Saturday, February 4, 2017

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


JPCC kati ya Tanzania na Malawi ni chachu ya kuimarisha mahusiano

Wajumbe wanaoshiriki katika Kikao cha 4 cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya  Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi kilichofunguliwa leo jijini Lilongwe, Malawi wamehimizwa katika majadiliano yao ya  siku tatu  kubuni mkakati utakaowezesha kutatua changamoto zinazojitokeza kutokana na muingiliano mkubwa wa ngazi mbalimbali za ushirikiano baina ya wananchi  wa  mataifa hayo mawili.

 Kauli hiyo imetolewa na Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya Wataalam, Balozi Ramadhan Mwinyi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipokuwa anasoma hotuba ya ufunguzi.

"Kama mnavyofahamu kunapokuwa na maingiliano makubwa ya wananchi wa nchi mbili kama zilivyo nchi zetu, changamoto haziwezi kukosa kujitokeza. Hivyo ni jukumu letu sisi wataalamu kubuni mkakati wa kuhakikisha kuwa changamoto hizo zinashughulikiwa haraka iwezekanavyo".

Balozi Mwinyi alieleza kuwa kikao hicho ni fursa nzuri kwa Serikali za Tanzania na Malawi kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi zao katika maeneo tofauti ikiwemo uchumi, uwekezaji, biashara, kutunza mazingira, elimu, Tehama, kilimo, uhamiaji, uchukuzi na masuala ya ulinzi na usalama, Hivyo alihimiza wajumbe wa pande zote mbili kuwa wabunifu katika majadiliano yao ili watoke na mipango inayotekelezeka kwa kuwa wananchi wanachohitaji ni maendeleo na sio mikakati inayoishia katika makabrasha.

Aidha, Balozi Mwinyi aliekeza kuwa watu wengi walistaajabu kusikia ujumbe wa Tanzania unakuja Malawi kushiriki kikao hiki kama walivyostaajabu kuona Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya mazungumzo hivi karibuni na Rais wa Malawi, Mhe. Prof. Peter Mutharika pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia. Alisema hakuna cha kustaajabisha hapo, isipokuwa ifahamike lengo kuu la pande zote mbili ni kuona uhusiano kati ya Tanzania na Malawi unaimarishwa na kwamba mkutano huo ni ushahidi kuwa nchi hizi mbili zipo karibu zaidi kuliko hapo awali.

Naibu Katibu Mkuu aliihakikishia Serikali ya Malawi kuwa Serikali ya Tanzania imedhamiria kushirikiana na nchi hiyo katika kuboresha mahusiano ya kidiplomasia, uchumi na kijamii, hivyo alisisitiza umuhimu wa yale yote yatakayoafikiwa katika mkutano huo yanatekelezwa katika muda uliopangwa.

Alishauri iundwe timu ya ngazi ya Makatibu Wakuu ambayo itakuwa inakutana kila baada ya miezi sita kutathmini utekelezaji wa maazimio ya kikao hicho.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi, Dkt. Dalitso Kabambe alisisitiza umuhimu wa nchi hizi mbili kuweka mikakati itakayorahisisha wananchi kufanya biashara bila vikwazo. "Bisahara ni jambo muhimu lazima tuhakikishe kuwa Serikali zetu zinaweka mazingira mazuri ili wananchi wafanye biashara kwa wepesi".

Kikao hicho kinatarajiwa kufungwa rasmi na Mawaziri wa Mambo ya Nje siku ya Jumapili tarehe 05 Februari 2017 ambapo Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anatarajiwa kuwasili Malawi tarehe 04 Februari 2017. Mawaziri hao pia wataweka saini Mikataba mitatu ya ushirikiano katika mashauriano ya kisiasa na kidiplomasia, usafiri wa anga na utalii.

Wajumbe wa Tanzania katika kikao hicho wanatoka katika sekta mbalimbali wakiwemo wajumbe kutoka mikoa miwili ya Mbeya na  Ruvuma inayopakana na Malawi ambao wanaongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla.



Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Tarehe  03 Februari 2017


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi na Mwenyekiti Mwenza wa Kikao cha JPCC kati ya Tanzania na Malawi, Dkt. Kalitso Kabambe akisoma hotuba ya iufunguzi na ukaribisho.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi akisoma houtuba ya ufunguzi wa kikao cha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi, Dkt. Dalitso Kabambe. Kikao hicho kinafanyika Lilongwe, Malawi kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 03 Februari 2017.


Wajumbe wa Tanzania wakisikiliza hotuba za Makatibu Wakuu. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla, Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Suleiman Salehe na Kaimu Mkurugenzi kutoka Mamlka ya Viwanja vya Ndege.


Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Ali Ubwa na mjumbe mwingine ambaye jina lake halikupatikana.


Bw. Kalitso Kabambe akiwa na Balozi wa Malawi nchini Tanzania.


