Thursday, July 28, 2016

Wizara ya Mambo ya Nje yamkabidhi Waziri Mkuu michango ya Madawati

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akikabidhi hundi ya michango ya madawati kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika tarehe 28 Julai, 2016 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chamazi iliyopo Mbagala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi akipokea Hundi ya michango ya Madawati kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Geofrey Mwambe kutoka kwa  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa. Mhe. Mwambe kabla ya uteuzi wake wa kuwa Mkuu wa Wilaya alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta ya Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri Mkuu, Mhe.Kassim  Majaliwa akihutubia hadhara iliyohudhuria kushuhudia makabidhiano ya michango ya Madawati yaliyotolewa na Ubalozi wa Kuwait pamoja na Jumuiya ya Mabohora iliyopo nchini. Katika hotuba yake aliwahimiza wanafunzi wa Shule ya Msingi Chamazi kusoma kwa bidii pamoja na Walimu ambao aliwaeleza kuwa serikali ya awamu ya tano inafanyia kazi malalamiko yao na itahakikisha wanalipwa stahili zao zote.
Mhe. Waziri Mahiga akihutubia wananchi katika hafla hiyo ambapo alieleza kuwa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje (waliopo Wizarani na katika ofisi zetu za Ubalozi) wamekabidhi michango yenye thamani ya fedha taslim za Kitanzania shilingi 100, 176,825.52 katika kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli katika kuboresha sekta ya elimu nchini.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mhe. Waziri Mahiga mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Shule ya Msingi Chamazi, pembeni kwa Waziri Mahiga ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje  na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba. 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwa pamoja na viongozi waliokaa meza kuu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa.
Mhe. Waziri Mkuu akisalimia sehemu ya Wanafunzi wa shule ya Msingi Chamazi.
Mhe. Waziri Mkuu akiwasalimia sehemu nyingine ya Wanafunzi hao

Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja Mhe. Waziri Mkuu
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Waziri Mkuu pamoja na meza kuu.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi akimkaribisha Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al- Najem katika hafla ya makabidhiano ya madawati, ambapo Ubalozi wa Kuwait umechangia jumla ya madawati 600.
Msemaji na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi Mindi Kasiga (Kushoto) akiwa na Kaimu Mkuu wa Itifaki Bw. James Bwana wakiratibu hafla hiyo ya makabidhiano
Mhe. Waziri Mahiga akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Humphrey Polepole, kulia kwa Mhe. Polepole ni Mkuu wa Wilaya ya Kindononi Mhe. Ally Hapi na Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Ramadhan Madabida.
=================================================


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), ameipongeza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa kuitikia wito wa Serikali wa kuchangia madawati kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu nchini.


Mhe. Majaliwa ametoa pongezi hizo leo wakati wa hafla ya kupokea mchango wa Madawati wa Wizara zilizofanyika katika Shule ya Msingi Chamazi Jijini Dar es Salaam.



Katika hotuba yake Mhe. Waziri Mkuu alisema kuwa anaipongeza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki chini ya uongozi wa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga kwa juhudi za kuwashirikisha wadau wanaofanya kazi kwa karibu na Wizara hiyo wakiwemo Mabalozi, Watumishi na Jumuiya mbalimbali za kimataifa katika kutekeleza wito wa Serikali na hatimaye kufanisha azma hiyo

“Nampongeza Balozi Mahiga kwa mbinu alizotumia za kuwashawishi Mabalozi, Watumishi na Jumuiya mbalimbali za kimataifa na hatimaye leo napokea madawati hayo ambayo ni msaada mkubwa kwa wanafunzi wa Wilaya hii ya Temeke ambayo ina idadi kubwa ya watu na wanafunzi pia” alisema Mhe. Majaliwa.

