Friday, July 10, 2015

Wizara ya Mambo ya Nje yamuaga Balozi wa Palestina

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano  wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya akimkabidhi picha yenye mchoro wa Mlima Kilimanjaro Balozi wa Palestina aliyemaliza muda wake wa uwakilishi nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Nasri Abu Jaish. Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa heshima yake na Wizara ya Mambo ya Nje.
Balozi Simba akitoa neno la shukrani kwa Balozi wa Palestna nchini.
Picha juu na chini ni Mabalozi wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Simba (Hayupo pichani)
Balozi Jaish akitoa neno la shukrani kwa ushirikiano na upendo aliokuwa akipata kutoka Wizarani na kwa watanzania kwa ujumla.  
Balozi Jaish akiendelea kuongea. 
Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba akimpongeza Balozi Jaish mara baada ya kumaliza kuzungumza
Balozi Jaishi akimkabidhi Balozi Simba zawadi ya Picha yenye mfano wa Nyumba ya Ibada (Msikiti)
Naibu Kaitbu Mkuu Balozi Hassan Simba Yahya akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Palestina aliyemalimaliza muda wake wa uwakilishi nchini Tanzania.
Balozi Simba (Wa tatu kutoka kushoto), Balozi Jaish (Wa nne Kutoka kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Joseph Sokoine (Wa pili Kutoka Kushoto), Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Bwa. Elibariki N. Maleko, wa kwanza, wapili na watatu ni Maafisa Mambo ya Nje.


Picha na Reginald Philip

Thursday, July 9, 2015

MEMBE ASISITIZA UMUHIMU WA VIWANDA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb.), akiongea kwenye muhadhara kabla ya Mtoa mada mkuu Prof. Justin Yifu Lin hajaongea katika muadhara uliokuwa unazungumzia umuhimu wa viwanda nchini ulioandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje 
Makamu wa Rais wa zamani wa Benki ya Dunia, Prof. Justin Yifu Lin akitoa mada yake juu ya uwanzishaji wa viwanda nchini Tanzania katika muadhara ulioandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya (Kulia), na kushoto ni Balozi Mstaafu Mhe. Elly Mtango wakisikiliza kwa makini mada iliyokuwa ikitolewa na Dkt. Lin (hayupo pichani). 
Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje wakimsikiliza kwa makini Prof. Lin (hayupo pichani), Katikati ni Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Nigel Msangi, Kushoto ni Afisa Mawasiliano mwandamizi wa Mambo ya Nje Bw. Ally Mkumbwa nao wakifuatilia kwa makini Muhadhara uliokuwa ukiendelea 
Balozi Simba akichangia mada katika muadhara uliokuwa ukiendelea  
Muhadhiri Chuo cha Diplomasia Bw. Innocent Shoo akiuliza swali 
Afisa Mambo ya Nje Bi. Felisita Rugambwa naye akiuliza swali katika muhadhara 
Dkt Lin akijibu maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kulizwa.
Picha ya juu na chini ni watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje nao wakisikiliza mada kwa makini
KKatibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akitoa neno la shukrani kwa Prof. Lin, kwa niaba ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje mara baada ya kumalizika kwa muhadhara huo
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akizungumza jambo huku akisikilizwa na Prof. Lin (Kulia) na Mhe. Membe (Katikati). 
Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Diaspora Bi. Rosemary Jairo akizungumza jambo kwa Prof. Lin (kushoto) na Katibu Mkuu Balozi Mulamula.

Picha na Reginald Philip



  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe, amesema upatikanaji wa gesi ni nyenzo muhimu ya uendelezaji wa viwanda vya kati ili kutengeneza ajira na kuharakisha maendeleo ya nchi.

Mhe. Membe alipongeza uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kuichagua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tatu za Afrika itakapohamishia baadhi ya viwanda vyake, akazitaka taasisi za uwekezaji na uendelezaji wa viwanda kuweka mikakati madhubuti ya kutumia fursa hiyo kikamilifu.

Mhe. Waziri alisema hayo leo wakati wa mhadhara wa aliyekuwa Mchumi Mkuu na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Prof. Justin Yifu Lin, kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar Es Salaam, uliohudhuriwa na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na wadau wengine.

Alisema uendelezaji wa viwanda lazima utiliwe mkazo katika mpango wa Tanzania kuingia uchumi wa kati 2025. "Tuache kukimbilia viwanda vikubwa vinavyohitaji mitaji mikubwa, ambayo hatuna.Tuchague viwanda vya kati vitakavyoajiri watu wengi kwa uwekezaji wa wastani."

