Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akimpokea rasmi Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mhe. Jean-Marc Ayrault (kushoto) alipotembelea Wizarani katika ziara yake ya kikazi nchini. Mazungumzo kati yao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ufaransa ili kuchangia maendeleo ya nchi hizi mbili. Pia Waziri Mahiga alitumia fursa hiyo kumpa salamu za pole kutokana na mashambulio ya kigaidi yaliyotokea nchini Ufaransa hivi karibuni. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2016.
|
Waziri Mahiga akizungumza huku Mhe. Waziri Ayrault akimsikiliza. |
|
Wajumbe waliofuatana na Mhe. Waziri Aryault nao wakifuatilia mazungumzo. Kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Malika Berak |
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.