Mhe. Waziri Mkuu aliongeza kusema kuwa, Serikali imetekeleza kikamilifu azma ya kutoa elimu bure kwa tija ambapo shule zimefanikiwa kuandikisha wanafunzi wengi wa darasa la kwanza mwaka huu kuliko ilivyokuwa hapo awali. Aidha, alieleza kuwa Serikali inaendelea kumaliza changamoto zilizotokana na ongezeko hilo ikiwa ni pamoja na kuendelea kuongeza madawati, vyumba vya madarasa na kuboresha maslahi ya Walimu.

“Azma ya Serikali ya Elimu bure imekuwa na tija kwani wazazi wameandikisha kwa wingi watoto wao ambapo nimeambiwa shule hii ya Chamazi imeandikisha zaidi ya wanafunzi 700 wa darasa la kwanza, hayo ni mafanikio makubwa na kinachotakiwa ni Serikali kutekeleza mkakati wake wa kumaliza changamoto  zilizopo ili kuendana na ongezeko hilo” alisisitiza Waziri Mkuu.

Vilevile Mhe. Majaliwa alitumia fursa hiyo kuwaasa wazazi na walezi kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu maendeleo ya watoto wao shuleni ikiwa ni pamoja na kutimiza wajibu wao wa msingi wa kuwapatia chakula, mavazi na vifaa kwa ajili ya kujifunzia.

Aidha, Mhe. Waziri Mkuu alitoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali bila kujali dini, rangi, kabila wala itikadi za kisiasa kuendelea kuchangia maendeleo ya nchi hususan katika sekta ya elimu ili kuwawezesha watoto wa kitanzania kupata elimu bora.

Awali akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga alisema kuwa ili kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli na kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa maendeleo ya nchi, Wizara ilihamasika na kuhakikisha inachangia sekta hiyo ya elimu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. 

Wakati wa hafla hiyo Wizara ilimkabidhi Waziri Mkuu jumla ya Shilingi milioni mia moja zilizochangwa na Watumishi wa Wizara, madawati 600 kutoka Ubalozi wa Kuwait hapa nchini na mengine 105 kutoka Jumuiya ya Mabohora nchini. Kati ya fedha hizo shilingi milioni 85 zilikabidhiwa kwa ajili ya kutengeneza madawati kwa ajili ya Shule za Wilaya ya Temeke huku milioni 15 zikipelekwa Wilaya ya Manyoni kwa ajili ya madawati.

-Mwisho-
 




Wednesday, July 27, 2016

Tanzania na Korea Kusini kuimarisha ushirikiano

Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbelwa Kairuki (katikati) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa masuala ya Afrika na Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Korea Kusini, Bw. KWON Hee-seog (hayupo pichani). Mazungumzo hayo rasmi ambayo yalijikita katika kujadili masuala ya ushirikiano baina ya Tanzania na Korea Kusini yalifanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2016. Wengine katika picha ni Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo.
Mkurugenzi wa masuala ya Afrika na Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kusini, Bw. Kwon Hee-seog (kulia) akizungumza ambapo alieleza nia ya Serikali ya Korea katika kuendelea kuimarisha ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hususan katika sekta ya elimu, biashara, uwekezaji na masuala ya utamaduni. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi masuala ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Korea ni Bw. JO Joosung.
Bw. Kwon Hee- seog akiwa pamoja na wajumbe aliofuatana nao wakifuatilia mazungumzo.
Mkutano ukiendelea

Tuesday, July 26, 2016

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje awa mgeni rasmi siku ya Taifa la Misri

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akitoa hotuba kama mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Taifa la Misri yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Katika hotuba yake Mhe. Dkt. Kolimba alisifu ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Misri na kuahidi kuendelea kuuimarisha kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa mataifa haya.