Mhe. Membe alisema uendelezaji wa viwanda usambae nchi nzima ili kuvutia vijana kuishi vijijini badala ya kukimbilia mijini. "Sasa hivi nchi yetu ina viwanda takriban 3,000 lakini zaidi ya theluthi mbili viko Dar Es Salaam. Lazima umeme upelekwe vijijini kuleta uwiano wa maendeleo ya viwanda," alisisitiza.

Katika mhadhara wake, Prof. Lin alisema nchi nyingi zinazoendelea zilifanya maamuzi yasiyo sahihi kuhusu viwanda. "Nchi nyingi zilifuata kile kinachoitwa Muafaka wa Washington na kuanzisha viwanda vikubwa kwa maelekezo ya nchi tajiri, ambavyo viliwashinda kuendesha kwa kuwa vilihitaji uwekezaji mkubwa sana."

Alisema nchi za Asia zilizoendelea kwa haraka ni zile zilizoamua kuzingatia mazingira halisi na kwenda hatua kwa hatua katika kuanzisha viwanda. "Hii iliimarisha uchumi wao na kuukuza."

Prof. Lin alisema serikali zina wajibu wa kusimamia uendelezaji wa viwanda kwa kuweka sera sahihi, kuhimiza uwekezaji kwenye uzalishaji wa bidhaa zenye masoko ya uhakika na kusaidia sekta binafsi ishiriki kikamilifu.

Akiongelea Tanzania, Mchumi huyo wa Kichina alisema ingawa gharama za ajira ziko chini, gharama za uendeshaji ziko juu, hivyo hazivutii uwekezaji. Alisema moja ya sababu kubwa za Shilingi ya Tanzania kushuka thamani ni uuzaji mdogo wa bidhaa nchi za nje.

(mwisho)

Monday, July 6, 2015

Rais Kikwete aongoza Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa EAC kuhusu Burundi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na baadhi ya Wawakilishi wa Wakuu wa Nchi Wanachama wakiimba Wimbo wa Jumuiya  hiyo tayari kwa kuanza Mkutano wao Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 06 Julai, 2015.
 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt.Richard Sezibera akisoma Maazimio  yaliyofikiwa katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa EAC huku Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Rais Kikwete (wa tano kutoka kushoto waliokaa) pamoja na viongozi wengine wakisikiliza kwa makini. Pamoja na mambo mengine Wakuu wa Nchi wamemteua Rais Museveni kusimamia majadiliano ya makundi yanayopingana nchini Burundi na Uchaguzi wa Rais ufanyike tarehe 30 Julai, 2015 badala ya tarehe 15 Julai mwaka huu.
 Katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula (katikati) kwa pamoja na  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki, Bi.Joyce Mapunjo (kulia) pamoja na wajumbe wengine waliohudhuria mkutano huo wakiimba wimbo wa Jumuiya.
  Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Chirau Ali Mwakere pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Kenya, Mhe. Phyllis Kandie 

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bundala akiwa na Wajumbe wengine kabla ya mkutano kuanza
 Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe.Ali Siwa (katikati) na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe.Ladislaus Komba (kulia)  wakati wa mkutano huo.
 Afisa Mwandamizi kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi, Bi. Victoria Mwakasege akiwa na Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais wakisikiliza maazimio ya wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yakisomwa.
 Afisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw.Mkumbwa Ally akijadiliana jambo na Afisa wa Mambo ya Nje, Bi.Samira Diria muda mfupi kabla ya mkutano huo kuanza.
Sehemu ya Wajumbe waliohudhuria mkutano huo uliofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam.
Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
 Picha ya pamoja.

Picha na Reuben Mchome
==================================

Wakuu wa Nchi wa EAC wamteua Rais Museveni kusimamia majadiliano nchini Burundi

Mkutano wa Tatu wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kujadili hali ya kisisasa nchini Burundi umefanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Julai, 2015 chini ya Uenyekiti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Katika Mkutano huo ambao umehudhuriwa pia na Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni na Mawaziri wa Mambo ya Nje na wale wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka nchi zote wanachama, umeazimia masuala mbalimbali kwa ajili ya kuhakikisha hali ya kisiasa na utulivu  nchini Burundi inarejea.

Katika mkutano huo, Wakuu wa Nchi wamemteua Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kusimamia majadiliano ya makundi yanayopingana nchini Burundi.

Pia wakuu hao wa nchi wameitaka Serikali ya Burundi kuyanyang’anya silaha makundi yote nchini humo kikiwemo kikundi kinachojiita Imbonera Kure”. Aidha, wameomba Umoja wa Afrika (AU) usimamie zoezi hili kwa kupeleka Timu ya Waangalizi wa Kijeshi ili kuhakikisha linafanikiwa. 

Azimio jingine ni kuvitaka vyombo vya usalama chini ya Sekretarieti ya Maziwa Makuu (ICGLR) kutafiti na kuhakiki uwepo wa kikundi cha waasi cha FDLR nchini Burundi.

