Wednesday, August 12, 2015
Tuesday, August 11, 2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
UTEUZI
NA UHAMISHO WA MABALOZI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Joseph B. Masikitiko kuwa
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kabla ya uteuzi huo Ndugu
Masikitiko alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo (TBS).
Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Balozi
mmoja na kuwabadilishia vituo vya kazi Mabalozi wawili kama ifuatavyo:
(i)
Lt.
Gen. Charles L. Makakala, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania
nchini Zimbabwe. Kabla ya uteuzi huo Lt. Gen. Makakala alikuwa Mkuu wa Chuo cha
Taifa cha Ulinzi (National Defence
College).
(ii) Balozi Wilson Masilingi
aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi amehamishwa kwenda kuwa Balozi wa
Tanzania nchini Marekani kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Liberata
Mulamula aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje ya
Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa. Atakuwa pia anaiwakilisha Tanzania nchini
Mexico
(iii)
Balozi Irene Kasyanju
aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi kushika nafasi
inayoachwa wazi na Balozi Wilson Masilingi.
Taarifa
iliyotolewa leo, Jumanne, Agosti 11, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi
Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Uteuzi na uhamisho huu unaanzia
tarehe 07 Agosti, 2015.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
11 Agosti, 2015
Monday, August 10, 2015
Katibu Mkuu amuaga rasmi Balozi wa Finland aliyemaliza muda wa kazi nchini
Balozi Mulamula akiendelea kuzungumza. |
Sehemu ya Wageni walioudhuria hafla hiyo wakimsikiliza Balozi Mulamula (hayupo pichani). |
Balozi Antila akiendelea Kuzungumza |
Balozi Mulamula na Balozi Antila wakitakiana afya njema kwa kugonganisha Glasi |
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga ambaye alikuwa mshereheshaji wakati wa hafla hiyo akizungumza. |
Balozi Mulamula akimkabidhi zawadi ya picha ya Mlango wa Zenji Balozi Antila. |
Wageni waliohudhuria Hafla hiyo wakifurahia kwa kupiga makofi wakati Balozi Mulamula akimkabidhi Balozi Antila zawadi ya picha (Hawapo pichani). |
Balozi Mulamula (Wa pili kulia), Balozi Mpango (Wa kwanza kushoto), Balozi Antila (Wa pili kutoka kushoto), na Balozi Sokoine wakiwa katika picha ya pamoja. |
Balozi Mulamula na Balozi Antila wakiwa katika Picha ya Pamoja na wageni walioudhuria hafla hiyo.
Picha na Reginald Philip
|
Mkurugenzi wa Ushirikano wa Kimataifa awashauri vijana kufanya kazi na Mashirika ya Kimataifa
Juu na Chini ni picha ya Vijana waliohudhuria Kongamano hilo wakimsikiliza Balozi Mushy (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada. |
Balozi Mushy akimwelezea jambo Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi katika Kongamano la Vijana |
Friday, August 7, 2015
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika akutana na Ujumbe wa EU nchini
Sehemu ya Ujumbe huo kutoka Umoja wa Ulaya hapa wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Sokoine na Balozi Kochanke |
Afisa Mambo ya Nje, Bi Felista Rugambwa (wa kwanza kushoto) akinukuu mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kwenye Mkutano huo. |
Mkutano ukiendelea |
Picha na Reginald Philip.
Wednesday, August 5, 2015
Waziri Membe amuaga rasmi Balozi wa Hispania aliyemaliza muda wa kazi nchini
Sehemu ya Mabalozi na wagenui waalikwa wakimsikiliza Balozi Luis (hayupo pichani) |
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine akizungumza machache wakati wa hafla hiyo |
Mhe. Waziri Membe kwa pamoja na Mhe. Balozi Luis, Mabalozi na wageni waalikwa wakimsikiliza Balozi Sokoine ambaye haonekani pichani |
Bi. Kasiga ambaye alikuwa mshereheshaji wakati wa hafla hiyo akizungumza |
Balozi Luis akimweleza jambo Waziri Membe |
Maafisa Mambo ya Nje walioshiriki hafla hiyo. Kushoto ni Bi. Olivia Maboko na Bi. Tunsume Mwangolombe Mhe. Membe na Mhe. Luis wakitakiana afya njema |
Mhe. Membe akimkabidhi zawadi Balozi Luis |
Waziri Membe akizungumza na Balozi Luis |
Waziri Membe akiagana na Balozi Luis mara baada ya hafla hiyo |
Balozi Luis akiagana na Balozi Sokoin |
Picha ya pamoja |
Friday, July 31, 2015
Marais wastaafu wajadili uongozi wa Afrika
MARAIS WASTAAFU
WAJADILI UONGOZI WA AFRIKA
Marais wastaafu wa nchi sita za Afrika wamekutana Jijini Dar es
Salaam jana kutafakari mustakabali wa Bara lao wakizingatia mabadiliko ya
kiuchumi, kisiasa na kiteknolojia ulimwenguni. Mjadala huo ulioitishwa na Rais
Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Benjamin Mkapa, ulifunguliwa rasmi na Rais wa Uganda,
Mhe. Yoweri Museveni.
