Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka H. Luvanda akimvalisha cheo cha Brigedia Jenerali A.S Mwami ambaye ni Mwambata Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini India.Brigedia Jenerali A.S Mwami ni miongoni mwa Maafisa Wakuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania ambao Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliwapandisha vyeo tarehe 12 Aprili, 2018. Awali Brigedia Jenerali Mwami alikuwa na cheo cha Kanali. Hafla hiyo fupi imefanyika katika Ubalozi wa Tanzania nchini India na kuhudhuriwa na watumishi wa ubalozi huo. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.