Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga(Mb) akiongea katika mkutano na Ujumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Msingi za Wapalestina(Committee on the exercise of Inalienable rights of the Palestinian People), kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mwakilishi wa kudumu wa Senegal katika Umoja wa Mataifa, kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Deusdedit Kaganda. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam, tarehe 04/12/2017.
Ujumbe huo uliwasili nchini tarehe 02/12/2017, dhumuni la ziara hiyo ni kuendeleza mahusiano ya kisiasa na kidiplomasia kati ya Tanzania na Palestina, pamoja na kutoa elimu ya uelewa kwa jamii ya Watanzania kuhusu hali ya Wapalestina chini ya utawala wa Israel.
Mhe. Waziri akipokea kitabu chenye kuelezea Historia ya Watu
wa Wapelestina kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati,
Mhe. Riyad Mansour ambaye pia ni mwangalizi wa kudumu
kutoka Umoja wa Mataifa wa hali ya Palestina.
Mhe. Waziri akiwa na Ujumbe wa Tanzania na Ujumbe wa
Kamati wakieendelea na Mazungumzo
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi. Mindi Kasiga wa
kwanza kushoto, anayefuata ni Bi. Ellen Maduhu kutoka Idara
ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Gerald Mbafu Msaidizi wa
Waziri na nyuma yao ni waandishi wa Habari wakifuatilia
mazungumzo hayo.
Ujumbe wa Kamati ukifuatilia mazungumzo hayo.
Mhe. Waziri akizungumza na vyombo vya habari (hawako
pichani) baada ya Mkutano.