Friday, August 19, 2016

Mkutano wa tano wa Bunge la tatu la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) kuanza Arusha

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
 


Simu: 255-22 211906-12, 2126827  

Fax: +255-22 2116600, 2120488/2126651
Barua pepe: gcu@nje.go.tz

Tovuti: www.foreign.go.tz/ www.meac.go.tz


                20 KIVUKONI FRONT,
                           P.O. BOX 9000,
            11466 DAR ES SALAAM, 
                                    Tanzania.

 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkutano wa tano wa Bunge la tatu la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) kuanza  Arusha
Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) linatarajia kuanza vikao vyake mapema wiki ijayo Jijini Arusha, Tanzania, kwa muda wa wiki mbili kuanzia Jumatatu Agosti 22, 2016 hadi Ijumaa Agosti 2, 2016.

Pamoja na mambo mengine Bunge hilo linatarajia kujadili ripoti ya ukaguzi wa hesabu kutoka Kamati ya Fedha kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2015. Ripoti hiyo inayozingatia na kuonyesha taarifa za ukaguzi wa hesabu za fedha kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2015, inahusisha taasisi na vyombo mbalimbali vilivyopo chini ya Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Miradi 20 inayotelezwa na kusimamiwa na Sekretariati, kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 134 ya Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Tume ya ukaguzi iliwasilisha ripoti yake kwenye Baraza la Mawaziri na kujadiliwa na Baraza hilo Mei 24, 2016. Ripoti hii ya tume ya ukaguzi inayoonesha kuwa bajeti imetekelezwa kwa 65% inajadiliwa kipindi ambacho Jumuiya inapitia kipindi kigumu cha ukosefu wa fedha.
Pia Bunge linatarajia kujadili ripoti ya Kamati ya Kilimo, Utalii na Maliasili kuhusu uangalizi wa shughuli za Utalii katika Jumuiya. Vilevile Bunge litajadili ripoti nyingine ya kamati ya Kilimo, Utalii na Biashara ambapo itaangazia hali ya ujangili ndani ya JumuiyaKama sehemu ya kudumisha ushirikiano na wadau wengine kwenye kanda, EALA itapokea ripoti kuhusu masuala ya vijana ndani ya Jumuiya kufuatia matokeo ya utafiti uliofanywa na Shirika la Afrika Mashariki (The East African Institute) chini ya uangalizi wa Shirika la Mtandao wa Maendeleo la Aga Khan (Aga Khan Development Network)
Vikao vya EALA vinafanyika kwa utaratibu wa mzunguko miongoni mwa Nchi Wanachama kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 55 ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wakati huohuo Bunge linafanya kazi kwa ukaribu na wadau mbalimbali sambamba na kupokea taarifa kuhusu Bunge hilo. Bunge hilo linatarajiwa kuongozwa na Spika wake Mhe. Daniel Kadega.

Mwisho
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 26 Mei 2016.




No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.