Mhe. Prof. Kabudi akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya AICC, Balozi mstaafu, Ladis Komba (kulia) alipokuwa akimpatia taarifa fupi kuhus bodi hiyo. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi, Balozi Brigedia Jenerali (mst.), Francis Mndolwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC, Bw. Elishilia Kaaya. |
Monday, May 13, 2019
Prof. Kabudi akutana na Bodii ya AICC
Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na China lafanyika Arusha
Wadau mbalimbali wakishiriki kongamano hilo |
Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki naye akifuatilia matukio wakati wa kongamabo la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China lililofanyika Arusha |
Mhe. Waziri Kairuki akiendelea na hotuba yake huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Adolf Mkenda na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Daqarro wakisikiliza |
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, Bw. GodfreySimbeye akizungumza |
Mdau kutoka China naye akiwasilisha mada |
Sehemu ya wawekezaji kutoka China wakifuatilia kongamano lililoandaliwa na Tanzania kwa ajili yao |
Sehemu ya wadau kutoka Tanzania nao wakifuatilia kongamano |
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na Mhe, Daqarro wakati wa kongamano hilo |
Wadau wakifuatilia kongamano |
Kongamano likiendelea |
Sunday, May 12, 2019
Waziri Mkuu awapokea watalii kutoka China
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
|
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amepokea kundi la kwanza la Watalii 336 kati ya watalii 10,000 kutoka China watakaotembelea nchini mwaka huu 2019.
Akizungumza
wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ajili ya watalii hao
ambao watafanya ziara ya kitalii kwa siku nne, Mhe. Majaliwa amesema kuwa
ziara hiyo ni fursa kubwa kwa Tanzania kutangaza vivutio vya utalii kwa raia
hao wa China na duniani kwa ujumla.
Mhe.
Waziri Mkuu ameeleza kuwa, Tanzania kwa miaka mingi imekuwa ikipokea watalii,
hata hivyo kwa miaka ya hivi karibuni kutokana na kuboreshwa kwa mbinu za
kuvutia watalii kutoka nje pamoja na kuweka msisitizo kwenye diplomasia ya
uchumi kupitia Balozi zetu nje, Tanzania imeanza kupokea watalii makundi kwa
makundi kutoka duniani kote.
Akielezea
vivutio vya utalii vilivyopo nchini, Mhe. Waziri Mkuu amesema kwamba Tanzania
ni nchi pekee yenye vivutio vya utalii vya asili kama vile hifadhi za wanyama,
fukwe za bahari, milima mirefu, vyakula na mavazi ya asili ambavyo havipatikani
kokote duniani isipokuwa Tanzania.
“Wageni
wetu mmefika kwenye nchi salama kabisa, nawaomba mwendelee kufurahia vivutio
vilivyopo. Ni matumaini yangukuwa, mtapfika Ngorongoro kwenye bonde
lililosheheni wanyama badala ya maji kama yalivyo mabonde mengi. Eneo hili ni
maarufu kama Ngorongoro Crater huwezi kulipata kokote duniani isipokuwa
Tanzania pekee," alisema Mhe. Majaliwa.
Kadhalika
Mhe. Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuuelezea Mlima Kilimanjaro kwa Watalii
hao ambao ni Mlima mrefu barani Afrika na kuwaeleza kuwa hakuna anayeweza
kuuona, kuuzunguuka wala kuupanda Mlima huo bila kuja Tanzania. “ Mkiwa hapa
kwetu mtauona mlima mrefu kuliko yote Afrika ambao unapatikana Tanzania tu,
Mlima Kilimanjaro. Ukitaka kuuzunguka mlima huu lazima uje Tanzania, ukitaka
kuuona vizuri njoo Tanzania na ukitaka kuupanda tembelea Tanzania” alisisitiza
Mhe. Waziri Mkuu.
Aidha,
Mhe. Waziri Mkuu alitumia nafasi hiyo kuwashukuru na kuwapongeza wote
waliofanikisha ziara ya watalii hao akiwemo Balozi wa Tanzania nchini China,
Mhe. Mbelwa Kairuki na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na kuwaomba Watalii hao kuwa mabalozi wazuri wa vivutio vya utalii vya Tanzania wanaporudi nchini kwao.
Awali
akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi, alisema kuwa ziara ya watalii hao
imedhihirisha namna Wizara kupitia Balozi zake na kwa kushirikiana na wadau
wengine inavyotekeleza Diplomasia ya Uchumi ambayo imejikita katika kuvutia
watalii na wawekezaji pamoja na kukuza biashara nchini.
Vilevile
aliongeza kuwa, Serikali kwa sasa ina mpango mkubwa wa kutangaza utalii kwenye
nchi mbalimbali kupitia mpango uliopewa jina la “New Horizon, Tour Africa” na
kuwataka Watanzania kuchangamkia fursa hii ya watalii wanaoendelea kuja nchini
makundi kwa makundi ili wanufaike na uwepo wao.
Kwa
upande wake, Waziri wa Maliasilia na Utalii, Mhe. Hamis Kigwangala alieleza
kwamba, sekta ya utalii nchini imepiga hatua kubwa katika kipindi kifupi cha
Serikali ya Awamu ya Tano na kwamba ni ndoto yake kuendelea kukuza sekta hiyo
muhimu kwa uchumi wan chi. “Hii ni hatua kubwa kwenye sekta ya utalii nchini
kuona makundi ya watalii yakija nchini mfululizo. Tumeamua kuwekeza katika nchi
tano za kipaumbele cha pili kwa maana ya China kama mdau wetu namba moja,
Israel, Oman na nchi zingine za mashariki ya kati, Australia na Urusi,
alifafanua Mhe. Kigwangala.
Naye
Mwenyekiti wa Kampuni ya TouchRoad International Holding Group ya China, Bw.
Liehui He ambayo ndiye mratibu mkuu wa ziara za watalii hao, alisema kuwa amefurahishwa
na mapokezi makubwa na kwamba kampuni yake itaendelea kushirikiana na Serikali
kwenye sekta ya utalii kama walivyoahidi kwenye makubaliano waliyosaini kati
yao na TTB.
Wakiwa
nchini, Watalii hao watatembelea maeneo mbalimbali ya utalii ikiwa ni pamoja na
Hifadhi ya Wanyama ya Manyara, Ngorongoro, Serengeti, Olduvai Gorge pamoja na
kutembelea Maboma ya wamaasai. Aidha, sehemu ya watalii hao ambao ni wawekezaji
57 kutoka kampuni 26 za China wanatarajiwa kushiriki Kongamano la Uwekezaji
litakalofanyika jijini Arusha tarehe 13 Mei 2019.
Kutokana
na jitihada za Ubalozi wa Tanzania nchini China za kutangaza utalii, Bodi ya
Utalii Tanzania (TTB) ilisaini makubaliano na Kampuni ya TouchRoad
International Holding Group ya China kwa ajili ya kusafirisha watalii 10,000
kutoka China watakaotembelea nchini kwa kutumia ndege maalum ikiwemo Ndege ya
Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL). Makubaliano hayo pia ni kwa kampuni hiyo
kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania kwenye soko la China.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Arusha
12 Mei 2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Palamagamba John Kabudi akizungumza wakati wa hafla ya kuwakaribisha nchini watalii kutoka China. |
Sehemu ya Watalii hao wakifuatilia hotuba zilizotolewa |
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akiwa kwenye hafla ya kuwakaribisha watalii kutoka China ambao ameongozana nao. |
|
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Caesar Waitara pamoja na mdau kutoka Bodi ya Utalii wakiwa kwenye hafla hiyo. |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) akisalimiana na mmoja wa watalii kutoka China. |
Mhe. Waziri Mkuu akimsikiliza Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi alipokuwa akimweleza jambo kabla ya kuwasili kwa watalii kutoka China. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mgwira. |
Friday, May 10, 2019
Waziri wa Mambo ya Nje akutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi wa Afrika kutoka Norway
Kulia ni Balozi wa Norway hapa nchini, Mhe. Elisabeth Jacobsen pamoja na maafisa kutoka ubalozi huo wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi na mgeni wake (hawapo pichani). |
Picha ya pamoja |
Prof. Palamagamba John Kabudi akiagana na Mgeni wake. |
Waziri Kabudi aongoza maadhimisho ya miaka 25 ya uhuru wa Afrika Kusini
Juu na Chini ni sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo |
Prof. Palamagamba John Kabudi akiendelea kuzungumza kwenye hafla hiyo huku Balozi wa Afrika Kusini nchini, Mhe. Thamsanga Dennis Msekelu (aliyeketi) akimsikiliza. |
Sehemu nyingine ya wageni wakimsikiliza Prof. Kabudi hayupo pichani. |
Juu na chini ni sehemu nyingine ya wageni waalikwa aliohudhuria maadhimisho hayo wakisikiliza hotuba hiyo ya Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Hayupo pichani). |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU FURSA ZA MASOMO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO KWA WATANZANIA
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea nafasi za masomo ya
muda mrefu katika fani ya Sayansi kutoka Serikali ya Misri.
Masomo
hayo ambayo ni kwa ngazi ya Shahada ya
Uzamili na Uzamivu yatatolewa kwenye Chuo Kikuu cha Alexandria kilichopo nchini
Misri chini ya udhamini wa Mpango wa Bonde la Mto Nile (Nile Basin Initiative).
Mwisho
wa kuomba nafasi hizo ni tarehe 30 Mei 2019. Kwa maelezo zaidi kuhusu kozi hizo
na namna ya kuomba, tafadhali tembelea tovuti ifuatayo: www.nbs.alexu.edu.eg
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
10 Mei 2019
Thursday, May 9, 2019
Prof. Kabudi akutana kwa mazungumzo na Balozi wa Vietnam
Mazungumzo yakiendelea |
Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Doanh wakiwa katika picha ya pamoja. |
Subscribe to:
Posts (Atom)