ZIARA
YA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA BRAZIL NCHINI 14 – 17, APRILI, 2018
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil, Mhe.
Balozi Fernando Jose Marroni de Abreu anatarajia kufanya ziara hapa nchini
kuanzia tarehe 14 hadi 17 Aprili, 2018.
Katika ziara hiyo,
pamoja na mambo mengine, atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Susan Alphonce
Kolimba tarehe 16 Aprili, 2018. Viongozi hawa watajadiliana namna ya kuboresha
mahusiano na mashirikiano ya kidiplomasia baina ya Tanzania na Brazil, hususan
katika eneo la uwekezaji na biashara.
Mhe. Dkt. Kolimba na
Mhe. Balozi Fernando Jose Marroni de Abreu wanatarajiwa kushiriki kwenye
majadiliano ya kisiasa, mambo makubwa yatakayojadiliwa ni; Ushirikiano wa
kiuchumi na biashara ikiwemo, matokeo ya kusainiwa kwa mkataba wa msamaha wa
deni la Tanzania kwa Brazil, pamoja na masuala mengine yenye maslahi kwa
wote kiuchumi na kibiashara, taathmini ya utekelezaji wa Mradi wa Pamba Ziwa
Victoria ‘Cotton Victoria Project’ na kuimarisha ushirikiano katika sekta ya
mifugo nchini hususan kusaidia jitihada za Serikali za kuboresha ufugaji wa ng’ombe
aina ya zebu.
Aidha, katika
majadiliano hayo pia watazungumzia
kuhusu Masuala ya kimataifa hususan mageuzi ya Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa, na Masuala ya Kikanda hasa Migogoro ya kisiasa nchini Sudan
ya Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Burundi.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
13 Aprili, 2018
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.