Tuesday, October 16, 2018

Dkt. Ndumbaro akutana na Balozi wa Uganda,Uingereza na Kaimu Balozi wa Marekani

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro(Mb.) na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe wamekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani Bi. Inmi Patterson. Katika mazungumzo yao Bi. Patterson alitumia firsa hiyo kujitambulisha na kuwampongeza kwa kuteuliwa kuwa Naibu Waziri na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo. Aidha, Dkt Ndumbaro amemuhakikishia Bi. Patterson kumpa ushirikiano wa karibu katika kutekeleza majukumu yake. Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam Tarehe 16/10/2018
Mazungumzo yakiendelea,  wa pili kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe na wakwanza kulia ni Katibu wa Naibu Waziri Bw. Charles Faini na wa kwanza kushoto ni Afisa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.  
Dkt. Ndumbaro akiagana na Bi. Patterson


=====Dkt. Ndumbaro akutana na Balozi Cooke=====





Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damasi Ndumbaro (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza hapa nchini Mhe. Sarah Cooke, katika Mazungumzo hayo Mhe. Cooke ametumia fursa hiyo kujitambulisha na kuwapongeza Mhe. Ndumbaro pamoja na Katibu Mkuu Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (hayupo pichani). Aidha, Balozi Cooke alimweleza Dkt. Ndumbaro pamoja na Dkt. Mnyepe kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza ni wa muda mrefu ambapo nchi hizi mbili zinashirikiana katika sekta mbalimbali za kukuza uchumi zikiwemo Elimu, Afya na Kilimo. Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam Tarehe 16/10/2018
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (wa kwanza kushoto), pamoja na Maafisa wa Mambo ya Nje, wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Dkt. Ndumbaro na Balozi Cooke.
Picha ya pamoja mara ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya Dkt. Ndumbaro (wa pili kulia) na Balozi Cooke (wa pili kutoka kushoto), Dkt. Mnyepe pamoja na Afisa Ubalozi wa Uingereza Bw. Matt Sutherlal 



======Dkt. Ndumbaro akutana na Mhe. Kabonero=======  




Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damasi Ndumbaro (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uganda nchini Mhe. Richard T. Kabonero. Katika Mazungumzo hayo Mhe. Kabonero ametumia fursa hiyo kujitambulisha na kumpongeza Mhe. Ndumbaro pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (hayupo pichani). Aidha, Balozi Kabonero alitumiafursa hiyo kumweleza Dkt. Ndumbaro pamoja na Dkt. Mnyepe kuwa mahusiano kati ya Tanzania na Uganda ni ya muda mrefu, ambapo kutokana na mahusiano mazuri kati ya nchi hizi imepelekea Serikali ya Uganda kuamua kupitisha ujenzi wa bomba la mafuta tanzania, ambapo ujenzi huo utazalisha fursa mbalimbali na kukuza vipato vya wananchi wa pande zote mbili pamoja na kukuza uchumi baina ya mataifa hayo mawili. Pia ameupongeza ufanisi mzuri wa Bandari ya Dar es Salaam katika kuwa hudumia.

Kwa upande wa Dkt. Ndumbaro amemuhakikishia Balozi Kabonero kumpatia ushrikano wa kutosha wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ya kuiwaikilisha Taifa lake hapa nchini, Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam Tarehe 16/10/2018
Katibu Mkuu wa Wizaraya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (wa kwanza kushoto), pamoja na Maafisa Mambo ya Nje wafuatilia kwa makini mazungumzo hayo. 
Mazungumzo yakiendelea
Mhe. Dkt. Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Kabonero.
Picha ya pamoja.





Monday, October 15, 2018

Ubalozi wa Tanzania, Komoro waadhimisha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

