Monday, August 1, 2016

Waziri Mahiga akutana na wageni mbalimbali waliotembelea Wizarani


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akizungumza na Kaimu Balozi wa Oman nchini, Bw. Mohammed Sulaiman Alrawahi. Mazungumzo yao ambayo yalijikita zaidi katika masuala ya ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili yalifanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam, tarehe 1 Agosti, 2016. 
Mazungumzo yakiendelea
=========================================

...Wakati huo huo Mhe. Waziri Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mteule wa Italia nchini.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Augustine Mahiga (Kushoto) akizungumza na Balozi wa Italia nchini, Mhe.Roberto Mengon ambaye alimtembelea Wizarani Jijini Dar es Salaam tarehe 1 Agosti, 2016. Katika Mazungumzo yao Mhe. Waziri alimshukuru Mhe. Roberto kwa mchango mkubwa ambao umekuwa ukitolea na Serikali ya Italia katika kusaidia Sekta ya Elimu, miundombinu na afya kwamba Tanzania itazidi kuimarisha ushirikiano na nchi hiyo.
Mhe. Robert katika mazungumzo yake alieleza kuwa amefurahishwa sana na hali ya amani iliyopo nchini Tanzania kwa kuwa wananchi wa makabila na imani tofauti wameweza kuchanganyika na kuishi pamoja na kutumia lugha moja ya Kiswahili na kwamba ni mfano unaotakiwa kuigwa na mataifa mengine.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Ushirikiano wa Maendeleo, Kanda ya Afrika Mashariki ya Italia iliyopo Nairobi, Kenya Bi. Teresa Savanella ambaye alifuatana na Mhe. Roberto akieleza namna ambavyo Taasisi hiyo ambayo inayojishughulisha na kutoa Elimu ya Ufundi inavyotekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kusaidia vijana wa Afrika Mashariki kupata elimu ya ufundi kwa ajili ya kujiajiri. Kulia ni Afisa wa Ubalozi wa Italia nchini.

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine(kushoto) pamoja na Afisa Mambo ya Nje Bw. Antony Mtafya wakifuatilia mazungumzo.
Picha ya pamoja

===========================================

...Mkutano kati ya Mhe. Waziri Mahiga  na Naibu Meya wa Bermuda 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Naibu Meya wa Mji wa Hamilton nchini Bermuda, Mhe. Donal Smith kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa. Katika mazungumzo yao, Mhe. Waziri alieleza nia ya Serikali  ya Tanzania katika kushirikiana na wawekezaji mbalimbali wanaotaka kuja  nchini hususan katika miradi ambayo ina tija kwa Taifa na ambayo itatoa ajira kwa Watanzania ili kuweza kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya  Tanzania kuwa nchi ya Viwanda. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 1 Agosti, 2016
Mhe. Donal nae akimweleza Mhe. Waziri Mahiga kuhusu lengo la ziara yake nchini kuwa ni kuitambulisha Kampuni ya Nelson & Pade inayojishughulisha na kilimo cha kisasa cha mbogamboga na ufugaji wa samaki inayotaka kuja kuwekeza nchini. Pia alimweleza nia ya nchi yake ya kuja kuwekeza kwenye uchimbaji wa mawe aina ya lime (limestone) na matumizi yake katika ujenzi wa kisasa pamoja na kuleta wawekezaji  katika viwanda vya kutengeneza madawa ya binadamu.
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine (kushoto) pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Mona Mahecha wakifuatilia mazungumzo.
Mhe. Waziri Mahiga akiangalia moja ya miradi ya kilimo inayofanywa na Kampuni ya Nelson & Pade
Mazungumzo yakiendelea

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.