JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA
USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Simu: 255-22 211906-12,
2126827
Fax: +255-22 2116600,
2120488/2126651
|
|
20 KIVUKONI FRONT,
P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM,
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkutano
wa tano wa Bunge la tatu la Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EALA) kuanza Arusha
Bunge la Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EALA) linatarajia kuanza vikao vyake mapema wiki ijayo Jijini
Arusha, Tanzania, kwa muda wa wiki mbili kuanzia Jumatatu Agosti 22, 2016 hadi
Ijumaa Agosti 2, 2016.
Pamoja na mambo mengine
Bunge hilo linatarajia kujadili ripoti ya ukaguzi wa hesabu kutoka Kamati ya
Fedha kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2015. Ripoti hiyo inayozingatia na kuonyesha
taarifa za ukaguzi wa hesabu za fedha kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2015,
inahusisha taasisi na vyombo mbalimbali vilivyopo chini ya Sekretariati ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Miradi 20 inayotelezwa na kusimamiwa na
Sekretariati, kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 134 ya Mkataba wa
uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Tume ya ukaguzi iliwasilisha ripoti yake
kwenye Baraza la Mawaziri na kujadiliwa na Baraza hilo Mei 24, 2016. Ripoti hii
ya tume ya ukaguzi inayoonesha
kuwa bajeti imetekelezwa kwa 65% inajadiliwa kipindi ambacho Jumuiya inapitia
kipindi kigumu cha ukosefu wa
fedha.
Pia
Bunge linatarajia kujadili ripoti ya Kamati ya Kilimo, Utalii na Maliasili
kuhusu uangalizi wa shughuli za Utalii katika Jumuiya. Vilevile Bunge
litajadili ripoti nyingine ya kamati ya Kilimo, Utalii na Biashara ambapo
itaangazia hali ya ujangili ndani ya JumuiyaKama sehemu ya kudumisha
ushirikiano na wadau wengine kwenye kanda, EALA itapokea ripoti kuhusu masuala
ya vijana ndani ya Jumuiya kufuatia matokeo ya utafiti uliofanywa na Shirika la
Afrika Mashariki (The East African Institute) chini ya uangalizi wa Shirika la
Mtandao wa Maendeleo la Aga Khan (Aga Khan Development Network)
Vikao
vya EALA vinafanyika kwa utaratibu wa mzunguko miongoni mwa Nchi Wanachama kwa
mujibu wa kifungu cha sheria namba 55 ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki. Wakati huohuo Bunge linafanya kazi kwa ukaribu na wadau
mbalimbali sambamba na kupokea taarifa kuhusu Bunge hilo. Bunge hilo
linatarajiwa kuongozwa na Spika wake Mhe. Daniel Kadega.
Mwisho
Imetolewa na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar
es Salaam,
26 Mei 2016.