Thursday, August 28, 2014

Ziara ya Mhe. Naibu Waziri nchini Singapore

Mhe. Dkt.  Mahadhi Juma Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa kwenye mazungumzo na mwenyeji wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara Mhe. Kasiviswanathan Shanmugam, Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore. 
Mhe. Dkt.  Mahadhi Juma Maalim (wa pili kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. Kasiviswanathan Shanmugam, Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore (wa tatu kushoto), Balozi Mbelwa Kairuki (kulia) na Mhe. John Kijazi (kushoto), Balozi wa Tanzania nchini India na Singapore.  

Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mawaziri saba wa Mambo ya Nje wa Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara wakiwa na mwenyeji wa Mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore Mhe. Kasiviswanathan Shanmugam (wa tano kutoka kushoto). 
Mawaziri wa Mambo ya Nje wakiwa kwenye ziara kwenye mojawapo ya vyuo maalum nchini Singapore Institute of Technical Education ambapo Tanzania inashirikiana nacho kwenye kutoa mafunzo kwa walimu wa VETA. 

 ....Ufunguzi wa Ubalozi wa Heshima wa Tanzania nchini Singapore

Mhe. Dkt.  Mahadhi Juma Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (kushoto) akikata utepe kufungua rasmi ofisi za Ubalozi wa Heshima za Tanzania nchini Singapore akishirikiana na Mhe. S.S. Teo, Balozi wa Heshima. Kulia ni Mhe. John Kijazi, Balozi wa Tanzania nchini India ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Singapore.
Mhe. Dkt.  Mahadhi Juma Maalim (wa pili kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. John Kijazi (wa kwanza kushoto), Balozi wa Tanzania nchini India ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Singapore, Mhe.S.S. Teo, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Singapore na Balozi Mbelwa Kairuki, Murugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.