Thursday, March 9, 2017

Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa aipongeza Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Antonio Guterres (kushoto) kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam jana. Mhe. Guterres alisimama kwa muda katika uwanja huo akitokea nchini Kenya kwa ajili ya kufanya mazunguzmo na Balozi Mahiga. Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine, Mhe Guterres aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudi zake za kutafuta amani nchini Burundi kupitia kwa Msuluhishi wa Mgogoro huo Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Benjamin Willium Mkapa. 
Aidha, Dkt. Mahiga aliwasilisha Salamu Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri Mahiga akizungumza jambo huku Mhe. Guterres akimsikiliza kwa makini.
 Dkt. Mahiga akiendelea kuzungumza na Mhe. Guterres huku Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (wa pili kutoka kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy wakiwasikiliza kwa makini.
 Picha ya pamoja   

  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Bi. Mindi Kasiga naye akiagana na Mhe. Guterres  

Mhe. Guterres akiagana na Dkt. Mahiga mara baada ya kumaliza kufanya mazungumzo yao.



   PRESS RELEASE



UN SECRETARY GENERAL STOPS IN DAR ON HIS WAY TO NEW YORK

H.E. Dr. John Pombe Magufuli, the President of the United Republic of Tanzania has urged the United Nations to continue its support in bringing about political stability in Burundi and the Democratic Republic of Congo.

In his special message to the United Nations Secretary General Mr. Antonio Guterres President Magufuli explained that the recent instability in the two countries has created refugees’ influx in Tanzania and its neighbors, hence the region is committed to ensure political stability is restored.

Delivering President Magufuli’s message to the United Nations Secretary General Mr. Antonio Guterres, Tanzania’s Foreign Minister Augustine Mahiga said that as the chair of EAC, Tanzania is hopeful with the progress been made in the mediation process in Burundi under the leadership of President Yoweri Museveni of Uganda and facilitated by the former President of Tanzania, H.E. Benjamin William Mkapa. Hon. Mahiga also informed the UN Secretary General that the upcoming EAC Summit is expected to receive a progressive report about the process.

With regards to the Democratic Republic of Congo, Minister Mahiga revealed that the Southern African Development Community is intending to include the agenda of political transition in DRC, whereby SADC member states are expecting positive deliberations. Tanzania is the current chair of the SADC organ of political, defense and security with the mandate to support the achievement and maintenance of peace and security as well as the rule of law in the SADC region.

Upon receiving President Magufuli’s message, Mr. Guterres praised Tanzania for its ability to uphold principles of good governance in the country as well as maintaining peace and creating a peaceful environment in the EAC and SADC regions.

Mr. Guterres commended President Magufuli’s efforts in Burundi peace process, and his readiness to host refugees from Burundi, emphasizing the role played by regional communities in Africa in resolving leadership crisis in African countries.

“The United Nations appreciates the work done by President Mkapa in Burundi under the EAC and its leadership. If the region come together the way EAC has done in the case of Burundi, I am sure together they will be able to establish lasting solutions” he remarked.

Minister Mahiga told the reporters that President Magufuli met Mr. Guterres during the AU Summit in Addis Ababa earlier this year, where the two leaders exchanged cordial discussions about various issues concerning the region.

“President Magufuli instructed me to deliver his message to Mr. Guterres, and has also extended an invitation to the Secretary General at an appropriate time to have a working visit in the country” concluded Hon. Mahiga.

Mr. Guterres was met and held talks with Foreign Minister Mahiga at the Julius Nyerere International Airport yesterday night where he was on transit from Somalia and Kenya for a working visit. Also present at the airport was the United Nations Resident Coordinator, Mr. Alvaro Rodriguez and officials from the Ministry of Foreign Affairs including the Director of Multilateral Cooperation Ambassador Celestine Mushy and Ministry’s Spokesperson Ms. Mindi Kasiga. 

Issued by:
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Dar es salaam, Tanzania
March 9, 2017.

Wednesday, March 8, 2017

Waziri Mahiga akutana na Mabalozi wa Tanzania nchini Oman, Korea, Kampala,Uganda, Kenya, Algeria, Qatar na Sudan

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) akizungumza  na Mabalozi wanao kwenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali (hawapo pichani), mazungumzo hayo yalifanyika leo katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam. 
Mhe. Mahiga alitumia fursa hiyo kuwasisitiza umuhimu wa kutekeleza majukumu yao kikamilifu, sambamba na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.
Waheshimiwa Mabalozi wakimsikiliza Waziri Mahiga,  kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Abdallah Kilima, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Grace Mgovano na Balozi wa Tanzania nchini Korea, Mhe.  Matilda Masuka.
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Mabalozi  wakimsikiliza Waziri Mahiga. Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Sudan, Mhe. Silima  Haji, Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma Rajab, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Pindi Chana na Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Omar Mzee.
Mazungumzo yakiendelea.
Picha ya pamoja Mhe. Waziri na Waheshimiwa Mabalozi

Monday, March 6, 2017

Waziri Mahiga azungumza rasmi na Mabalozi kuhusu kuhamia Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiongea na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa yanayowakilisha hapa nchini (hawapo pichani) kwenye kikao kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Aziz P.Mlima. Katika kikao hicho Mhe. Mahiga aliwaeleza rasmi kuhusu mpango wa Serikali kuhamia Dodoma na kuwaomba nao kuwa tayari kuutekeleza.

Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia kikao
Sehemu nyingine ya Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wakifuatilia kikao.
Kikao kikiendelea
Mkuu wa Mabalozi  ambaye pia ni Balozi wa Angola nchini, Mhe. Ambrosio Lukoki (kushoto) akizungumza katika kikao hicho. Pamoja na mambo mengine alieleza kuwa Jumuiya ya wanadiplomasia imelipokea agizo la Makao Makuu ya Nchi kuhamia Dodoma na kwamba wapo tayari kushiriki katika hatua zote za maandalizi ya kuhamia Dodoma ili kufanikisha zoezi la kuhama na kuisaidia Serikali katika huduma za ushauri na uzoefu wa namna nzuri ya kuhamisha miji mikuu.
Kulia ni Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Grace Martin na Balozi Mlima wakifuatilia kikao.
Sehemu ya Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kikao.
Balozi wa Malawi nchini Mhe. Hawa Ndilowe akichangia hoja katika kikao hicho.
Balozi wa Japan nchini, Mhe. Masaharu Yoshida naye akichangia hoja katika kikao.
Kikao kikiendelea.





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Balozi Mahiga aongea na Mabalozi kuhusu kuhamia Dodoma

Mabalozi na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wa hapa nchini wametakiwa kuyahimiza makampuni ya nchi yao kutumia fursa za uwekezaji zinazotokana na zoezi la Serikali la kuhamia Dodoma. 
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb) katika kikao maalum cha kuwafahamisha wanadiplomasia hao uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Tano wa kuhamia Dodoma.
“Uamuzi wa kuhamishia Makao Makuu ya Serikali mjini Dodoma umetengeneza fursa nyingi za uwekezaji katika maeneo mbalimbali kama vile utengenezaji wa vifaa vya ujenzi; ujenzi wa majengo ya ofisi, biashara na makazi; huduma za kijamii kama hospitali, shule, miundombinu ya maji safi na maji taka; TEHAMA; bustani za mapunziko; shughuli za kilimo na utalii. Hivyo, nachukua fursa hii kuwaomba muwahimize wawekezaji kutoka nchi zenu kuchangamkia fursa hizo”, Balozi Mahiga aliwambia wanadiplomasia wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.
Balozi Mahiga alieleza kuwa uamuzi wa kuhamisha Makao Makuu ya Serikali kutoka Dar Es Salaam kwenda Dodoma ulifanywa mwaka 1973 lakini tokea kipindi hicho haukuweza kutekelezwa kutokana na sababu mbalimbali hadi Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ilipoingia madarakani.
Mhe. Waziri alieleza kuwa zoezi la Serikali kuhamia Dodoma limepangwa kutekelezwa kwa awamu nne ambapo awamu ya kwanza tayari imeshakamilika. Katika awamu hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imehamisha watumishi 47 kati ya 152 waliopo Makao Makuu akiwemo yeye mwenyewe, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu. 
Waziri Mahiga aliendelea kueleza kuwa kufuatia kuanza utekelezwaji wa uamuzi huo ambao ulitangazwa rasmi na Mhe. Magufuli alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM tarehe 23 Julai 2016, hakuna budi kwa Ofisi za Balozi na Mashirika ya Kimataifa nazo zianze kujiandaa kwa ajili ya kuhamia mji huo Mkuu wa Serikali.  
Aliongeza kuwa, katika kipindi hiki cha mpito, baadhi ya Watumishi wa Wizara watakuwepo Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine watasaidia mawasiliano na ofisi hizo. Aidha, katika kipindi hicho, Wizara katika ofisi zake mpya zilizopo kwenye Jengo la LAPF mjini Dodoma itaimarisha mawasiliano kwa njia ya simu, mtandao wa internet na kufunga kifaa cha kufanyia mikutano kwa njia ya video ili kurahisisha mawasiliano na ofisi za Balozi.
Mhe. Mahiga aliwafahamisha Mabalozi hao kuwa Serikali itatenga eneo maalum ambalo litakuwepo kwenye mji wa Serikali utakaojengwa Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za balozi na mashirika ya kimataifa.  Alisema pindi Serikali itakapokamilisha zoezi la kupitia upya Mpango Mkuu wa Mji wa Dodoma, itawasiliana na Balozi hizo ili ziweze kuwasilisha maombi ya mahitaji ya ardhi wanayohitaji.
Balozi Mahiga alihitimisha kikao hicho kwa kuwashauri wanadiplomasia wanaomiliki majengo jijini Dar es Salaam kuingia makubaliano maalum na kampuni zinazohitaji ofisi hapa jijini ili kampuni hizo ziwajengee majengo ya ofisi mjini Dodoma. 
Kwa ujumla wanadiplomasia walipokea uamuzi huo na kuiomba Wizara iwasilishe taarifa hiyo kwa maandishi ili nao waiwasilishe kwenye Serikali zao kwa ajili ya utekelezaji.
                                                                                                                                                                         
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 06 Machi 2017.