UBALOZI WA TANZANIA VISIWANI COMORO WAADHIMISHA SIKU YA MWALIMU NYERERE
TAREHE 13 Oktoba, 2018
Ubalozi wa Tanzania Visiwani Comoro kwa kushirikiana na Umoja na Vijana Visiwani hapa ujilikanao kama Udjamaa wa Komori na Afrika Mashariki tarehe 13 Oktoba, 2018 uliadhimisha siku ya Mwalimu Nyerere (Nyerere Day). Maadhimisho hayo yalifanyika katika ukumbi wa mkutano wa Ubalozi uliopo katika mtaa wa Oasis, Moroni, Visiwani Comoro.
Hii ni mara ya kwanza kufanyika maadhimisho hayo Visiwani hapa ambapo lengo lake ilikuwa ni:-
i.              Kuonyesha mchango wa Mwalimu Nyerere na Tanzania kwa ujumla katika ukombozi wa Visiwa vya Comoro.
ii.            Kuelezea historia ya baba wa Taifa hasa kwa Vijana wa Comoro amabapo historia hiyo ilipotea kutokana na juhudi za Mfaransa.
iii.          Kudumisha ushirikiano wa kihistoria na kindugu uliopo baina ya Tanzania na Comoro hasa kwa kuzingatia kwamba Comoro ipo katika harakati za kujianga kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Katika maadhimisho hayo, Balozi wa Tanzania, Visiwani Comoro, Mhe. Sylvester M. Mabumba alifanya mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari viliopo Visiwani hapa na kuelezea kuhusu maisha na Mwalimu Nyerere na mchango wake katika harakati za ukombozi kwa Bara la Afrika. Aidha, katika hilo Mhe. Balozi alisistiza kudumisha amani Visiwani Comoro wakati nchi hiyo ikielekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Rais mapema mwaka 2019.
Balozi wa Tanzania Visiwani Komoro Mhe. Sylvester M. Mabumba akifanya mahojiano na Vyombo mbalimbali vya Habari Visiwani Komoro
Balozi Mabumba (wa tano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Umoja wa Vijana wa Komoro maarufu kama Udjamaa wa Komoro na Afrika Mashariki



Naibu Waziri Dkt. Ndumbaro awa mgeni rasmi maadhimisho ya Taifa la Hispania

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro akihutubia wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya Taifa la Hispania iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi. Katika hotuba yake Mhe. Naibu Waziri ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Uhispania. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mabalozi na wageni mbalimbali.
Kaimu Balozi wa Hispania Bibi. Teresa Martin naye akihutubia kwenye hafla hiyo 
Juu na Chini Sehemu ya Mabalozi na Wageni mbalimbali walio hudhuria hafla hiyo




Wednesday, October 10, 2018

Maoni ya Muswada wa Sheria ya Madini wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kukusanywa

Mwenyekiti wa Kamati ya kukusanya maoni kuhusiana na muswada wa Madini wa Afrika Mashariki Bi. Uwumukiza Francise, akionyesha kitabu cha muongozo wa utekelezaji wa shughuli za kibunge za Bunge la Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kukusanya maoni kwa wadau wa kila nchi wanachama wa Afrika Mashariki, ili kuuboresha kabla bunge halijaupitisha.  Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali, mkutano huo umefanyika kwenye Hotel ya Tiffany iliyopo jijini Dar es Salaam tarehe 10. 10. 2018 
Dkt. Abdullah H. Makame akichangia jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. 
Sehemu ya wadau waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia kwa makini ufunguzi huo
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Josephine Sebastian Lemoyan naye alipata fursa ya kuchangia kwenye mkutano huo ambapo alisema wanawake bado ni wadhaifu katika sekta ya madini  kwakua wana fursa chache za mitaji ya Madini. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Joachim Otaru naye akielezea jambo kwenye mkutano huo 
Maafisa kutoka Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kwa makini mkutano huo, katikati ni Bw. Amedeusi Mzee akichangia mada juu ya mswada huo wa madini, wa kwanza kulia ni Bw. Abel Maganya pamoja na Bi. Laila Kagombola ( wa kwanza kushoto) wakisikiliza kwa makini maoni yaliyokuwa yakitolewa.
Picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa Mkutano










Tuesday, October 9, 2018

Tanzania kushiriki mazoezi ya kikosi cha dharura cha SADC nchini Malawi


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) zimejipanga kuzuia na kudhibiti madhara yanayosababishwa na machafuko ya kisiasa katika jumuiya hiyo na Bara la Afrika kwa ujumla. Wawakilishi wa nchi hizo wamekusanyika nchini Malawi kuanzia tarehe 1 Oktoba hadi 17 Oktoba 2018 kwa ajili ya kufanya mazoezi ya namna ya kutuliza ghasia pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathirika katika kipindi cha machafuko

Wawakilishi wa Tanzania kutoka Jeshi la Wananchi, Magereza na taasisi za kiraia ikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni miongoni mwa watu 600 wanaoshiriki zoezi hilo lililopewa jina la EX UMODZI CPX 2018 na kaulimbiu ya Afrika ni Amani na Maendeleo (Africa for peace and prosperity).

Katika hafla ya ufunguzi wa mazoezi hayo iliyofanyika leo tarehe 08 Oktoba, 2018 katika Chuo cha Kijeshi cha Malawi kilichopo mji wa Salima takriban kilomita 120 kutoka Lilongwe, Naibu Waziri wa Ulinzi wa Malawi, Mhe. Evaton Chemulirenji alisema mazoezi hayo ni utekelezaji wa maazimio ya SADC na Umoja wa Afrika (AU) wa kuandaa kikosi cha kukabiliana na machafuko barani Afrika (Standby Force-SF) ambacho kinatakiwa kiwe kimekamilika ifikapo Januari 2019.

Alisema madhumuni ya mazoezi hayo ni kuhakikisha kuwa kikosi cha SF kinapewa mafunzo ya vitendo ya kutosha ili kiwe na ujuzi na mbinu za kushiriki operesheni za kulinda amani na/au kuingilia kati na kuzuia machafuko (peace keeping and enforcement) pale yanapotokea barani Afrika. Aidha, alisema mazoezi hayo ni muhimu kwa kuwa yatasaidia kuimarisha ushirikiano na kuaminiana baina ya nchi wanachama wa SADC.

Mazoezi hayo yanajumuisha makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na majeshi  ya ulinzi,  askari polisi, askari magereza na raia wa fani tofauti kama vile za Utawala wa Sheria, siasa, mawasiliano, Utawala, haki za binadamu na jinsia ambao wana mchango mkubwa katila masuala ya operesheni za kulinda amani.

Wanajeshi watafanya zoezi la namna ya kutuliza machafuko na raia watajifunza namna ya kusaidia jamii punde tu machafuko yanapodhibitiwa na vikosi vya usalama.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Salima, Malawi

08 Oktoba 2018

Naibu Waziri wa Wizara ya Ulinzi wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Evaton Chimulirenji akitoa hotuba wakati wa hafla ya ufunguzi  rasmi wa mafunzo na mazoezi ya namna ya kutuliza ghasia pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathirika katika kipindi cha machafuko iliyofanyika tarehe 08 Oktoba, 2018 katika Chuo cha Kijeshi cha Malawi kilichopo katika mji wa Salima nje kidogo ya jiji la Lilongwe.Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Sekretarieti ya SADC yanajumuisha makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na majeshi  ya ulinzi,  askari polisi, askari magereza na raia wa fani tofauti kama vile za Utawala wa Sheria, siasa, mawasiliano, Utawala, haki za binadamu na jinsia ambao wana mchango mkubwa katila masuala ya operesheni za kulinda amani.

Mratibu wa Program ya Mafunzo yanayofanyika nchini Malawi akieleza mpangilio wa program ya mafunzo hayo kwa ujumla

Mratibu Mkuu wa Mafunzo hayo Meja Jenerali A.B Mhone naye akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo
Naibu Waziri wa Ulinzi wa Malawi  Mhe. Evaton Chimulirenji (kushoto) akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Malawi Generali Supini Phiri (kulia) pamoja na Mkuu wa Misheni ya mafunzo hayo, Mhe. Bi. Eunice Lumbia



Sehemu ya viongozi wa kijeshi wakifuatilia hotuba zilizokuwa zinatolewa wakati wa ufunguzi huo
Kikosi cha Tanzania kinachoshiriki mafunzo hayo kikiwa kimetulia wakati wa gwaride rasmi la ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo. Kikosi hicho kinajumuisha wanajeshi, askari magereza na raia kutoka fani mbalimbali za utawala, siasa na mawasiliano

Kikosi cha Malawi ambao ni wenyeji wa mafunzo hayo kikiwa kimetulia wakati wa gwaride la ufunguzi rasmi wa mafunzo
Kikosi cha Tanzania kikiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Zakarriya Kera (kushoto) ambaye pia ni kiongozi wa washiriki kutoka kundi la Raia kwenye mafunzo hayo akiwa katika picha na baadhi ya washiriki ambao ni wanajeshi na raia kutoka Tanzania.


Sunday, October 7, 2018

Dkt. Mahiga ashiriki Mkutano wa TICAD

Kufuatia  mwaliko wa Mhe. Taro Kono, Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ameshiriki Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika, (Tokyo International Conference for African Development-TICAD). Mkutano huo umeanza tarehe 6-7 Oktoba, 2018, Tokyo, Japan.

Mkutano huo ambao umewashirikisha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika, pamoja na masuala mengine, unajadili maazimio ya Mkutano wa Tano na wa Sita wa TICAD iliyofanyika mwaka 2013 na 2016, pamoja na kuandaa agenda za Mkutano wa Wakuu wa nchi wa TICAD VII unaotegemea kufanyika Yokohama, mwezi Agosti, 2019.
 
Masuala yaliyojadiliwa ni pamoja; Changamoto tangu kukamilika kwa TICAD VI mwaka 2016; Mageuzi ya kiuchumi na ukuaji shirikishi; Kuimarisha sekta ya Afya, Amani na Usalama katika jamii na; kuimarisha mawasiliano barani Afrika na duniani kote. Maeneo haya yanaenda sambamba na   Agenda 2030 ya Umoja wa Mataifa na Agenda 2063 ya Umoja wa Afrika.
Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akisikiliza kwamakini wakati Mawaziri wengine wakichangia mada kwenye mkutano huo Tokyo, Japan.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga mara baada ya kushiriki mkutano wa ngazi ya Mawaziri, alipata fursa ya kukutana na Waziri wa MAmbo ya Nje wa Japan Mhe. Taro Kono, katika mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Japani katika sekta mbalimbali. Aidha, Dkt. Mahiga aliishukuru serikali ya Japani kwa Mchango wake wa kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo nchini Tanzania hususani miundombinu ya barabara.  Kwa upande wake, Mhe. Kono amesifia jitihada za Serikali ya Tanzania katika kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi, ushirikiano katika ngazi za kimataifa, na kuipongeza Tanzania katika kukuza na kulinda usalama barani Afrika na duniani 
Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Mhe. Sameh Shoukry walipokutana kwenye Mkutano wa TICAD ngazi ya Mawaziri nchini Japan.
Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Bi Sadako Ogata, aliyekuwaga Mkurugenzi wa UNHCR mara baada ya kumalizika mkutano wa TICAD uliyofanyika Tokyo Japan.





Thursday, October 4, 2018

Naibu Waziri Dkt. Ndumbaro awa mgeni rasmi maadhimisho ya Taifa la Ujerumani

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akihutubia wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya Taifa la Ujerumani iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Katika hotuba yake Mhe. Naibu Waziri ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Ujerumani. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mabalozi na wageni mbalimbali

Mhe. Dkt. Ndumbaro akimsikiliza Balozi wa Ujerumani nchini, Mhe. Detlef Wachter alipokuwa akimweleza jambo wakati wa hafla ya siku ya Taifa la Ujerumani

HAFLA YA UPOKEAJI WA HATI ZA UTAMBULISHO WA MABALOZI WA NCHI MBALIMBALI.IKULU DSM


Wednesday, October 3, 2018

Rais Dkt. Magufuli amuapisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe kuwa Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe  Magufuli  akimkambidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha  Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea saluti toka kwa Ndg. Mwantumu Bakari Mahiza muda mfupi baada ya kumuapisha kuwa Skauti Mkuu wa Chama Cha Skauti Tanzania. Aliyeketi ni Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe aliyemuapisha kuwa Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro, Katibu Mkuu kiongozi Balozi John Kijazi na Skauti Mkuu Ndg. Mwantumu Bakari Mahiza pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama  baada ya kuwaapisha Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe na Skauti Mkuu wa Tanzania Ndg. Mwantumu Bakari Mahiza Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 20 Ikulu jijini Dar es salaam.





Sunday, September 30, 2018

Rais Dkt. Magufuli amuapisha Dkt. Ndumbaro kuwa Naibu Waziri

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha  Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe  Magufuli  akimkambidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha  Dkt. Damas  Daniel Ndumbaro kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Jaji Mstaafu Harold Nsekela akimuongoza  Dkt. Damas Daniel Ndumbaro  kula kiapo cha maadili ya viongozi baada ya kumuapisha kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea  baada ya kumuapisha  Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri Mhe. Job Ndugai na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya pamoja baada ya Dkt. Damas Daniel  Ndumbaro  kuapishwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika.