Thursday, April 12, 2018

Poland yafungua rasmi Ofisi za Ubalozi nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland, Mhe. Prof. Jacek Czaputowicz wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Ofisi za Ubalozi wa Poland hapa nchini. Ufunguzi wa Ofisi za Ubalozi huo zilizopo Masaki, Jijini Dar es Salaam ulifanyika tarehe 12 Aprili, 2018. Ili kuimarisha na kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Poland, nchi hiyo ilifungua tena Ubalozi wake hapa nchini mwaka 2017 baada ya kuufunga mwaka 2008 na kabla ya uzinduzi wa ofisi hizi hapo nchi hiyo ilikuwa inawakilishwa kutokea Nairobi, Kenya.
Waziri Mahiga akimpongeza Waziri Czaputowicz kwa uamuzi wa nchi hiyo wa  kufungua Ofisi za Ubalozi hapa nchini.
Mhe. Waziri Mahiga kwa pamoja na Mhe. Waziri Czaputowicz wakizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa ufunguzi wa ofisi za Ubalozi wa Poland nchini.
Mkutano kati ya Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Waziri Czaputowicza na waandishi wa habari ukiendelea.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.