Sehemu  ya ujumbe wa Malawi ukifuatilia hotuba za ufunguzi

Wajumbe wa pande zote mbili wakiwa katika kikao cha JPCC

Naibu Katibu Mkuu, Balozi Mwinyi akihojiwa na Mwandishi wa TBC, Bw. Hosea Cheo

Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Victoria Mwakasege akihojiwa na Mwandishi wa TBC

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla akifanya mahojiano na Mwandishi wa TBC

Friday, February 3, 2017

Waziri Mahiga afanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi wa  Kuwait nchini Mhe.Jasem Ibrahim Al Najem walipokutana kwa mazungumzo Wizarani Jijini Dar es Salaam. Mazungumzo hayo yalijikita katika kujadili namna ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo nchini itakayo fadhiliwa na serikali ya Kuwait ikiwemo uchimbaji visima vya maji, miradi ya kuendeleza elimu na kuboresha sekta ya afya.

Waziri Mhe. Mahiga akimsikiliza Balozi wa Kuwait nchini Mhe.Najem

Waziri Mahiga na Balozi wa Kuwait nchini wakifurahia jambo

Waziri Mahiga apokea nakala za hati za utambulisho wa Balozi Mteule wa Oman

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Oman nchini Mhe.Ali A. Al Mahruqi alipowasili Wizarani kuwasilisha nakala za hati za utambulisho

Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga na Balozi Mteule wa Oman nchini Tanzania Mhe. Mahruqi wakionesha nakala ya hati ya utambulisho

Waziri Mhe.Balozi Dkt. Mahiga akimsikiliza Balozi Mteule wa Oman nchini

Mazungumzo yakiendelea, Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Abasi Kilima akifuatila mazungumzo

Picha ya pamoja

Waziri Mahiga apokea nakala za hati za utambulisho wa Balozi Mteule wa Iran


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Iran Nchini Tanzania Mhe.Mousa Ahmed Farhang aliwasili Wizarani kuwasilisha nakala za hati za utambulisho

Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akizungumza mara baada ya kupokea nakala za hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Iran nchini Tanzania Mhe.Farhang. Kushoto ni Maafisa kutoka Ofisi za Ubalozi wa Iran nchini na Maafisa Kutoka Wizarani (kulia) wakifuatilia mazungumzo. Katika mazungumzo hayo Waziri alimkaribisha Balozi na kumhaidi kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika utekelezazi wa majukumu yake na kwa nchi ya Iran kwa ujumla, ili kuendeleza na kudumisha uhusiano wa Kidiplomasia uliodumu kwa muda mrefu kati ya Tanzania na Iran.


Waziri Mhe. Balozi Dk. Mahiga akizungumza na mgeni wake Mhe.Balozi Farhang

Balozi Mteule wa Iran Mhe. Farhang akizunguza mara baada ya kuwasilisha nakala za hati za utambulisho

Waziri Mhe.Balozi Dkt. Mahiga akipokea nakala za hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Iran nchini Tanzania Mhe. Farhang


Thursday, February 2, 2017

Naibu katibu Mkuu akutana na ujumbe kutoka Sweden


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Naje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi akisalimiana na mmoja wa wajumbe kutoka Sweden walipokutana kwa mazungumzo Wizarani Jijini Dar es Salaam. Mazungumzo yao yalijikita katika kuendeleza ushirikiano wa Kiplomasia, shughuli za Kijamii na Kiuchumi baina ya nchi hizi mbili

Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhan Mwinyi akizungumza alipokutana na ujumbe kutoka Sweden, Kushoto ni Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Katarina Rangnitt
Mazungumzo yakiendelea

Mkurugenzi Mkuu wa Maendeleo ya Kimataifa kutoka Sweden Bw.Johannes Oljelund akizungumza alipokutana na Naibu Katibu Mkuu, Wa tatu kushoto Mkurugenzi Mkuu wa Biashara Bi.Karin Olofsdotter

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Balozi Joseph Sokoine (wapili kulia) akifuatilia mazungumzo, Wa kwanza kulia ni Afisa kutoka Wizarani Bi. Tunsume Mwangolombe

Watumishi wapewa semina ya maandalizi ya kuhamia Makao Makuu ya Serikali Dodoma

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara Bi. Mindi Kasiga akifungua warsha ya kuwaandaa watumishi wa Wizara kuhamia Makao Makuu ya Serikali Dodoma hivi karibuni.

Mkurugenzi wa  Utawala na Usimamizi Rasmilimali watu Bw.Nigel Msangi akizungumza na watumishi (hawapo pichani) katika warsha hiyo.

Mwezeshaji wa warsha hiyo Bibi.Margaret Mussai kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto akizungumza na watumishi 

Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi, Bw. Darius Damas Kalijongo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto akitoa mada katika warsha hiyo

Mtumishi akichangia jambo wakati wa warsha