Wednesday, August 24, 2016

Rais Magufuli apokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Waheshimiwa Mabalozi wa Ireland, Somalia, Italia na Korea Kusini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mhe. Paul Sherlock Ikulu Jijini Dar es Saalam
Balozi wa Ireland nchini Tamzamia, Mhe. Paul Sherlock akisaini Kitabu cha Wageni Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Paul Sherlock (wa tatu kushoto). Wengine katika picha, kulia kwa Mhe. Balozi ni Maafisa alioambatana nao na kutoka kulia Balozi Zuhura Bundara, Mshauri wa Rais wa masuala ya Diplomasia na Balozi Joseph Sokoine, Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Balozi Mteule wa Somalia nchini Tanzania, Mhe. Mohammed Hassan Abdi akisaini Kitabu cha Wageni Ikulu Jijini Dar es Saalam kabla ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli

Balozi wa Somalia nchini Tanzania, Mhe. Mohammed Hassan Abdi akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Balozi Mteule wa Somalia nchini Tanzania, Mhe. Mohammed Hassan Abdi (katikati) akitoa heshima wakati Wimbo wa Taifa ulivyokuwa ukipigwa mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Saalam kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Kushoto kwa Mhe. Balozi ni Kaimu Mkuu wa Itifaki, Bw. James Bwana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Somalia nchini Tanzania, Mhe. Mohammed Hassan Abdi mara baada ya kuwasilisha Hati za utambulisho

Balozi Mteule wa Italia nchini Tanzaia, Mhe.Roberto Mengoni akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ikulu, Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Roberto Mengoni akiwasilisha Hati zUtambulisho kwa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akisalimia na Balozi Mteule wa Italia, Mhe. Roberto Mengoni Ikulu Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Italia nchini, Mhe. Roberto Mengoni (katikati) akitoa heshima kwa wimbo wa Taifa alipowasili Ikulu kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe  Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi kutoka Ofisi ya Ubalozi wa Italia na Wizarani. Wapili kulia ni Balozi Joseph  Sokoine, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na wa kulia ni Balozi Zuhura Bundala, Mshauri wa Masuala ya Diplomasia wa Rais.




Balozi Mteule wa Jamhuri ya Watu wa Korea nchini Tanzania, Mhe. Kim Yong Su akisaini Kitabu cha Wageni Ikulu Jijini Dar es Salaam kabla ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Korea nchini Tanzania, Mhe. Kim Yong Su akiwasilisha  Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na  Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Korea Mhe. Kim Yong Su mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho




No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.