Ulihudhuriwa na Marais Wastaafu wa Nigeria, Mhe. Olusegun
Obasanjo, Ghana, Mhe Jerry Rawlings, Malawi, Mhe. Bakili Muluzi; Botswana, Mhe.
Festus Mogae, na Namibia, Mhe. Hifikepunye Pohamba.
Marais wastaafu pamoja na wanazuoni na watu mashuhuri wa Afrika walisisitiza
muhimu wa kujenga mtangamano wa bara hilo ili kuleta maendeleo ya haraka ya
kiuchumi. Washiriki walikubaliana kuwa juhudi za pamoja zifanywe kudhibiti
vikwazo dhidi ya mtangamano, ikiwa ni pamoja na historia ya tawala tofauti za
kikoloni; elimu na teknolojia duni, na ukosefu wa utashi wa kisiasa.
Pamoja na kusifia hatua zilizofikiwa kuboresha demokrasia
barani Afrika, washiriki walisema maendeleo ya uchumi yanahitaji kasi kubwa
zaidi ili wananchi wafaidike na rasilimali nyingi zilizopo.
Uongozi wa nchi za Afrika ulikosolewa kwa kushindwa kutoa
kipaumbele kwa maendeleo ya kiuchumi na kuzembea utekelezaji wa maamuzi
yanayochukuliwa kwenye majukwaa mbalimbali ya pamoja, kama vile Umoja wa Afrika
na Jumuiya za Maendeleo za kikanda.
Ilishauriwa jumuiya za kikanda ziimarishwe kwa kutengewa
rasilimali za kutosha na kupewa uwezo zaidi wa kufanya maamuzi ili
ziwe misingi ya kujenga umoja wa kiuchumi.
Washiriki walisifia Mpango Mkakati wa Umoja wa Afrika wa kulifanya
bara hilo liongoze duniani kiuchumi na kiteknolojia ifikapo mwaka 2063,
lakini wakasisitiza uwekwe mpango madhubuti wa utekelezaji ili kufikia azma
hiyo.
Katika hotuba yake, Rais Museveni alisema Afrika inayo misingi imara
ya umoja. Alitupilia mbali madai kuwa bara hilo lina mgawanyiko mkubwa wa
kijamii. "Bara hili lina makundi manne tu ya kilugha," alisema.
Kiongozi huyo wa Afrika Mashariki alihimiza juhudi zaidi kuleta
mtangamano wa kiuchumi na kisiasa Afrika. "Lazima tujenge mtangamano wa
kiuchumi. Pale inapowezekana, tuungane kisiasa pia."
Alisema Afrika ilitawaliwa na wakoloni kwa sababu haikuwa na
mtangamano, kitu kinacholifanya bara hilo liendelee kubaki nyuma kimaendeleo.
Alitaka hatua za pamoja zichukuliwe kuendeleza viwanda na maliasili za Afrika,
ikiwapo madini, mafuta na gesi.
Jana usiku, Mhe. Mkapa aliwaandalia wageni wake hafla ya chakula cha jioni ambapo pia Jukwaa la Uongozi
Afrika lilikabidhi zawadi kwa washidi wa shindano la kuandika insha lililoshirikisha
vijana 522 kutoka nchi 11 za bara hilo.
Mshindi wa kwanza ni Munyaradzi Shifetete kutoka Zimbabwe, ambaye
alikabidhiwa cheti na fedha taslim. Wengine waliokabidhiwa zawadi na Rais
Mstaafu wa Botswana, Mhe. Mogae, ni Vicky Mbabaazi kutoka Uganda, Sholopelo
Sholopelo kutoka Botswana, Joseph Wanga kutoka Kenya na Omolo Juema kutoka
Uganda.
(mwisho)
Press Release
H.E Simonetta Sommaruga, President of Switzerland
PRESS RELEASE
H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to H.E. Simonetta Sommaruga, President of the Swiss Confederation on the occasion of the National Day of Switzerland on 1st August, 2015.
The message reads as follows;
“H.E. Simonetta Sommaruga,
President of the Swiss Confederation,
Bern,
SWITZERLAND
Your Excellency,
It is my pleasure and privilege to extend to you, my heartfelt congratulations on the occasion of your country’s National Day. As you celebrate this important occasion, allow me to take this opportunity to express my gratitude on the good relations that exist between our two countries and peoples.
The Government of Tanzania highly values the existing ties and is ready to work with the Government of Switzerland in deepening the friendship between our two countries and strengthening collaboration in bilateral and multilateral frameworks.
Please accept, Your Excellency, my best wishes for your personal good health and continued peace and prosperity for the people of Switzerland”.
Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam
31st July 2015
Kaimu Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana kwa mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC
Balozi Simba akizungumza na Dkt. Tax |
Mkutano ukiendelea |
Naibu Katibu Mkuu Balozi Simba (Kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)
Picha na Reginald Philip
|
Subscribe to:
Posts (Atom)