Aidha, Wakuu wa Nchi wameitaka Serikali ya Burundi kuahirisha Uchaguzi wa Rais  uliopangwa kufanyika tarehe 15 Julai, 2015 na sasa ufanyike tarehe 30 Julai, 2015 ili kutoa muda kwa msuluhishi kusimamia majadiliano kama ilivyopangwa.

Wakuu hao wa nchi pia wametaka yeyote atakayeshinda nafasi ya Urais nchini Burundi kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayojumuisha vyama vilivoshiriki kwenye Uchaguzi na vile ambavyo havikushiriki.

Pia, Wakuu wa nchi wameitaka Serikali ya Burundi kuheshimu Mkataba wa Amani na Maridhiano wa Arusha wa mwaka 2000 na kutoifanyia marekebisho ya aina yoyote Katiba ya Burundi.

Vilevile, Wakuu hao wa nchi wameiomba AU kuidhinisha na kupitisha maamuzi haya ya EAC na kwamba Jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki itatuma Timu ya Waangalizi katika Uchaguzi wa Rais nchini Burundi.

-Mwisho-








Rais Museni awasili nchini kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC

Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Museveni yupo nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu hali ya kisisasa nchini Burundi utakaofanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 06 Julai, 2015.
Mhe. Rais Museveni akisilimiana na Wakuu wa Vyombo vya Usalama waliofika Uwanjani kumpokea.
Mhe. Rais Museveni akiongozana na mwenyeji wake Waziri Membe mara baada ya kuwasili
Mhe. Rais Museveni akikagua Gwaride la Heshima
Rais Museveni kwa pamoja na Waziri Membe wakifuatilia burudani kutoka kwa moja ya kikundi kilichokuwepo uwanjani hapo kwa mapokezi
Mhe. Rais Museveni akimsikiliza Mhe. Membe  katika mazungumzo mafupi kabla ya kuondoka Uwanjani hapo. Wengine katika picha ni Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Ladislaus Komba (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Sofia Mjema (mwenye kitambaa kichwani) na Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Uganda hapa nchini.

Picha na Reginald Philip


Sunday, July 5, 2015

Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa EAC wafunguliwa Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb.) akifungua Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki ambao pamoja na mambo mengine utapokea na kujadili taarifa ya ziara ya Mawaziri nchini Burundi kuhusu hali ya kisisasa nchini humo. Mkutano huo ambao ni maandalizi ya Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi utakaofanyika tarehe 06 Julai, 2015, umefanyika kwenye Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Julai, 2015.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Dkt. Richard Sezibera naye akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Joyce Mapunjo wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nao wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa Mkutano huo
Waziri wa Afrika Mashariki nchini Rwanda, Mhe. Valentine Rugwabiza (wa pili kushoto)  pamoja na wajumbe wengine waliohudhuria Mkutano huo. 
Balozi wa Tanzana nchini Burundi Mhe. Rajab Gamah (Kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Mhe. Henry Okello Oryem 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bundara (Kushoto) akiwa na  Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi, Bi. Victoria Mwakasege wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri.
Maafisa Mambo ya Nje nao wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri. Kutoka kushoto ni Bw. Ally Ubwa, Bi. Grace Martin na Bw. Mudrick Soraga
Mkutano ukiendelea

Picha na Reginald Philip

Friday, July 3, 2015

Rais Kikwete aweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa jengo la MICT

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (mwenye tai nyejundu) akiwa pamoja na viongozi mbalimbali katika eneo la Lakilaki jijini Arusha linalojengwa jengo la taasisi ya Mechanism for International Criminal Tribunals (MICT) inayorithi shughuli za Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR). Mhe. Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi huo jijini Arusha tarehe 01 Julai 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wa tano kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali na viongozi wa Umoja wa Mataifa waliopo Arusha na waliomwakilisha Katibu Mkuu wa Umoja huo katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi


Balozi Irene Kasyanju, Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje (wa pili kulia), Bi. Tully Mwaipopo, Afisa wa Uabalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa pamoja na Amer Jandu wa pili kutoka kushoto na Bw. Samuel Akorimo, Afisa Mkuu wa MICT, Arusha wakiwa eneo la Lakilaki. Bw. Jandu ni mmiliki wa kampuni ya kitanzania iliyoshinda kandarasi ya kujenga jengo hilo.


Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda wa kwanza kulia na Balozi Kasyanju wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa mbele ya jiwe la msingi lililowekwa na Rais Kikwete.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Hassan Simba Yahya wa pili kushoto, Balozi Kasyanju, Balozi Mushy na Bw. Akorimo wakikagua eneo la ujenzi kabla ya shughuli za uwekaji wa jiwe la msingi kuanza.