Thursday, April 12, 2018

Waziri Mahiga ampokea nchini Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland, Mhe. Prof. Jacek Czaputowicz mara baada ya kumkaribisha rasmi Wizarani tarehe 12 Aprili, 2018. Katika mazungumzo yao walisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali zikiwemo elimu, kilimo, utalii, biashara na uwekezaji. Mhe. Czaputowicz yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo pamoja na mambo mengine atazindua rasmi ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini.
Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Waziri Czaputowicz wakionesha Mkataba wa Makubaliano kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na Poland.
Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Grace Martin (kulia)  kwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Salvator Mbilinyi (kushoto), Afisa Mambo ya Nje, Bi. Mona Mahecha (wa pili kushoto) na Afisa Mawasiliano, Bi. Robi Bwiru (wa pili kulia) wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri Mahiga na Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland, Mhe. Czaputowicz (hawapo pichani).
Balozi wa Poland nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski (kulia) akiwa na Wajumbe wengine kutoka Poland  wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Waziri Mahiga na Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland, Mhe  Czaputowicz (hawapo pichani)
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.