Sehemu ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini wakimsikiliza Mhe. Dkt. Kolimba (hayupo kwenye picha) kwenye maadhimisho ya siku ya Taifa la Misri
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Suzan Kolimba akitakiana afya njema na Balozi wa Misri nchini, Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf wakati wa maadhimisho ya Taifa la Misri yaliyofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya wageni waalikwa akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Balozi Simba Yahya (wa tatu kutoka kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo (wa pili kushoto), Msaidizi wa Naibu Waziri, Bw. Adam Isara (kushoto)  na Maafisa wa Ubalozi wa Misri (k
Sehemu ya Wageni waalikwa


   

Balozi wa Misri nchini pamoja na mkewe wakimkaribisha Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi kwenye maadhimisho ya Taifa la Misri
Meza kuu wakifurahia burudani kutoka kwa mtumbuizaji ambaye ni raia wa Misri anayeishi hapa nchini
Picha ya pamoja
Maafisa wa Ubalozi wa Misri wakiagana na Mhe. Mwinyi
Mhe. Dkt. Susan akiagana na Balozi wa Misri mara baada ya maadhimisho ya Taifa hilo
Balozi Yahya na Balozi Shelukindo wakiwa na mmoja wa wageni waalikwa
Picha ya pamoja

Friday, July 22, 2016

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje akutana na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa China nchini


Msemaji na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akizungumza na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa China nchini,  Bw. Zhang Biao alipomtembelea leo katika Ofisi za Wizara.  Katika mazungumzo yao walizungumzia namna ya kuendelea kushirikiana hususan katika   kuhakikisha Sera za Mambo ya Nje za Tanzania na China zinajulikana kitaifa na kimataifa kwa kuimarisha tasnia ya Mawasiliano kwa Umma.
Maafisa wa Ubalozi wa China nchini waliofatana na Bw. Zhang Biao wakifuatilia mazungumzo. Kutoka kushoto ni  Bi. Sun Lihua na Mkurugenzi wa Diplomasia na Habari Bw. Xu Jingchun.
Picha ya pamoja.

Thursday, July 21, 2016

Waziri Mahiga akutana na Balozi wa Iran nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Iran nchini Mhe. Mehdi Agha Jafari alipomtembelea leo katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam. Katika Mazungumzo yao Mhe. Waziri alimweleza  Balozi huyo kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano na Iran  hususan katika kuhakikisha Diplomasia ya uchumi baina ya mataifa hayo inaimarika kwa manufaa ya mataifa hayo. 
Mhe. Balozi Mehdi Agha Jafari akizungumza ambapo alieleza kuwa Serikali ya Iran itazidi kushirikiana na Tanzania katika sekta za Elimu, Biashara, Afya na Kilimo.
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima (kushoto) pamoja na Msaidizi wa Waziri, Bw. Adolf Mchemwa wakifuatilia kwa makini mazungumzo.
Mhe. Balozi Mehdi Agha Jafari akimkabidhi ujumbe maalum Mhe. Waziri Mahiga 
Mazungumzo yakiendelea

Ubalozi wa Kuwait nchini wakabidhi vitendea kazi kwa Chuo cha Diplomasia


Balozi wa Kuwait nchini, Mhe. Jasem Al-Najem akimkabidhi vitendea kazi zikiwemo Kompyuta kwa Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia (CFR), Dkt. Bernard Achiula. Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika Ofisi za Chuo hicho zilizopo eneo la Kurasini Jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi(wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Mhe. Balozi Abdallah Kilima wakiwa pamoja na Mhe. Jasem Al-Najem na Dkt. Achiula ambao waliiwakilisha Wizara katika makabidhiano hayo.
Balozi Mwinyi akiongea na Mhe. Jasem Al-Najem ambapo katika mazungumzo yao walizungumzia namna ya kuimarisha uhusiano uliodumu kwa muada mrefu baina ya mataifa ya Tanzania na Kuwait na alimshukuru kwa kukisaidia chuo hicho ambacho kipo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kumwomba kupanua wigo katika sekta ya Elimu ikiwemo kuwa na program za mafunzo na kubadilishana uzoefu baina y anchi hizi mbili.
Balozi Abdallah Kilima (kushoto) akitoa neno la shukrani kwa Mhe. Balozi Nasem Al-Najem na kueleza namna ambavyo Wizara imejidhatiti katika kuhakikisha inasimamia masuala yote ya Kidiplomasia na ushirikiano.
Mkurugenzi wa Taaluma katika Chuo cha Diplomasia, Dkt. Wetengere Kitojo akifafanua jambo wakati ujumbe huo ulipotembelea Maktaba ya Chuo. Wa pili kutoka kulia ni Bi. Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mhe. Balozi Jasem Al-Najem akiendelea kutembelea madarasa na huduma nyingine za wanafunzi katika chuo hicho.
Mhe. Balozi akisalimiana na Wanafunzi wa waliokuwa wakifundishwa somo la lugha ya Kiarabu
Balozi Mwinyi akifafanua jambo kwa Mhe. Al-Najem wakati wakitembelea maeneo ya Chuo hicho.
Dkt.Achiula akikabidhi zawadi ya kinyago kwa Mhe. Balozi Al-Najem ambapo pia alitumia fursa hiyo kumshukuru kwa msaada alioukabidhi kwa Chuo hicho.
Mhe. Balozi Al-Najem akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Chuo cha Diplomasia.

