Wednesday, March 2, 2016

Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa UNESCO kwa upande wa Afrika atembelea Wizara ya Mambo ya Nje

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa UNESCO kwa upande wa Afrika, Bw. Firmin Matoko walipokutana kwa ajili ya mazungumzo kwenye Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje.


Balozi Mushy akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa UNESCO kwa upande wa Afrika, Bw. Firmin Matoko. Mazungumzo hayo pamoja na Mambo mengine yalijikita katika vipaumbele vya UNESCO ambavyo ni elimu na jinisia. Kwa upande wa elimu, Balozi Mushy alieleza hatua ya Serikali ya awamu ya tano kutoa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari. Kuhusu jinsia, alieleza hatua ya Serikali ya kujumuisha wanawake katika nafasi za uongozi ikiwa ni pamoja na kuimchagua Makamu wa Rais Mwanamke wa kwanza. Mwingine katika picha ni Mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues.

Wajumbe wakiendelea na mazungumzo


Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Ngusekela Nyerere na Afisa wa UNESCO wakinukuu mambo muhimu ya mazungumzo.


Balozi Mushy akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Bw. Matoko.


Picha ya pamoja.

Friday, February 26, 2016

Waziri Mahiga arudisha Fomu Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga  akiwasili katika Jengo la Sukari "Sukari House" zilipo Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ili kuweza kukabidhi Fomu za Uadilifu na Tamko la Mali kwa Viongozi kama taratibu za Maadili ya Utumishi wa Umma zinavyowataka viongozi wote wa Umma kukamilisha zoezi hilo mara baada ya kuingia madarakani.
Waandishi wa Habari wakimuhoji Mhe. Waziri Mahiga mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ambapo Mhe. Waziri Mahiga alieleza kuwa ujazaji wa fomu hizo ni taratibu za kawaida za kiutumishi na kwa upande wake ameshawahi kujaza fomu hizo mara kadhaa katika Utumishi wake hivyo kwa sasa anahuisha taarifa zake.
Waziri Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga walipokutana katika Ofisi za Sekretarieti ya Uongozi wa Maadili ya Umma katika zoezi la kukabidhi fomu za Uadilifu na Tamko la Mali, kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga.




Waziri Mahiga aongoza maadhimisho ya Siku ya Taifa la Kuwait

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akizungumza katika hafla  ya kusheherekea Siku ya Taifa la Kuwait iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Februari, 2016. Kushoto ni Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al Najem. Katika hotuba yake Waziri Mahiga alilipongeza Taifa la Kuwait kwa kuendeleza mahusiano mazuri kati yake na Tanzania  katika sekta mbalimbali zikiwemo za biashara, kilimo na maj.
Waziri akiendelea kuhutubia
Balozi Al Najem naye akizungumza katika hafla hiyo.


Sehemu ya Mabalozi na viongozi mbalimbali kutoka Serikalini wakisikiliza hotuba  zilizotolewa na Mhe.Dkt. Mahiga na Mhe. Al Najem (hawapo pichani). 
Waziri Mahiga (kulia) akisalimiana na Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi ambaye alihudhuria hafla hiyo.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Mhe. Mwinyi.   
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na  Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al Najem.
Waziri Mahiga  kwa pamoja na Balozi Al Najem na Mabalozi wengine  wakishiriki kukata keki kama ishara ya kuadhimisha wakati wa hafla hiyo. Anayeshhudia pembeni ni Rais Mstaafu Mhe.Mwinyi. 
Picha ya pamoja

Picha na Reginald Philip 



Rais wa Guinea Bissau Kushirikiana na Serikali ya Tanzania


Thursday, February 25, 2016

TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA JPC NA ZAMBIA


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Ramadhan Mwinyi akifungua rasmi Mkutano wa JPC kati ya Tanzania na Zambia.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimaendeleo na Mashirika ya Kimataifa, Bw. Sylvester Mundanda  ambaye alimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya nchini Zambia akiwasilisha ujumbe wa Serikali ya Zambia katika mkutano huo. 
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Samuel Shelukindo akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Ramadhan Mwinyi hayupo pichani ili aweze kufanya ufunguzi wa Mkutano huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchini Zambia, Bi. Angela Mulenga ambaye aliambatana na ujumbe wa maafisa walioiwakilisha Serikali ya Zambia katika Mkutano huo akijadili jambo na Bw. Sylvester Mundanda.
Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Mhe. Judith Kapijimanga (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Balozi Grace Mujuma wakijadili jambo wakati wa mkutano huo.
 Sehemu ya maafisa wa Serikali ya Zambia wakifuatilia Mkutano.

