TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ziara ya Kampuni kubwa za uwekezaji kutoka Austria na India
Ujumbe
wa Makampuni 16 makubwa ya uwekezaji kutoka Austria utafanya ziara ya kikazi hapa
nchini kuanzia tarehe 28 hadi 30 Januari, 2019.
Ziara
ya ujumbe huo nchini ni mwendelezo wa jitihada za Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani
ambao unawakilisha pia nchini Austria na wadau mbalimbali katika kutekeleza
diplomasia ya uchumi. Pamoja na mambo
mengine, diplomasia ya uchumi inalenga kwenye kutafuta na kuleta wawekezaji
wenye nia ili wawekeze katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kukuza
uchumi na kuinua kipato cha wananchi.
Makampuni
hayo ya Austria yana nia ya kuangalia fursa za uwekezaji hapa nchini katika
sekta mbalimbali ikiwemo afya, mawasiliano ya simu, umeme wa kutumia maji na
usafirishaji.
Ukiwa
nchini, ujumbe wa Kampuni 8 umeomba kuonana na kufanya majadiliano na viongozi
wa Wizara mbalimbali tarehe 29 Januari, 2019 jijini Dodoma akiwemo Mhe. Japhet
Ngailonga Hasunga (Mb.), Waziri wa Kilimo; Mhe. Dkt. Medard Kalemani (Mb.),
Waziri wa Nishati; Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb.), Waziri wa Fedha na Mipango;
Mhe. Ummy Mwalimu (Mb.), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake
na Watoto na Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano.
Lengo
la ujumbe huo kukutana na Mawaziri hao ni kutaka kufahamu kuhusu kazi na miradi
mbalimbali inayosimamiwa na kutekelezwa na wizara hizo ili waone namna ya
kuwekeza katika maeneo hayo.
Aidha,
ujumbe huo utashiriki kwenye Kongamano la Biashara lililoandaliwa kwa
ushirikiano kati ya Chama cha Wafanyabiashara, Wakulima na Wenyeviwanda
Tanzania (TCCIA) na Ubalozi wa Austria. Kongamano hilo litafanyika kwenye
Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam tarehe 28 Januari 2019.
Serikali ya Tanzania na Austria zina mahusiano
ya kidiplomasia ya muda mrefu tangu uhuru ambapo Austria imeendelea kutekeleza
miradi mbalimbali kupitia mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) hapa nchini
hususan katika sekta ya kilimo, afya na kuwajengea uwezo wanawake. Ziara
ya ujumbe wa makampuni hayo ni dalili njema za kuanza kuimarika zaidi kwa
mahusiano kati ya Tanzania na Austria.
Wakati
huohuo, Ujumbe
wa wawekezaji kutoka Kampuni ya Bureau
Facility Services Pvt Ltd (CISB) ya
India utafanya ziara hapa nchini kuanzia tarehe 29 Januari hadi 05 Februari
2019. Ziara hiyo ina lengo la kukamilisha utaratibu wa kuwekeza katika maeneo
kadhaa ikiwemo ujenzi wa kiwanda cha madawa, kutafuta fursa ya kuwekeza kwenye
miundombinu kama vile barabara na madaraja na ujenzi wa nyumba na hoteli.
Wajumbe hao wanatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na Mawaziri na Viongozi
Wakuu Waandamizi wa sekta husika.
Ujumbe
huo wa watu watatu utaongozwa na Bw. Alban Rodricks kutoka CISB ambaye
alishafanya ziara hapa nchini mara kadhaa. Aidha, Ujumbe huo unatarajiwa
kukutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Hamisi Kigwangala (Mb.), Waziri wa Maliasili
na Utalii, Mhe. Ummy A. Mwalimu (Mb.), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia Wazee na Watoto na Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe (Mb.), Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Mhe. Angellah Kairuki (Mb), Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji.
Katika
ziara yao hiyo fursa mbalimbali za kiuwekezaji zinatarajia kuibuliwa pamoja na
kujadiliana namna bora ya kushirikiana kati ya Tanzania na India.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
27 Januari 2019
|
Sunday, January 27, 2019
Ziara ya Kampuni kubwa za uwekezaji kutoka Austria na India
Kuwahudumia Wakimbizi ni jukumu la Wote sio la Nchi moja
Mheshimiwa Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Balozi Modest J. Mero (kushoto) na viongozi wengine wa Baraza la Wakimbizi Duniani. |
Saturday, January 26, 2019
Dkt. Mahiga amwakilisha Rais katika Jukwaa la Uchumi Duniani
Mhe. Waziri Mahiga akifanya mazungumzo na Bi. Rachel Samren, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Millicom (Millicom International Cellular S.A) tarehe 25 Januari 2019 Davos, Uswisi. |
Mawaziri wa Tanzania na Uganda wajadili Ujenzi wa Bomba la Mafuta
Ujumbe wa Tanzania uliokwenda nchini Uganda kwa ajili ya ya mkutano wa majadiliano ya ujenzi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghfi kutoka Uganda hadi Bandari ya Tanga, ujumbe huo kutoka kulia ni Mhe. January Makamba (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira); Mhe. William Lukuvi(Mb), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. Dkt. Medard Kalemani (Mb), Waziri wa Nishati; Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb), Waziri wa Katiba na Sheria na Mhe. Dkt. Aziz Mlima, Balozi wa Tanzania nchini Uganda.
Mkutano wa Bomba la Mafuta ghafi ulifanyika Kampala Uganda
kuanzia tarehe 21 hadi 25 Januari 2019. Mkutano huo ulianza kwa ngazi za
Wataalam, Makatibu Wakuu na kuhitimishwa kwa ngazi ya Mawaziri. Mkutano ulienda
vizuri na upo katika hatua nzuri ya majadiliano ili kuanza utekelezaji. Pande
zote mbili zimekubaliana mambo mbalimbali ya msingi ambayo.yanafungua na
kuandaa njia za utekelezaji wa Mradi.
|
Mhe. Dkt. Aziz Mlima, Balozi wa Tanzania nchini Uganda (kushoto) akiwa katika kikao cha wataalamu cha kujadili utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Bandari ya Tanga. |
Mhe. January Makamba (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) akichangia jambo katika mkutano huo. |
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mkutano huo kumalizika. kushoto kwake ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya adini wa Uganda, Mhe. Irene Muloni. |
Tanzania na Bosnia na Herzegovina Kuanzisha Mahusiano ya Kidiplomasia
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Balozi Modest J. Mero (kulia) na Mwakilishi wa Kudumu wa Bosnia na Herzegovina katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Ivica Dronjic wakiweka saini Makubaliano ya kuanzisha Mahusiano ya Kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Bosnia na Herzegovina. Makubaliano hayo ambayo yatazingatia Mkataba wa Vienna wa masuala ya mahusiano ya kidiplomasia wa Mwaka 1961 uliwekwa saini New York, Marekani tarehe 25 Januari 2019.
|
Friday, January 25, 2019
Tanzania yashinda Tuzo Maonesho ya Kimataifa ya Utalii, India
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Tanzania
yashinda Tuzo Maonesho ya Kimataifa ya Utalii, India
Ubalozi wa Tanzania, New Delhi, Taasisi za Serikali
na kampuni binafsi mbalimbali za utalii nchini zimeshiriki Maonesho ya
Kimataifa ya Utalii ya Mwaka 2019 nchini India yajulikanayo kama OTM 2019
[Outbound Travel Mart-2019] kwa lengo la kutangaza na kutafuta fursa mpya za
soko la utalii nchini humo.
Maonesho hayo maarufu na makubwa kabisa katika
ukanda wa Asia-Pasifiki yalianza tarehe 23 Januari, 2019 na yamemalizika leo
tarehe 25 Januari, 2019, Maonesho haya hufanyika kila mwaka katika Jiji la
Mumbai na kushirikisha taasisi mbalimbali za utalii duniani.
Taasisi za Serikali zinazoshiriki ni Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro (NCAA) na Kituo cha Kutangaza Utalii wa Zanzibar India [Zanzibar Tourism
Promotion Centre]. Kwa upande wa kampuni binafsi ni Leopard Tours, Zara Tours,
Ngarawa Hotel and Resort, DOTCOM Safaris Ltd na Jackal Adventures.
Katika Maonesho hayo, Banda la Tanzania limeibuka
Mshindi wa Kwanza kwa upande wa Banda bora lilopambwa kwa unadhifu na kuvutia
watu wengi [The winner of Best Decoration Award].
Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Baraka Luvanda
amesema kuwa maonesho hayo ni fursa adhimu kwa nchi kutangaza vivutio vya
utalii ambapo wafanyabiashara wapatao 15,000 wanaojishughulisha na masuala ya
utalii walishiriki kutoka katika mataifa zaidi ya 50 duniani. Washiriki
wamepata fursa ya kupeana taarifa muhimu kuhusu mwelekeo na maendeleo ya
biashara ya utalii katika maeneo mbalimbali duniani, vivutio vipya pamoja na
kufanya biashara.
Akiwa katika maonesho hayo, Balozi Luvanda alieleza
kuwa maonesho yalisaidia washiriki kukutana na wadau na kuanzisha uhusiano wa
kibiashara unaotarajiwa kufungua soko la utalii nchini baada ya wadau hao
kupata maelezo ya kutosha kuhusu vivutio vilivyopo nchini na faida
zake. Kwa ujumla, India ina soko kubwa la utalii. Tunategemea idadi ya
watalii kutoka India wanaokwenda Tanzania itaongezeka mara dufu baada ya kuanza
kwa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania [Air Tanzania] moja kwa
moja kutoka Tanzania kuja India ambapo zinategemewa kuanza kabla ya mwezi wa
Juni 2019.
‘Nachukua fursa hii kwa dhati kuwapongeza sana
Maafisa wote walioshiriki katika Banda letu la Tanzania la Maonesho kwa kazi
nzuri iliyowezesha ushindi huo wa kwanza kwa upande wa Banda bora
lilopambwa kwa unadhifu na kuvutia watu wengi [The winner of Best Decoration
Award]”, alisema Balozi Luvanda.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
25 Januari 2019
|
Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya Utalii wa India, Mhe. K. J. Alphons akiwa katika banda la Tanzania. Kulia kwake ni Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akiwa na washiriki wengine katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Mwaka 2019 Jijini Mumbai, India tarehe 23 Januari, 2019 |
Picha
ya pamoja ya washiriki baada ya kupokea Tuzo ya ushindi wa kwanza kwa upande wa
Banda bora la maonesho lilipambwa kwa unadhifu na kuvutia watu wengi [The Winner of Best Decoration Award] katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Mwaka 2019 Jijini
Mumbai, India tarehe 25 Januari, 2019.
|
Wageni mbalimbali wanatembelea banda la Tanzania ili kupata maelezo kuhusu vivutio vya utalii nchini. |
Wageni
katika banda la Tanzania wakipata maelezo kuhusu fursa na vivutio vya utalii
nchini.
|
Naibu Waziri awasilisha taarifa ya Wizara ya utekelezaji wa majukumu kwa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara kwa Kipindi cha Julai hadi Desemba, 2018 mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) (hawapo pichani) kilichofanyika kwenye Ofisi za Bunge, Dodoma tarehe 25 Januari, 2019. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan M. Mwinyi. |
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), Mhe. Mussa Azan Zungu akizungumza wakati wa kikao kati ya Wajumbe wa Kamati ya NUU na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kulia ni Katibu wa Kamati |
Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama |
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Salum Mwinyi Rehani akichangia jambo wakati wa kikao kati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kushoto ni Mhe. Ruth Mollel, Mjumbe wa Kamati hiyo. |
Mjumbe wa Kamati, Mhe. Fakharia Shomar Khamis nae akichangia hoja wakati wa kikao kati ya Kamati ya NUU na Wizara |
Sehemu nyingine ya Wakurugenzi kutoka Wizarani wakifuatilia kikao |
Wakurugenzi kutoka Wizarani wakisoma nyaraka mbalimbali wakati wa kikao |
Juu na chini ni Wakurugenzi kutoka Wizarani |
Wajumbe wa Kamati ya NUU wakifuatilia kikao |
Kikao kati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki |
Mjumbe wa Kamati, Mhe. Prosper Mbena akichangia jambo wakati wa kikao |
Mjumbe wa Kamati, Mhe. Janeth Masaburi nae akichangia jambo |
Mhe. Mboni Mhita ambaye ni Mjumbe wa Kamati akitoa ushauri kwa Wizara kuhusu kuboresha masuala mbalimbali katika kutekeleza Diplomasia ya Uchumi |
Mjumbe wa Kamati ya NUU, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha nae akizungumza |
Wajumbe wa Kamati wakifuatilia kikao |
Watumishi kutoka Wizarani wakifuatilia kukao |
Thursday, January 24, 2019
Mama Shamim Khan atunukiwa tuzo ya heshima nchini India
Mbunge wa zamani na aliyekuwa Naibu Waziri kwenye Wizara mbalimbali nchini, Mama Shamim Khan akitunukiwa Tuzo ya Juu (Pravasi Bharatiya Samman Award
) na Rais wa India, Mhe. Ram Nath Kovind tarehe 23 Januari, 2019. Kushoto kwake ni Waziri Mkuu wa
Mauritius, Mhe. Pravid Kumar Jugnauth ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.Tuzo hiyo ilitolewa wakati wa Mkutano wa 15 wa Diaspora wa India uliofanyika katika mji wa Varanasi, Utter Pradesh nchini humo.
|
Rais wa India, Mhe.
Ram Nath Kovind akihutubia katika hafla ya kuhitimisha Mkutano wa 15 wa Diaspora wa India [15thPravasi Bharatiya
Divas 2019] uliofanyika tarehe 23 Januari, 2019 katika mji wa Varanasi, Uttar Pradesh nchini India
|
Picha ya pamoja |
Mama Shamim Khan katika picha ya pamoja na Afisa Ubalozi wa
Tanzania, New Delhi, Dkt. Kheri Goloka baada ya kupokea Tuzo tarehe 23 Januari,
2019.
=======================================================================
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Yah: Mama Shamim Khan atunukiwa
tuzo ya juu ya heshima na Mhe. Ram Nath Kovind, Rais wa India
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
24 Januari 2019
|
Wednesday, January 23, 2019
Balozi wa Tanzania, Ujerumani awasilisha hati za utambulisho nchini Bulgaria
Balozi
wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye anawakilisha pia nchini Bulgaria , Mhe.
Dkt. Abdallah Posi akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya
Bulgaria, Mhe. Rumen Radev. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu ya nchi hiyo hivi
karibuni.
|
Mhe.
Balozi Dkt. Posi akizungumza na Mhe. Rais Radev mara baada ya kuwasilisha hati
za utambulisho
|
Mhe.
Balozi Dkt. Posi akiagana na Mhe. Rais Radev mara baada ya kuwasilisha hati za
utambulisho
|
Mhe. Balozi Dkt. Posi akiwa mbele ya gwaride la heshima alipowasili Ikulu ya Bulgaria kwa ajili ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa nchi hiyo. |
Subscribe to:
Posts (Atom)