirikiana katika kutambua fursa za maendeleo na kutoa mchango kwa taifa lao la Tanzania.

Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ubalozi wa Tanzania, Moroni. Wakati akifungua mkutano huo, Mhe. Chabaka Kilumanga, Balozi wa Tanzania nchini Comoro aliwaeleza Watanzania hao kwamba Serikali ya Tanzania inathamini sana na kutambua umuhimu wao Serikali imeanzisha Idara inayoshughulikia Watanzania wanaoishi Ughaibuni katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Aidha, Kitengo kama hicho kimeanzishwa katika Ofisi ya Rais wa Zanzibar. Sambamba na hilo, Viongozi wote wamekuwa wakikutana na Watanzania wanaoishi Ughaibuni, kila wanapopata fursa ya kufanya hivyo, wanapokuwa nje ya nchi. Mkuu wa Utawala wa Ubalozi, Nd. Ali Jabir Mwadini alitoa mada kuhusu misingi ya uanzishaji wa Jumuiya za Kiraia na kubainisha vipengele muhimu vinavyopaswa kuzingatiwa hususani katika katiba ya Jumuiya.
Mwisho, ulifanyika uchaguzi wa viongozi wa muda waliopewa jukumu la kuandaa katiba.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.