Sehemu ya maafisa wa Serikali ya Tanzania wakifuatilia Mkutano.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga  akiwakaribisha wageni waalikwa ambao ni Viongozi na Maafisa wa Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zambia katika Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia (JPC) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa muda wa siku mbili kuanzia leo.
===============================================================================

         Serikali za Tanzania na Zambia zinakutana katika kikao cha siku mbili kujadili na kukubaliana maeneo ya ushirikiano ambayo watayasimamia  kwa pamoja kwa lengo la kuongeza kasi ya maendeleo ya nchi hizo mbili. Kikao hicho kinachojulikana kama Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia (JPC) kinafanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuanzia leo.

         Katika hotuba yake ya ufunguzi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi alieleza kuwa uhusiano wa Tanzania na Zambia ni mzuri na kufanyika kwa kikao hicho ni uthibitisho dhahiri.

 Aidha, Balozi Mwinyi  alieleza kuwa kufanyika kwa kikao hicho kunatoa fursa kwa wajumbe kuchambua kwa pamoja hatua zilizofikiwa na changamoto  zilizojitokeza katika utekelezaji wa maeneo yaliyoafikiwa wakati wa kikao cha 8 cha JPC kilichofanyika Lusaka Juni 2006. Maeneo hayo ni pamoja na biashara, viwanda, mawasiliano, uchukuzi, nishati, uhamiaji, kilimo, elimu, michezo, madini, utalii, maliasili na utamaduni.

“Haya ni baadhi ya maeneo ambayo nchi zote mbili zinayapa umuhimu mkubwa ili kuharakisha maendeleo ya pande zote mbili Katika majadiliano yetu tutalenga zaidi maeneo haya ili tubuni utaratibu mzuri wa kushirikiana katika utekelezaji kwa lengo la kuleta tija kwa nchi na wananchi wake”. Balozi Mwinyi alifafanua.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimaendeleo na Mashirika ya Kimataifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Zambia, Bw, Sylevester Mundanda alieleza kuwa Tanzania na Zambia zimejaliwa kuwa na maliasili lukuki kama vile ardhi, madini, maji na wanyama pori, hivyo, endapo kama zitatumiwa vizuri zinaweza kubadilisha uchumi wa nchi hizo kwa ajili ya kuwaletea maisha bora wananchi wake.

Alisisitiza umuhimu wa kukubaliana maeneo machache ya kipaumbele na kuyawekea mikakati ya utekelezaji na ubunifu bila kusahau kujiwekea utaratibu wa kupima ufanisi kila baada ya muda. 

Bw, Mundanda alihitimisha kwa kusema kuwa vikao vya JPC ni fursa nzuri kujadili changamoto za kiuchumi na kubuni mikakati ya pamoja kukabiliana nazo ili uchumi uweze kukua kwa faida ya wananchi wa pande zote.

Wednesday, February 24, 2016

Press Release


The President of the United Republic of Tanzania, H.E Dr. John Pombe Joseph Magufuli has sent congratulatory message to the President of the Republic of Uganda, H.E Yoweri  Kaguta Museveni following his re-election as the President at the election held on February 18th 2016. The message reads as follows:

“H.E. Yoweri Kaguta Museveni,
President-Elect of the Republic of Uganda,
KAMPALA.

Your Excellency and Dear Brother,
It gives me great pleasure, on behalf of the Government and people of the United Republic of Tanzania and indeed on my own behalf, to extend to Your Excellency our heartfelt congratulations on your re-election as the President of the Republic of Uganda. Your re-election at the helm of your country is a true reflection of the confidence that the people of Uganda have in you as well as a testimony of their trust in your exemplary leadership.
I also take this opportunity to congratulate your party, National Resistance Movement for its outstanding victory in the General Elections. As you are well aware, both my party, Chama Cha Mapinduzi (CCM) and the Government of the United Republic of Tanzania have enjoyed brotherly relations with the Ugandan people throughout the years. 
While congratulating you on your well deserved re-election, I wish to reaffirm my readiness and determination to continue working with you in further strengthening our relations for the benefit of our two countries and peoples.
Please accept, Your Excellency and Dear Brother, the assurances of my highest consideration”.


Issued by the Ministry of Foreign Affairs, East African, Regional and International Cooperation

February 24, 2016 

SERIKALI NA AKDN WAJADILIANA KUBORESHA MKATABA WA USHIRIKIANO


Maafisa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika kikao cha pamoja na Taasisi ya Maendeleo ya Aga Khan (The Aga Khan Development Network- AKDN). Wa tatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine ambaye alifungua rasmi kikao hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz P. Mlima. Kushoto kwa Balozi Sokoine ni  Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Baraka H. Luvanda ambaye aliongoza mazungumzo kwa upande wa Serikali ya Tanzania.  Kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere kilipitia upya Mkataba wa Ushirikiano wa Kimaendeleo kati ya Serikali na AKDN ambao ulisainiwa mwaka 2001.
Kiongozi wa Ujumbe wa Mtandao wa Maendeleo wa Agakhan Dkt. Shakif Sachedina wa kwanza kushoto ambaye aliongoza mazungumzo kwa upande wa AKDN akiwa na baadhi ya wajumbe wakifuatilia mazungumzo ya kikao.
Sehemu nyingine ya wajumbe wa AKDN wakifuatilia kikao.
Wajumbe wa Serikali ya Tanzania walioshiriki kikao hicho ambapo Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa ilikuwa mwenyeji. Ujumbe wa Serikali ulihusisha Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU); Mamlaka ya Mapato Tanzania; Ofisi ya Rais Ikulu; Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Wizara ya Sera na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu; Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Balozi Joseph Sokoine akiagana na wajumbe wa AKDN baada ya kukamilisha zoezi la ufunguzi wa kikao hicho.




Tanzania na Uturuki kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Mhe. Mevlut Cavusoglu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki alipowasili nchini humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kwa madhumuni ya kukuza ushirikiano baina ya Tanzania na Uturuki.
Mhe. Dkt. Mahiga na Mhe.Cavusoglu wakiwa katika mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Uturuki
Mazungumzo yakiendelea
===========================================

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dr. Augustine Mahiga amefanya ziara ya kikazi nchini Uturuki tarehe 23 na 24 Februari, 2016.

Wakati wa ziara hiyo Mhe. Mahiga alikutana kwa mazungumzo na Mhe. Mevlut Cavusoglu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki pembeni mwa Mkutano wa Mawaziri kuhusu Somali, uliofanyika mjini Istanbul Uturuki tarehe 23na 24 Februari, 2016. 

Katika mazungumzo, Mawaziri hao walikubaliana kukuza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na Uturuki kwa kutilia mkazo mahusiano ya kibiashara na uwekezaji. Aidha, Mhe. Waziri Mahiga aliwakaribisha Waturuki kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya kilimo hususan kuanzisha viwanda vya kuongeza thamani mazao ya kilimo. 

Vilevile, aliwakaribisha kuweka program za kubadilishana uzoefu kwenye sekta ya kilimo baina ya wataalam wa Uturuki na Tanzania. 

Kwa upande wake, Mhe. Cavusoglu alieleza kwamba Uturuki inaipa Tanzania kipaumbele kama nchi ambayo ingependa kukuza mahusiano nayo ya kibiashara na uwekezaji. Pia alimkaribisha Mhe.  Waziri Mahiga na Tanzania kushiriki katika maonyesho ya biashara ya Expo 2016 pamoja na maonyesho ya Soko la Afrika, hapo baadae mwaka huu.