Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (Mb.) akihutubia kwenye Mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani, unaowakutanisha wadau mbalimbali wanao simamia na kutengeneza vifaa na miundombinu mbalimbali ya Tehama. Mkutano huo unatarajia kuangalia namna mbalimbali za kupambana na matumizi ya Tehama yanayochafua mazingira; umehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Serikalini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, akiwemo Waziri wa Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Dkt. Sira Ubwa (Mb.), Katibu Mkuu (Mawasiliano) Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Mwinyi, Mkurugenzi wa ITU (International Telecomunication Union), Dkt. Chaesub Lee, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Mhandisi Kilaba. Mkutono huo unafanyika katika Hoteli ya Sea Clif Mangapwani, Zanzibar kuanzia tarehe 9-12, Aprili 2018. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.