Sunday, August 24, 2014

Mhe. Membe Amwakilisha Rais Kikwete Michezo ya Shule Afrika Mashariki

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akitoa hotuba kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Uzinduzi wa mashindano ya michezo ya shule za Sekondari za Afrika Mashariki yajulikanayo kama (FEASSA) leo katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga (kulia) akifuatilia kwa makini hotuba kutoka kwa Waziri Membe. 
Viongozi mbalimbali wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri Membe kwaniaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard K. Membe akiwapungia mkono wanafunzi wa Shule za Sekondari kutoka Tanzania bara (hawapo pichani).
Wanafunzi wa Shule za Sekondari kutoka Tanzania ambao wanashiriki mashindano ya Shule za Sekondari za Afrika Mashariki wakiwa kwenye maandamano ya uzinduzi wa mashindano hayo leo katika Uwanja wa Taifa
Waziri Membe akipiga Mpira kuashiria kufunguliwa kwa mashindano hayo rasmi
Waziri Membe akisalimiana na wachezaji wa mpira wa miguu kutoka Shule ya Sekondari ya Makongo kabla ya kuanza mechi.
Waziri Membe akisalimiana pia na wachezaji wa shule ya Sekondari ya Mvara kutoka Uganda.
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa Stars ya Tanzania Martinus Ignatus 'Mart Nooij' (mwenye kofia) naye akiangalia kwa makini mechi kati ya timu ya Makongo Sekondari na Mvara (hawapo pichani) katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
Mechi ikiendelea
Waziri Membe akishangilia baada ya Makongo Sekondari kufunga goli.
Wachezaji wa Makongo Sekondari wakishangilia goli lao
Picha na Reginald Philip
 -------------------------------------------------------------------------------------------


Mhe. Membe Amwakilisha Rais Michezo ya Shule A. Mashariki



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), alimwakilisha Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufungua Mashindano ya 13 ya Shirikisho la Vyama vya Michezo vya Shule za Sekondari za Afrika Madhariki (FEASSSA), jijini Dar es Salaam Jana.


Mashindano hayo yanahisisha timu za michezo mbali mbali za Shule 205 kutoka Kenya, Uganda, Sudani Kusini, Rwanda, Burundi, Zanzibar na Tanzania Bara, zenye washiriki 3,000.

Mashindano yatarindima kwenye Uwanja wa Taifa kwa siku 10.
Katika hotuba iliyosomwa na Mhe. Membe, Rais Kikwete alisema michezo hiyo ni moja ya mikakati ya utekelezaji wa itifaki ya utengamano wa Afrika Mashariki.
"Aidha, michezo hii ni kiashiria tosha cha azma madhubuti tuliyo nayo ya kuimarisha Umoja wetu," alisema.

Alizitaka Nchi za Afrika Mashariki kushirikiana kuendeleza michezo, akashauri Mashindano hayo yashirikishe pia Shule za msingi.

"Kwa niaba ya Marais wa Nchi za Afrika Mashariki, na kwa niaba ya Nchi yangu, napenda kuwahakikishia kuwa serikali za nchi zote zitaendelea kuwainga mkono na kuwezesha michezo hii kufanyika kila mwaka," alisema.

"Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Mhe. Hawa Ghasia, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa); Mhe. Dkt. Shukururu Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi; Dkt. Abdullah Juma Abdullah, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mawaziri kutoka Sudani Kusini na Uganda.









No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.