Saturday, April 28, 2018

Watanzania Oman washerehekea miaka 54 ya Muungano kwa Mechi ya Mpira

Balozi wa Tanzania nchini Oman Mhe. Abdallah Kilima, akiwakabidhi Kombe Timu ya Zanzibar Heroes baada ya kuibuka mshindi wa mechi ya kuadhimisha miaka 54 ya Muungano dhidi ya Kilimanjaro Stars.Timu zilizoundwa na Watanzania waishio nchini Oman. Zanzibar Heroes ilishinda 2 - 1

Balozi Kilima akiwa kwenye picha ya pamoja na Timu ya Zanzibar Heroes
Balozi wa Tanzania nchini Oman akisalimiana na wachezaji wa Zanzibar Heroes na Kilimanjaro Stars kabla ya mechi hiyo ya kirafiki kusherehekea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuanza.

Friday, April 27, 2018

Tanzania na Kenya zaadhimisha mafanikio ya mahusiano ya kibiashara na kujadili mikakati ya baadae


Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Pindi Chana akitoa neno la ufunguzi katika Kongamano la biashara kati ya Tanzania na Kenya lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha kimataifa cha Kenyatta Jijini Nairobi, Kenya tarehe 27 Aprili 2018.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Chris Kiptoo ambaye pia ni mgeni rasmi katika kongamano hilo la biashara akitoa hotuba ya ufunguzi wa ambapo alieleza kuna umuhimu mkubwa wa kuongeza mzunguko wa biashara baina ya Tanzania na Kenya pia ni wakati mwafaka wa kutumia fursa za rasilimali zilizopo baina ya mataifa hayo.  

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akihutubia katika ufunguzi wa kongamano la biashara ambapo alieleza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo tayari kufanya biashara na Jamhuri ya Kenya na kwamba maadhimisho ya kipekee ya wiki ya Tanzania nchini Kenya ni mwanzo wa kuimarisha na kuboresha ushirikiano uliopo na hivyo akasisitiza ni vema uma wa mataifa haya mawili ukajielekeza katika kununua na kuuza bidhaa baina yao. 
Kaimu Mkurugenzi wa Sera na uhamasishaji na mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta binafsi (TPSF), Bi Neema Temba akitoa neno la utangulizi katika kongamano la biashara ambapo alisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kuwa na ushindani unaojenga baina yao na pia alieleza sekta binafsi ni vizuri ikatambua na kuunga mkongo jitihada za serikali katika kuweka mazingira wezeshi ya biashara.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta binafsi, Bw. Nick Nesbitt akitoa taarifa ya utangulizi ambapo alieleza kuwa kongamano hilo ni fursa muhimu kwa wafanyabiashara kukutana na kujadili masuala mbalimbali ya biashara na uwekezaji na hivyo akaipongeza serikali ya Tanzania kwa jitihada walizozianzisha.

Viongozi kutoka serikali ya Tanzania na Kenya wakifuatilia kongamano
Wajumbe wakifuatilia Kongamano.

Sehemu nyingine ya wafanyabiashara na wajumbe kutoka serikalini wakifuatilia kongamano.
Wafanyabiashara wakifuatilia kongamano.
Sehemu nyingine ya wafanyabiashara wakifuatilia kongamano.

Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya waadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo iliambatana na maonesho ya bidhaa za viwanda vya Tanzania

Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Pindi Chana akiwakaribisha wageni waalikwa katika ufunguzi  wa siku ya Tanzania ambayo huadhimishwa tarehe 26 Aprili siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Hafla ya maadhimisho hayo ilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta Jijini Nairobi, Kenya. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Ababu Namwamba ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar akihutubia wageni waalikwa waliohudhuria katika mchaparo ulioandaliwa na ubalozi wa Tanzania nchini Kenya tarehe 26 April 2018.

Viongozi wa Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jamhuri ya Kenya na Mkuu wa Mabalozi nchini Kenya wakikata keki katika kusheherekea maadhimisho ya muungano huo.

Viongozi wa Serikali kutoka Kenya na Tanzania wakifuatilia ufunguzi wa hafla hiyo, kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kenya, Balozi Macharia Kamau, Naibu Waziri Viwanda na Biashara, Mhe. Hassan Hafidh, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje, Mhe. Ababu Namwamba na Balozi mteule wa Jamhuri ya Kenya nchini Tanzania, Mhe. Kazungu Kambi.
Viongozi pamoja na wageni waalikwa wakisherehekea kwa pamoja  muungano wa Tanganyika na Zanzibar.



Sehemu ya waheshimiwa mabalozi na Wakuu wa mashirika ya kimataifa wanaowakilisha nchini Kenya wakifatilia hafla  hiyo.
Sehemu nyingine ya wawakilishi hao nchini Kenya wakifuatilia hafla.



