Thursday, April 12, 2018

Waziri Mahiga ahimiza wadhamini zaidi kujitokeza kufanikisha Wiki ya Tanzania nchini Kenya

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiwa na  Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania nchini Kenya, Balozi Anisa Mbega walipokutana na Wadhamini na Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya maonesho hayo (hawapo pichani) yanayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 25 - 28 Aprili 2018 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi, Kenya. 

Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 12 Aprili 2018 katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam  na kuambatana na hafla ya kukabidhi udhamini kwa ajili ya  kufanikisha  maonesho hayo maarufu kama ''Wiki ya Tanzania nchini Kenya'' ambayo yataenda sambamba na sherehe za miaka 54 za Muungano wa Tanzania. 


Sehemu ya wadhamini na  wajumbe wa kamati ya maandalizi wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiongozwa na Mhe. Waziri Mahiga (hayupo pichani)
Viongozi wa Kampuni ya NIDA TEXTILE MILLS (T) wakimkabidhi Mhe. Waziri Mahiga mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi 22,700,000/- kwa ajili ya kudhamini maonesho ya didhaa za viwanda vya Tanzania nchini Kenya. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Muhammad Waseem.

Mhe. Waziri Mahiga akimshukuru Mwakilishi wa Kampuni ya Mohamed Enterprises, Bi. Barbara Gonzale baada ya kutoa ahadi ya udhamini wa kiasi cha shillingi millioni ishirini na tano (25,000,000) kwa ajili ya kudhamini maonesho hayo.
Mhe. Waziri Mahiga akimshukuru mwakilishi kutoka kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd, Bw. Maleke Hans baada ya kutoa ahadi ya udhamini wa kiasi cha Dola za Marekani 5,000 (sawa na shilingi milioni kumi na moja  za Tanzania).
Mhe. Waziri Mahiga akisikiliza taarifa fupi ya udhamini na hatua ya maandalizi iliyofikiwa  kutoka kwa Katibu wa Kamati, Balozi Mbega, pembeni ni baadhi ya Wadhamini na Wajumbe wa Kamati.
Sehemu nyingine ya wajumbe wa kamati wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa ukitolewa na Balozi Mbega kwa Mhe. Waziri Mahiga.
Picha ya pamoja.



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.