Friday, April 27, 2018

Mabalozi wakabidhiwa Viwanja vya Ofisi Jijini Dodoma



Mkurugenzi wa iliyokuwa Manispaa ya Dodoma na sasa Jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi akiwaonesha Mabalozi ramani ya Mji wa Serikali ambayo ndani yake kuna viwanja vya kujenga ofisi za kibalozi jijini humo. Viwanja hivyo viligawiwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mapema mwaka huu kwa nia ya kuharakisha na kuhamasisha Jumuiya ya Kimataifa kujenga ofisi na makazi yao ya uwakilishi kwenye Makao Makuu ya nchi, Dodoma. Zoezi hilo la ugawaji wa viwanja liliratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma siku moja kabla ya mabalozi hao kuhudhuria sherehe za Muungano tarehe 26 Aprili 2018.


Sehemu ya Mabalozi na Jumuiya ya Wanadiplomasia wanaowakilisha Serikali na Mashirika ya Kimataifa nchini Tanzania, wakisikiliza maelezo ya awali kutoka kwa Mkurugenzi wa iliyokuwa Manispaa ya Dodoma na sasa Jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi (hayupo pichani) kuhusu viwanja vyao kwenye Makao Makuu ya Tanzania.

Bw. Godwin Kunambi akionesha ramani yenye viwanja 65 vyenye ekari tano kila kimoja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi na makazi ya Jumuiya ya Wanadiplomasia wanaowakilisha Serikali na Mashirika ya Kimataifa nchini Tanzania. Aliyekaa meza kuu ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw. Zakariyya Kera, Wizara ya Mambo ya Nje, akimwamwakilishi Katibu Mkuu Prof. Adolf Mkenda kwenye zoezi hilo.(Pichani juu na chini)   


Msafara wa Mabalozi ukiingia kwenye lango kuu la Mji Mpya wa Serikali, uliopo kilometa 17 kutoka katikati ya jiji eneo la Mtumba, ambapo viwanja hivyo vimetengwa maalum kwa ajili ya Jumuiya ya Diplomasia nchini Tanzania. 



Baadhi ya Mabalozi wakimsikiliza Bw. Godwin Kunambi na wataalam wake (hawapo pichani) wakielezea michoro mbalimbali ya miundombinu kwenye eneo hilo la wanadiplomasia. (Pichani juu na chini)







Sehemu ya msafara wa Mabalozi (juu na chini) 


Baadhi ya Mabalozi wakimsikiliza Mtaala wa miundombinu wa Jiji la Dodoma kwenye eneo hilo la wanadiplomasia. (Pichani juu na chini) 



Afisa Utawala wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisaidia kutoa ufafanuzi kwa wanadiplomasia waliotembelea eneo la viwanja lililopo Mtumba kilometa 17 kutoka katikati ya Jiji la Dodoma.


Baadhi ya wanadiplomasia wakiwa na nyuso za furaha kwenye kiwanja cha Ubalozi wa Zambia pamoja na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje. Kiwanja hicho cha mfano kilisafishwa kwa lengo la kuonesha ukubwa wa viwanja hivyo vilivyotolewa na Rais Magufuli ili kufanikisha uhamiaji wa Balozi hizo Jijini Dodoma, makao makuu ya nchi.


Magari ya kusafisha kiwanja yakiwa kwenye eneo la kiwanja cha mfano cha Ubalozi wa Zambia ambapo Mabalozi walitembelea.

(Juu na Chini)
Baadhi ya Mabalozi wakiingia kwenye eneo la kiwanja cha Ubalozi wa Zambia, lilipo kwenye eneo la Mtumba Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.