Sehemu ya mabalozi wa Afrika wakifuatilia hafla ya maadhimisho ya miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mhe. Naibu Waziri Namwamba akisalimiana na Mhe. Naibu Waziri Hafidh. 
Sehemu ya wajumbe wa kamati ya maandalizi, viongozi na wageni waalikwa wakifuatilia hafla ya maadhimisho ya Muungano.

Picha ya pamoja
Kikundi cha muziki wa taarabu cha Zanzibar Culture group kikitumbuiza.

Wahudumu wakihudumia vinywaji kutoka kampuni za kitanzania.

Mabalozi wakabidhiwa Viwanja vya Ofisi Jijini Dodoma



Mkurugenzi wa iliyokuwa Manispaa ya Dodoma na sasa Jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi akiwaonesha Mabalozi ramani ya Mji wa Serikali ambayo ndani yake kuna viwanja vya kujenga ofisi za kibalozi jijini humo. Viwanja hivyo viligawiwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mapema mwaka huu kwa nia ya kuharakisha na kuhamasisha Jumuiya ya Kimataifa kujenga ofisi na makazi yao ya uwakilishi kwenye Makao Makuu ya nchi, Dodoma. Zoezi hilo la ugawaji wa viwanja liliratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma siku moja kabla ya mabalozi hao kuhudhuria sherehe za Muungano tarehe 26 Aprili 2018.


Sehemu ya Mabalozi na Jumuiya ya Wanadiplomasia wanaowakilisha Serikali na Mashirika ya Kimataifa nchini Tanzania, wakisikiliza maelezo ya awali kutoka kwa Mkurugenzi wa iliyokuwa Manispaa ya Dodoma na sasa Jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi (hayupo pichani) kuhusu viwanja vyao kwenye Makao Makuu ya Tanzania.

Bw. Godwin Kunambi akionesha ramani yenye viwanja 65 vyenye ekari tano kila kimoja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi na makazi ya Jumuiya ya Wanadiplomasia wanaowakilisha Serikali na Mashirika ya Kimataifa nchini Tanzania. Aliyekaa meza kuu ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw. Zakariyya Kera, Wizara ya Mambo ya Nje, akimwamwakilishi Katibu Mkuu Prof. Adolf Mkenda kwenye zoezi hilo.(Pichani juu na chini)   


Msafara wa Mabalozi ukiingia kwenye lango kuu la Mji Mpya wa Serikali, uliopo kilometa 17 kutoka katikati ya jiji eneo la Mtumba, ambapo viwanja hivyo vimetengwa maalum kwa ajili ya Jumuiya ya Diplomasia nchini Tanzania. 



Baadhi ya Mabalozi wakimsikiliza Bw. Godwin Kunambi na wataalam wake (hawapo pichani) wakielezea michoro mbalimbali ya miundombinu kwenye eneo hilo la wanadiplomasia. (Pichani juu na chini)







Sehemu ya msafara wa Mabalozi (juu na chini) 


Baadhi ya Mabalozi wakimsikiliza Mtaala wa miundombinu wa Jiji la Dodoma kwenye eneo hilo la wanadiplomasia. (Pichani juu na chini) 



Afisa Utawala wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisaidia kutoa ufafanuzi kwa wanadiplomasia waliotembelea eneo la viwanja lililopo Mtumba kilometa 17 kutoka katikati ya Jiji la Dodoma.


Baadhi ya wanadiplomasia wakiwa na nyuso za furaha kwenye kiwanja cha Ubalozi wa Zambia pamoja na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje. Kiwanja hicho cha mfano kilisafishwa kwa lengo la kuonesha ukubwa wa viwanja hivyo vilivyotolewa na Rais Magufuli ili kufanikisha uhamiaji wa Balozi hizo Jijini Dodoma, makao makuu ya nchi.


Magari ya kusafisha kiwanja yakiwa kwenye eneo la kiwanja cha mfano cha Ubalozi wa Zambia ambapo Mabalozi walitembelea.

(Juu na Chini)
Baadhi ya Mabalozi wakiingia kwenye eneo la kiwanja cha Ubalozi wa Zambia, lilipo kwenye eneo la Mtumba Jijini Dodoma.

Tanzania yajikita kutumia fursa za soko la Afrika Mashariki

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akiongea na wawakilishi kutoka kampuni ya Agricom Afrika Ltd walioshiriki maonesho ya bidhaa za viwanda vya Tanzania nchini Kenya yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta Jijini Nairobi, Kenya tarehe 27 Aprili 2018.

=======================================

Tanzania yajikita kutumia fursa za soko la Afrika Mashariki.

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesisitiza kuendelea kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali za Tanzania na Kenya ili kuhakikisha bidhaa na mazao ya kilimo yanayozalishwa na wananchi yanapata soko la kuaminika katika ukanda wa Afrika Mashariki hususan Kenya.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda alipotembelea maonesho ya bidhaa za viwanda vya Tanzania nchini Kenya, yaliyofunguliwa rasmi na Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji, Mhe. Mwangi Kiunjuri tarehe 25 April, 2018 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi, Kenya.

Maonesho hayo ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Tanzania nchini Kenya ambayo imeambatana na maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Kongamano la biashara kati ya Tanzania na Kenya ambapo lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wafanyabiashara wa mataifa hayo ili waweza kufanya makubaliano ya kibiashara, kupeana uzoefu na kuwezesha bidhaa za viwanda vya Tanzania kupenyeza katika soko la Kenya kama ambavyo bidhaa na huduma za wakenya zilivyoingia katika soko la Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Aidha, aliongeza ushirikiano huo utasaidia kukuza biashara na uwekezaji na hivyo kuongeza ajira, kuinua pato la taifa na kipato cha mtu mmoja mmoja kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi kwa ujumla. ‘’ Tanzania itaendelea kushirikiana na mataifa yote na itaendelea kufata taratibu na kanuni za biashara zilizokubaliwa kimataifa” alisema Prof. Mkenda

Vilevile Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji alipata fursa ya kutembelea maonesho hayo ya bidhaa ambapo alisisitiza  umuhimu wa kuthamini bidhaa zetu na kwamba Serikali ya Tanzania na Kenya zitaendelea kuimarisha undugu na mshikamano uliopo kama ilivyokubaliwa na marais wa Tanzania na Kenya walipokutana Kampala, Uganda katika Mkutano wa 19 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo waliwataka viongozi katika nchi zao kumaliza vikwazo vya kibiashara.  “ Serikali itaendelea kuweka mazingira wezesha kwa wafanyabiashara hivyo natoa rai kwa wafanyabiashara wote kufuata taratibu na masharti katika kufanya biashara zao” alisema Prof. Ole Gabriel

Wiki ya Tanzania nchini Kenya imeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia ubalozi wake wa Nairobi, Kenya kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Bara), Wizara ya Viwanda na Biashara (Serikari ya Mapinduzi Zanzibar), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Taasisi ya Sekta Binafsi, Wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa Tanzania ambao walijitoa kwa hali mali katika kudhamini ili kufanikisha Wiki ya Tanzania nchini Kenya.

Prof. Adolf Mkenda pamoja na maafisa waandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji wakipata ufafanuzi wa biashara ya matunda na mboga mboga kutoka kampuni ya Agricom.



Prof. Mkenda akipata ufafanuzi wa ubora na matumizi ya mabomba yanayotengenezwa na kampuni ya kitanzania ya PLASCO LTD kutoka kwa Mhandisi Elisaria Aminiel.

Mmoja wa Mabalozi wanaowakilisha nchini Kenya akinunua mkanda kutoka banda la kampuni ya kitanzania inayozalisha bidhaa za ngozi WOISO Original Products, Pembeni ni mwakilishi kutoka kampuni hiyo, Bw. Justine Msigwa.

Ubalozi wa Tanzania, Uingereza waadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanzania kwa Ibada Maalum

Juu na Chini ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Dkt. Asha Rose-Migiro (katikati) akiwa na Watumishi wa Ubalozi pamoja na Watanzania waishio nchini Uingereza mara baada ya kumaliza Ibada Maalum ya kuadhimisha Miaka 54 ya Muungano wa Tanzania ambayo ilifanyika kwenye Kanisa la Westminster Abbey Jijini London.


Naibu Waziri akutana na kufanya mazungumzo na mshindi wa shindano la 28 la urembo katika taji la World Miss University Africa 2017

Mhe. Dkt. Susan Kolimba Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akizunguza na Bi. Queen Elizabeth Manule mshindi wa shindano la 28 la urembo katika taji la World Miss University Africa (2017) lililofanyika Cambodia tarehe 20 Desemba, 2017.Membo Bi. Queen Elizabeth alikuja kumsalimu Naibu Waziri na kuomba ushirikiano kutoka Wizarani na Serikalini kwa ujumla katika kutekeleza mpango wake wa kutangaza amani Duniani na kusaidia jamii.

Mhe. Naibu Waziri alimshukuru kwa kuja kumsalimia na kumpongeza kwa ushindi alioupata ambao unaitangaza Tanzania nje ya mipaka ya nchi.

Alimtaka ajivunie ushindi huo aliopata na kuwa mfano mzuri kwa wasichana wengine katika masomo na kuhudumia jamii inayomzunguka. Alimuahidi ushirikiano wa Wizara katika masuala ambayo ameazimia kuyafanya kwa ajili ya Jamii na kuitangaza Tanzania.
Mrembo Bi. Queen Elizabeth Manule ni mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Shahada ya Kwanza (Public Sector Accounting and Finance) katika Chuo cha Uhasibu (TIA).
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt.Susan Kolimba akisalimiana na Bi. Queen Elizabeth Manule walipokutana kwa mazungumzo Wizarani jijini Dodoma

Naibu Waziri Mhe. Dkt.Susan Kolimba akimsiliza Mrembo Bi. Queen Elizabeth Manule wapokutana kwa mzungumzo Wizarani jijini Dodoma.