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje azungumza na Balozi wa China nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima akizungumza na Balozi wa China nchini, Mhe. Dkt. Lu Youqing alipofika Wizarani kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na China. Katika mazungumzo yao walijadili namna ya kuendelea kuimarisha ushirikiano hususan katika masuala ya kukuza uchumi  kupitia viwanda na uwekezaji na kuendelea kukamilisha miradi mbalimbali ya pamoja ikiwemo ule wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Sehemu ya Ujumbe kutoka Ubalozi wa China.
Balozi nae akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na Katibu Mkuu, Dkt. Mlima
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Christopher Mramba (kushoto) pamoja na Bw. Humphrey Shangarai, Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo kati ya Dkt. Mlima na Balozi Lu (hawapo pichani)

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje azungumza na Balozi wa China nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima akizungumza na Balozi wa China nchini, Mhe. Dkt. Lu Youqing alipofika Wizarani kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na China. Katika mazungumzo yao walijadili namna ya kuendelea kuimarisha ushirikiano hususan katika masuala ya kukuza uchumi  kupitia viwanda na uwekezaji na kuendelea kukamilisha miradi mbalimbali ya pamoja ikiwemo ule wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Sehemu ya Ujumbe kutoka Ubalozi wa China.
Balozi nae akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na Katibu Mkuu, Dkt. Mlima
Mkurugenzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Christopher Mramba (kushoto) pamoja na Bw. Humphrey Shangarai, Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo kati ya Dkt. Mlima na Balozi Lu (hawapo pichani)

KATIBU MKUU AKUTANA NA MKURUGENZI MKAZI WA SHIRIKA LA TRADEMARK EAST AFRIKA

Mkurugenzi wa Shirika la TradeMark East Afrika (TMEA) Bw. John Ulanga (kushoto) akizungumza na Katibu Mkuu Balozi Dkt. Aziz P. Mlima (kulia) alipotembelea Wizarani leo. Bw. John Ulanga amechukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika hilo Dkt. Josaphat Kweka baada ya kumaliza mkataba wake wa kulitumikia shirika. Katika mazungumzo hayo Mkurugenzi mpya wa shikirika la TradeMark East Afrika Bw. John Ulanga  aliahidi kudumisha na kukuza ushirikiano na serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Nchini.
Katibu Mkuu Balozi Dkt. Aziz P. Mlima (wa pili kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi mpya wa Shirika la TradeMark East Afrika Bw. John Ulanga (kushoto). Wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Osward Kyamani (kulia) na Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji Bw. Bernard Haule (wapili kulia)
Katibu Mkuu Balozi Dkt. Aziz P. Mlima na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la TradeMark East Afrika wakiendelea na mazungumzo. Tokea kushoto ni Afisa Uchumi kutoka Wizarani na Mratibu wa maratibu wa mradi wa TMEA  Bi. Joyce (wakwanza kushoto) Kimei na Afisa kutoka TMEA Bi. Monika Hangi (wapili kushoto)
Mkurugenzi wa TMEA Bw. John Ulanga akielezea jambo kwa Katibu Mkuu Balozi Dkt. Aziz P. Mlima