                                                                                                                                                                         

Friday, March 3, 2017

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana kwa mazungumzo na Balozi wa Palestina nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt.Susan Kolimba amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Palestina hapa nchini Mhe.Hazem Shabat. Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha mahusiano baina ya Tanzania na Palestina katika sekta mbalimbali.
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo kati ya Dkt. Kolimba na Balozi wa Palestina (hawapo pichani).Kutoka kushoto ni Bw. Hangi Mgaka, Bw. Charles Faini na  Bi. KisaDoris Mwaseba.
Mazungumzo yakiendelea.

Thursday, March 2, 2017

Waziri Mahiga akutana na Rais wa Mahakama ya Afrika ya haki za Binadamu na Watu

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifafanua jambo alipokutana na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Jaji Sylvain Ore yenye Makao Makuu Jijini Arusha,Tanzania. Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Mhe. Wiziri Mahiga mjini Dodoma, wamejadili masuala mbalimbali ya kuboresha miundombinu ya mahakama hiyo ikiwemo majengo ya ofisi ili kuiongezea ufanisi zaidi.


Mazungumzo yakiendelea; Kushoto ni Wafanyakazi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu na kulia kwa Rais wa Mahakama, ni Mtumishi wa Wizara Bw. Beatus Kalumuna

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Jaji Sylvain Ore mara baada ya mazungumzo

Picha ya Pamoja

Waziri Mhe. Mahiga akiongea na wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya mazungumzo

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Jaji Sylvain Ore akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo

Waziri Mahiga akutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Arkadia Ltd

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ARKADIA Ltd.  Dr. Ezio Copat walipokutana kwa mazungumzo ofisini kwake mjini Dodoma 

Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akimsikiliza Dr. Copat walipokutana kwa mazungumzo mjini Dodoma
Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akifafanua jambo wakati wa mazungumzo

Mazungumzo yakiendelea

Kamati ya Kusimamia Soko la Pamoja la EAC yakutana jijini Dar Es Salaam

Mkurugenzi wa Ajira kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Bw. Amir Amir aliyeshika kipaza sauti ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kikao cha Kamati ya kusimamia utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki akifungua kikao hicho jana kwenye ukumbi wa hoteli ya Holiday In jijini Dar Es Salaam.

Bi. Agatha Nderitu akiwasilisha matokeo ya utafiti wa namna nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zilivyotekeleza Itifaki ya Soko la Pamoja kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2014 hadi 2016. Utafiti huo ulilenga maeneo ya Soko huru la bidhaa, mitaji na uhuru wa watu kusafiri ndani ya Jumuiya. Utafiti huo ulionesha kuwa nchi za EAC zimejitahidi kutekeleza Itifaki hiyo ingawa bado kuna vikwazo na sheria zinazozuia utekelezaji wa soko hilo kikamilifu hususan kwenye vikwazo visivyo vya kibiashara.

Baadhi ya washiriki wakifuatiliwa mada kuhusu tathmini ya utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la EAC

Wednesday, March 1, 2017

Naibu Waziri Mambo ya Nje akutana na Balozi wa Singapore nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (kulia) akizungumza na Balozi wa Singapore nchini, Mhe. Tan Puay Hiang, alipomtembelea Wizarani Jijini Dar es salaam.
Katika mazungumzo yao Mhe. Dkt. Kolimba alisisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili sambamba na kutambua mchango wa Serikali ya Singapore kwa Tanzania katika sekta ya Elimu sambamba na kuwajengea uwezo Watumishi wa Umma.
Mhe. Tan Puay Hiang nae akizungumza ambapo alieleza Serikali ya Singapore itaendelea kudumisha ushirikiano wa kidiplomasia uliopo baina ya Tanzania na Singapore pamoja na kuongeza maeneo ya ushirikiano hususan uwekezaji katika masuala ya nishati na miundombinu.
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo. Kulia ni Bw. Charles Faini na pembeni yake ni Bw. Emmanuel Luangisa.
Mazungumzo yakiendelea.Kushoto ni ujumbe alioambatana nao Mhe. Tan Puay Hiang.

Picha ya pamoja.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa DPRK nchini

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK) nchini, Mhe. Kim Yong Su, alipomtembelea leo katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kuzungumzia historia ya ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Tanzinia na DPRK pia walizungumzia ushirikiano katika masuala ya uchumi, hususan katika ujenzi wa miundombinu na kilimo chenye tija.
Mhe. Balozi Kim Yong Su nae akimweleza jambo Mhe. Dkt. Susan ambapo alitumia fursa hiyo kueleza namna Serikali DPRK ilivyojidhatiti katika kuhakikisha ushirikiano unazidi kuimarika kwa faida ya mataifa hayo mawili.
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo.Kushoto ni Bw. Benedict Msuya na pembeni yake ni Bw. Charles Faini.

Mazungumzo yakiendelea.
Picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo.