Monday, November 19, 2018

Dkt. Mahiga amwakilisha Mhe. Rais Magufuli katika Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Dkt. Mahiga amwakilisha Mhe. Rais Magufuli katika Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU

Mhe. Augustine P. Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alimwakilisha Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano Maalum wa 11 wa Wakuu Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliyofanyika tarehe 17-18 Novemba, 2018 mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mkutano huo, uliitishwa kufuatia maamuzi ya Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika mwezi Julai 2018 mjini Nouakchott, Mauritania ambapo Wakuu hao walielekeza uitishwe Mkutano Maalum kujadili kwa kina mabadiliko ya kitaasisi ndani ya Umoja huo.

Mkutano huo ulijadili na kutolea maamuzi mapendekezo kuhusu Muundo wa Uongozi (Portfolios) za Kamisheni za Umoja wa Afrika; chaguzi za Uongozi wa Kamisheni; Kusitisha ajira za viongozi wa Kamisheni; na Mabadiliko ya kiutawala na fedha ikijumuisha utendaji.
Mkutano ulikubaliana kupunguza idadi ya wajumbe wa Kamisheni klutoka 10 hadi 8 ambao ni Mwenyekiti wa Kamisheni, Makama Mwenyekiti na Makamishna 6. Maamuzi hayo yataanza kutekelezwa mwaka 2021 baada ya uongozi wa Kamisheni uliopo sasa kumaliza muda wake. Maamuzi yote yaliyotolewa yalilenga kuboresha utendaji wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika.

Mhe. Waziri aliungana na viongozi wengine waliochangia katika mjadala wa kuboresha utendaji wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kuunga mkono mabadiliko ya kitaasisi katika Umoja huo. Mhe. Waziri alieleza kwamba maamuzi hayo yanalenga kuleta ufanisi kwenye kutekeleza majukumu ya Kamisheni na kuhakikisha Afrika inapata maendeleo inayostahili haswa kwa kuzingatia Agenda 2063 ya Umoja wa Afrika.

Katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Mhe. Paul Kagame alitoa salamu za rambirambi kwa Serikali za Tanzania, DRC na Malawi kufuatia vifo vya walinda amani wa nchi hizo nchini DRC.
Mhe. Waziri alimshukuru Mhe. Kagame kwa salamu hizo za rambirambi na kuahidi kwamba Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele kupigania amani ya kudumu barani Afrika.

Mkutano pia ulijadili Mamlaka ya Wakala wa Maendeleo ya Umoja wa Afrika (African Union Development Agency - AUDA). Mkutano ulifahamishwa kuwa mchakato wa kubadilisha Taasisi ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Uchumi (New Economic Partnership for Africa’s Development – NEPAD) kuwa AUDA utakamilika Februari 2019 kama inavyoelekezwa katika Maaumuzi ya Umoja wa Afrika Na. 691. Mkutano ulikubaliana na mapendekezo yote kuhusu Mamlaka ya AUDA na kwamba programu na miradi ya AUDA itafadhiliwa kupitia bajeti ya Umoja wa Afrika na misaada ya washirika wa maendeleo.

Agenda nyingine iliyojadiliwa wakati wa mkutano huo ni mabadiliko katika Taasisi ya Mchakato wa Kujitathimini kiutawala Bora Africa (African Peer Review Mechanism - APRM), ambapo mapendekezo yalitolewa ya kuiunganisha APRM kuwa moja ya taasisi za Umoja wa Afrika na kugharamia shughuli zake kwa kutumia bajeti ya Umoja huo. Aidha, iliamuliwa kuwa Wanachama wote wa Umoja wa Afrika wawe Wanachama wa APRM na APRM iwe huru katika kutekeleza majukumu yake.

Agenda nyingine kuu iliyojadiliwa na kutolewa maamuzi ni mapendekezo ya makadirio mapya ya viwango vya kuchangia Umoja wa Afrika na mapendekezo ya adhabu kwa Nchi ambazo zitachelewa kulipa michango yake. Mkutano uliazimia kuitishwa kwa Mkutano kati ya Kamati ya Kudumu ya Mabalozi, Wataalam wa masuala ya Fedha kutoka nchi wanachama na Kamati ya Mawaziri wa Fedha kupitia makabrasha yote yanayohusu Viwango vya kuchangia na adhabu kwa nchi ambazo hazitoa michango yao kwa wakati. Mkutano huo, unatarajiwa kufanyika tarehe 28-29 Novemba, 2018, Addis Ababa, Ethiopia na mapendekezo ya wataalam yatawasilishwa kwenye Kikao kijacho cha Baraza la Mawaziri mwezi Februari 2019.

Mkutano pia ulipokea mapendekeo ya mgawanyiko wa majukumu kati ya AU, Jumuiya za Kikanda na Nchi Wanachama. Mgawanyo wa majukumu unapendekezwa kuwezesha Jumuiya za Kikanda, Umoja wa Afrika na Nchi Wanachama kila moja kutekeleza majukumu yake na yale ambayo watachangia kwa pamoja.

Pembezoni mwa Mkutano huho wa Dharura Wakuu wa Nchi na Serikali walizindua Mfuko wa Amani wa Umoja wa Afrika (AU Peace Fund) ambao utashughulikia masuala yote ya Amani na Usalama katika Nchi Wanachama  ikiwemo viashiria vya uvunjifu wa Amani ili kuzuia kuibuka kwa migogoro. Mhe. Waziri alishiriki katika uzinduzi huo.
                                                      -Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma, 19 Novemba 2018
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia. Nyuma yake ni Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Bi. Naimi Aziz.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Rais Mpya wa Ethiopia, Mhe. Sahle Work Zewdu katika Ikulu ya nchi hiyo tarehe 18 Novemba 2018. Dkt. Mahiga alikwenda kumpongeza Mhe. Rais kwa kuteuliwa na wote wawili walisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Ethiopia.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga. (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, Mhe. Dkt Workneh Gebeyehu alipokwenda kumtembelea kwa ajili ya kufahamiana jijini Addis Ababa. 



Rais Mkapa awasili Uganda kuwasilisha ripoti ya Usuluhishi ya mgogoro wa Burundi kwa Rais Museveni

Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz Mlima (kushoto) akimsikiliza Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ni  msuluhishi wa mgogoro wa Burundi. Rais Mkapa aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Entebbe asubuhi ya tarehe 19 Novemba 2018 kwa ajili ya kuwasilisha ripoti ya mkutano wa upatanishi uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha kwa Mpatanishi Mkuu wa mgogoro huo Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ni msuluhishi wa mgogoro wa Burundi akiwa katika chumba cha wageni maalum katika uwanja wa Ndege wa Entebbe leo. kulia ni Mwambata Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda, Brig Gen. Mkumbo, kushoto ni Msaidizi wa Rais Mkapa katika utatuzi wa mgogoro huo, Balozi David Kapya na anayemfuatia ni Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz Mlima.  


Mhe. Mkapa akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mlima, Balozi Kapya na Bw. Makocha Tembele ambaye ni Katibu wa Rais Mkapa.

Sunday, November 18, 2018

Dkt. Ndumbaro azungumzia ziara ya Kampuni kubwa kutoka Uturuki zenye nia ya kuwekeza nchini


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo) pichani kuhusu ziara ya ujumbe wa Makampuni 7 makubwa ya uwekezaji kutoka Uturuki itakayofanyika nchini kuanzia tarehe 18 hadi 24 Novemba, 2018. Ujumbe huo utatembelea mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Simiyu kwa ajili ya kuangalia fursa za uwekezaji katika ujenzi wa viwanda vya nguo, kiwanda cha kuongeza thamani bidhaa za kilimo, ujenzi wa maduka makubwa na hoteli za kimataifa. Mkutano huo na waandishi wa habari ulifanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 18 Novemba, 2018.
Sehemu ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakinukuu taarifa kutoka kwa Mhe. Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani)


Sehemu nyingine ya wanahabari wakiwajibika
Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa kuhusu ziara ya ujumbe wa Makampuni ya uwekezaji kutoka Uturuki iliyokuwa ikitolewa na Mhe. Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani)


Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Ali Davutoglu (kushoto) akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Jestas Nyamanga (katikati) pamoja na Afisa kutoka Ubalozi wa Uturuki wakifuatilia mkutano kati ya Dkt. Ndumbaro na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)
Mkutano ukiendelea
Mwandishi kutoka Gazeti la Nipashe, Bw. Gwamaka akimuuliza swali Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani)
Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Davutoglu nae akizungumza wakati wa mkutano huo kuhusu ziara ya ujumbe kutoka Uturuki huku Mhe. Dkt. Ndumbaro akisikiliza
Sehemu ya Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na JNICC wakimsikiliza Balozi Davutoglu (hayupo pichani)
Awali Bw. Hassani Mwamweta, Afisa Mambo ya Nje akieleza utaratibu kuhusu mkutano kati ya Mhe. Dkt. Ndumbaro na waandishi wa habari kabla ya mkutano huo kuanza.
Mhe. Naibu Waziri Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Balozi Davutoglu na wajumbe wengine akiwemo Bw. Nyamanga wakimsikiliza Bw. Mwamweta (hayupo pichani) akitoa utaratibu wa mkitano kabla ya mkutano kuanza
Kabla ya kushiriki mkutano na waandishi wa habari Mhe. Dkt. Ndumbaro alikutana na Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Davutoglu 


Mhe. Dkt. Ndumbaro akizungumza na Mhe. Balozi Davutoglu
  
Mhe. Dkt. Ndumbaro akimweleza jambo Mhe. Balozi Davutoglu  huku mara baada ya kumaliza mkutano kati yake na waandishi wa Habari.  Pembeni ni Bw. Nyamanga, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika
Mhe. Dkt. Ndumbaro akiagana na Mhe. Balozi Davutoglu

Mhe. Balozi Davutoglu akibadilishana mawazo na Bw. Nyamanga, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika pamoja na Bw. Mwamweta mara baada ya mkutano kati ya Dkt. Ndumbaro na waandishi wa habari kumalizika

======================================================

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUHUSU ZIARA YA UJUMBE WA MAKAMPUNI MAKUBWA YA UWEKEZAJI KUTOKA UTURUKI HAPA NCHINI

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameipongeza Serikali ya Uturuki kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano na Serikali ya Tanzania hususan katika kukuza biashara, uwekezaji na utalii.

Mhe. Dkt. Ndumbaro ametoa pongezi hizo wakati wa mkutano  na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam tarehe 18 Novemba 2018 kuhusu ziara ya ujumbe wa Makampuni 7 makubwa ya uwekezaji kutoka Uturuki.

Mhe. Dkt. Ndumbaro alisema kuwa, ziara ya ujumbe huo nchini ambayo itafanyika kuanzia tarehe 18 hadi 24 Novemba 2018 ni  mwendelezo wa jitihada za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Uturuki na wadau mbalimbali katika kutekeleza diplomasia ya uchumi ambayo pamoja na mambo mengine inalenga kwenye kutafuta na kuleta wawekezaji wenye nia ili wawekeze katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kukuza uchumi na kuinua kipato cha wananchi.

Akielezea ziara hiyo, Dkt. Ndumbaro alieleza kuwa, ujumbe wa wawekezaji kutoka Makampuni hayo ya Uturuki hapa nchini utatembelea mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Simiyu. Alisisitiza kwamba ujumbe huo umechagua mikoa hiyo kwa malengo  mahsusi ya kuwekeza katika sekta ya viwanda ikiwemo Kiwanda cha nguo, kiwanda cha sukari, kiwanda cha saruji, kiwanda cha vifaa vya ujenzi, kiwanda cha kuongeza thamani bidhaa na uwekezaji kwenye sekta ya nishati kwa mkoa wa Simiyu.

Aidha, kwa mkoa wa Dodoma ujumbe huo una nia ya kuwekeza katika ujenzi wa maduka makubwa (shopping malls), ujenzi wa majengo mbalimbali (real estate) na ujenzi wa hoteli zenye hadhi ya kimataifa.

“Tunaishukuru kwa dhati kabisa Uturuki kwani imekuwa nchi ya kwanza kutekeleza azma ya Serikali ya kuhamia Dodoma kwa kuonesha nia thabiti ya kuwekeza kwenye sekta mbalimbali mkoani humo ikiwemo maduka makubwa ya biashara (shopping malls) na hoteli za kimaifa zenye hadhi ya nyota tano” alisema Dkt. Ndumbaro.

Mhe. Dkt. Ndumbaro aliongeza kusema kuwa, ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na jitihada zinazofanywa na Serikali ikiwemo kusainiwa kwa mikataba mbalimbali ya ushirikiano, kuboreshwa kwa mazingira ya uwekezaji na biashara hapa nchini na ufunguzi wa Balozi. Alieleza kuwa, kutokana na jitihada hizo Kampuni nyingi za Uturuki zimeonesha nia na shauku ya kuwekeza na kufanya biashara hapa nchini.

“Takwimu zinaonesha kwamba kutoka mwaka 1990 hadi mwezi Septemba mwaka 2018 jumla ya Kampuni 48 za Uturuki zimewekeza Tanzania. Uwekezaji huo unathamani ya Dola za Kimarekani milioni 324.46 na umezalisha ajira 3,455 kwa Watanzania katika maeneo mbalimbali” alisema Dkt. Ndumbaro.

Akizungumzia biashara kati ya Tanzania na Uturuki, Mhe. Dkt. Ndumbaro alieleza kuwa imeimarika kwa kiasi kikubwa katika miaka ya hivi karibuni ikilinganishwa na miaka kadhaa iliyopita.

Mhe. Dkt. Ndumbaro alieleza kuwa awali Tanzania ilikuwa ikiingiza zaidi bidhaa kutoka Uturuki kama zana za kilimo, bidhaa za ujenzi, nguo na bidhaa mbalimbali za plastiki. Hata hivyo, mwaka 2017 kumekuwa na mabadiliko makubwa kwa Tanzania kuuza zaidi bidhaa zake Uturuki kama pamba, mbegu za mafuta, korosho na tumbaku kuliko Uturuki ilivyouza bidhaa zake Tanzania.

“Kwa mfano wakati bidhaa zilizouzwa Tanzania kutoka Uturuki zikiwa na thamani ya shilingi bilioni 6.091 tu, Tanzania iliuza bidhaa Uturuki zenye thamani ya Shilingi bilioni 154.749. Mabadiliko haya chanya yamechochewa na sababu mbalimbali ikiwemo juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki na Sekta Binafsi ya Tanzania kuchangamkia fursa mbalimbali za masoko zinazojitokeza Uturuki” aliongeza Dkt. Ndumbaro.

Mhe. Naibu Waziri alisema kuwa ujumbe wa Makampuni hayo makubwa kutoka Uturuki ni fursa muhimu kwa Tanzania hususan kwenye mikoa ambayo yameonesha nia ya kuwekeza. Aliongeza kuwa uwekezaji utakaofanywa na Makampuni hayo utatoa fursa kubwa kwa Watanzania ambapo inakadiriwa takribani ajira 1,400 zitatolewa na Makampuni hayo.

Kabla ya kuelekea Dodoma na Simiyu kwa ajili ya kuendelea na ziara, wawekezaji hao, watafanya mkutano na wadau muhimu wa masuala ya uwekezaji  jijini Dar es Salaam ambao  ni; Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji Tanzania (EPZA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Mkutano kati ya Dkt. Ndumbaro na Waandishi wa Habari ulihudhuriwa pia na Balozi wa Uturuki hapa nchini, Mhe. Ali Davutoglu ambaye nae alisisitiza nchi yake kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo uwekezaji, utalii na biashara ili kuzililetea maendeleo nchi hizi mbili.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam.
18 Novemba 2018


Tuesday, November 13, 2018

Dkt. Ndumbaro Ajibu Maswali Bungeni

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akijibu maswali Bungeni kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb).

 Dkt. Ndumbaro alianza kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kumuamini na  kumteua kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Dkt. Ndumbaro akijibu swali kuhusu sababu zinazofanya hadi sasa Tanzania kutoridhia Mkataba wa Afrika kuhusu Demokrasia, Chaguzi na Utawala Bora uliopitishwa mwaka 2017.

 Mhe. Naibu Waziri alieleza kuwa Tanzania inachelewa kuridhia kutokana na baadhi ya ibara za mkataba huo kukinzana na Katiba na Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Salma Kikwete akiuliza swali la nyongeza kwa Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani). 
Dkt. Ndumbaro akiendelea kujibu maswali mbalmbali ya nyongeza yaliyokuwa yakiulizwa na Waheshimiwa Wabunge.
Mkutano wa Bunge ukiendelea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga akimpongeza Naibu Waziri, Mhe. Damas Ndumbaro mara baada ya kumaliza kujibu Maswali Bungeni.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi akimpongeza Dkt. Ndumbaro mara baada ya kumaliza kujibu maswali.


 





















Job Announcement at the Commonwealth Secretariat

PRESS RELEASE

Job Announcement at the Commonwealth Secretariat

The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation call upon qualified Tanzanians to apply for the posts of Adviser-Commonwealth Blue Charter (Ocean Governance) and Outreach Coordinator- Blue Charter available at the Commonwealth Secretariat.

Job descriptions, terms and conditions of services applicable to the stated posts are available through: http://thecommonwealth.org/jobs

The deadline for application is 21st November 2018.

Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Dar es Salaam, 12 November 2018.




Tanzania kupokea Watalii 10,000 kutoka Shanghai mwaka 2019


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tanzania kupokea Watalii 10,000 kutoka Shanghai mwaka 2019

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imesaini makubaliano na kampuni ya Touchroad International Group ya China kwa ajili ya kusafirisha watalii 10,000 kutoka jiji la Shanghai kutembelea Tanzania mwaka 2019 kwa kutumia ndege Maalum (chartered flights).

Makubaliano hayo yalisainiwa sambamba na mikutano ya kutangaza utalii katika soko la China- Tourism Roadshow katika miji mitano ya China iliyoanza katika jiji la Shanghai tarehe 12 Novemba 2018.

Mikutano hiyo ni matokeo ya jitihada za Ubalozi wa Tanzania nchini China kwa kushirikiana na TTB ambapo katika mkutano wa kwanza uliofunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki, washiriki mbalimbali zaidi ya 200 walijitokeza wakiwemo makampuni ya utalii (tour operators), mawakala wa usafirishaji (travel agents), mashirika ya ndege (airlines), na vyombo vya habari.

 Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii, Bi. Devotha Mdachi alitoa mada maalum kuhusu vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania pamoja na fursa za uwekezaji katika sekta ya utalii.

Aidha, makampuni ya utalii kutoka Tanzania yalipata fursa ya kuelezea packages zao za utalii mahsusi kwa soko la China. 

Kadhalika, Shirika la Ndege la Tanzania lilitumia fursa hiyo kutangaza juu ya mpango wake wa kuanza safari za moja kwa moja kutoka Tanzania hadi China katika mji wa Guangzhou mwezi Februari 2019.

Mikutano ya kutangaza utalii itaendelea kufanyika katika miji mingine ikiwa ni pamoja na Guangzhou tarehe 14 Novemba 2018, Hong Kong tarehe 16 Novemba 2018, Chengdu tarehe 19 Novemba 2018 na Beijing tarehe 20 Novemba 2018.

                                                        -Mwisho-

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma, 13 Novemba 2018
Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki akitoa neno la ukaribisho katika mkutano wa kutangaza vivutio vya utalii uliofanyika Shaghai, China tarehe 12 Novemba 2018.


Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bi. Devotha Mdachi, Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo na viongozi wa kampuni ya Touchroad International Group wakiwa katika furaha baada ya kukamilika uwekaji saini wa makubaliano ambapo kampuni hiyo italeta watalii 10,000 nchini Tanzania mwaka 2019.

Wajumbe wameshika shuka la kimasai ambalo linaonesha utamaduni wa kabila hilo maarufu kutoka Tanzania.

Baadhi ya Washiriki wakiwemo viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, TTB na Balozi wa Tanzania nchini China wakiwa katika mkutano huo.

Monday, November 12, 2018

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU FURSA ZA MASOMO NCHINI PAKISTAN

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

FURSA ZA UFADHILI WA MAFUNZO KWA WATANZANIA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea fursa za ufadhili wa masomo ya muda mrefu kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Pakistan.

Mafunzo hayo ambayo ni kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili yatafanyika nchini Pakistan kwa kipindi cha mwaka 2018/2019.

Maelezo zaidi kuhusu mafunzo haya yanapatikana kupitia http://www.hee.gov.pk/english/scholarshipsgrants/ARL-FS

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 15 Novemba, 2018.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma
12 Novemba, 2018


Fly Your Ideas Students Competition


PRESS RELEASE

Fly Your Ideas Students Competition

The United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization (UNESCO) in collaboration with the Airbus have prepared 6th Fly Your Ideas (FYI) Competition.

The competition needs the students across the world to develop new ideas using the latest digital technologies to create smart solutions for a safer, cleaner and better connected world aimed at contributing to an eco-efficient aviation industry of the future.

The competition is open to students who studying bachelor, masters or PHD degree in any academic discipline.

The competition will involve several rounds concluding with live final where up to 6 finalist teams will present their ideas to a jury of experts for a chance to win a share of €45,000.

The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation call upon students around the country to participate in the competition which its registration deadline is on 16th November 2018 and the final will be in May-June 2019.

For more information about the Competition, Please visit: https://www.airbus-fyi.com

For inquiries, you can contact Rovani Sigamoney, Engineering Specialist of the capacity-building in Science and Engineering Section (email: r.sigamoney@unesco.org; tel +33145682237).   


Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Dar es Salaam.
12 November  2018.