Mhe. Naibu Waziri akipata maelezo kuhusu bidhaa mbalimbali zinazozalishwa Tanzania zilizokuwepo kwenye Banda hilo. Bidhaa hizo ni pamoja na Kahawa, Majani ya Chai na Viungo vya chakula |
Banda la Tanzania kama linavyoonekana |
Mhe. Waziri akipata maelezo ya namna watu wa makampuni mbalimbali walivyovutiwa na kahawa ya Tanzania |
Mhe. Naibu Waziri akikaribishwa na Bi. Latifa Kigoda, Afisa Mwandamizi kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) alipotembelea banda la Tanzania |
Mhe. Naibu Waziri akisaini kitabu cha wageni bandani hapo |
Mhe. Naibu Waziri akisikiliza maelezo kutoka kwa Bi. Kigoda kuhusu namna TIC ilivyojipanga kutangaza fursa za uwekezaji kwa wawekezaji mbalimbali wanaohudhuria mkutano wa TICAD VI |
Bi. Kigoda akimpatia Jarida Maalum lililoandaliwa na TIC kwa ajili ya kuvutia wawekezaji waliohudhuria mkutano wa TICAD VI |
Bi. Kigoda akimpatia maelezo Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Bi. Talha Waziri ambaye alikuwa amefuatana na Mhe. Naibu Waziri. |
Mmoja wa wageni aliyetembelea bandani hapo akipata maelezo ya fursa za uwekezaji zilizopo nchini kutoka kwa Bi. Kigoda |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Susan Kolimba akipata maelezo kutoka kwa Bw. Lameck Borega, Meneja wa Uwekezaji wa EPZA. |
Mhe. Dkt. Kolimba akimpatia ushauri wa namna ya kuwashawishi wawekezaji kuja nchini kuwekeza kupitia EPZA |
Mhe. Naibu Waziri akiwa amewasili kwenye Banda la Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na kupatiwa maelezo na Bi. Alistidia Karaze, Afisa Utafiti Mkuu kwenye Bodi hiyo |
Mhe. Naibu Waziri akimpatia ushauri Bi. Karaze wa namna ya kuboresha huduma za utalii nchini ikiwemo maonesho ili kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea nchini. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.