Monday, May 13, 2019

Prof. Kabudi akutana na Bodii ya AICC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kwa ajili ya kukutana na Bodi ya  Kituo hicho ikiwa ni mkutano wake wa kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo mwezi Machi 2019. Mkutano huo ulifanyika jijini Arusha tarehe 13 Mei 2019
Mhe. Prof. Kabudi akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya AICC, Balozi mstaafu,  Ladis Komba (kulia) alipokuwa akimpatia taarifa fupi kuhus bodi hiyo. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi, Balozi Brigedia Jenerali (mst.),  Francis Mndolwa  na Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC, Bw. Elishilia Kaaya.

Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na China lafanyika Arusha

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki akizungumza wakati wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na wawekezaji kutoka Jimbo la Zhejiang la  China lililofanyika jijini Arusha tarehe 13 Mei 2019. Katika hotuba yake Mhe. Kairuki alisisitiz akuwa Tanzania ni eneo salama zaidi kuwekeza barani Afrika kutokana na sababu za msingi kama amani, mazingira na sheria rafiki za uwekezaji pamoja na maeneo lukuki ya kuwekeza kama kilimo, madini, usindikaji, viwanda na utalii. Kongamano hilo ambalo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Serikalini na Sekta binafsi liliwahusisha sehemu ya watalii 300 waliowasili nchini kwa ziara ya kitalii ya siku nne. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Caesar Waitara kwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Jeri Muro wakifuatilia hotuba ya Mhe. Kairuki hayupo pichani


Wadau mbalimbali wakishiriki kongamano hilo


Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki naye akifuatilia matukio wakati wa kongamabo la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China lililofanyika Arusha 


Mhe. Waziri Kairuki akiendelea na hotuba yake huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Adolf Mkenda na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Daqarro wakisikiliza


Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, Bw. GodfreySimbeye akizungumza
Mdau kutoka China naye akiwasilisha mada


Sehemu ya wawekezaji kutoka China wakifuatilia kongamano lililoandaliwa na Tanzania kwa ajili yao


Sehemu ya wadau kutoka Tanzania nao wakifuatilia kongamano


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na Mhe, Daqarro wakati wa kongamano hilo


Wadau wakifuatilia kongamano


Kongamano likiendelea




Sunday, May 12, 2019

Waziri Mkuu awapokea watalii kutoka China

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI















Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amepokea kundi la kwanza la Watalii 336 kati ya watalii 10,000 kutoka China watakaotembelea nchini mwaka huu 2019.



Akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ajili ya watalii hao ambao watafanya ziara ya kitalii kwa siku nne, Mhe. Majaliwa amesema kuwa ziara hiyo ni fursa kubwa kwa Tanzania kutangaza vivutio vya utalii kwa raia hao wa China na duniani kwa ujumla.

Mhe. Waziri Mkuu ameeleza kuwa, Tanzania kwa miaka mingi imekuwa ikipokea watalii, hata hivyo kwa miaka ya hivi karibuni kutokana na kuboreshwa kwa mbinu za kuvutia watalii kutoka nje pamoja na kuweka msisitizo kwenye diplomasia ya uchumi kupitia Balozi zetu nje, Tanzania imeanza kupokea watalii makundi kwa makundi kutoka duniani kote.

Akielezea vivutio vya utalii vilivyopo nchini, Mhe. Waziri Mkuu amesema kwamba Tanzania ni nchi pekee yenye vivutio vya utalii vya asili kama vile hifadhi za wanyama, fukwe za bahari, milima mirefu, vyakula na mavazi ya asili ambavyo havipatikani kokote duniani isipokuwa Tanzania.

“Wageni wetu mmefika kwenye nchi salama kabisa, nawaomba mwendelee kufurahia vivutio vilivyopo. Ni matumaini yangukuwa, mtapfika Ngorongoro kwenye bonde lililosheheni wanyama badala ya maji kama yalivyo mabonde mengi. Eneo hili ni maarufu kama Ngorongoro Crater huwezi kulipata kokote duniani isipokuwa Tanzania pekee," alisema Mhe. Majaliwa.

Kadhalika Mhe. Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuuelezea Mlima Kilimanjaro kwa Watalii hao ambao ni Mlima mrefu barani Afrika na kuwaeleza kuwa hakuna anayeweza kuuona, kuuzunguuka wala kuupanda Mlima huo bila kuja Tanzania. “ Mkiwa hapa kwetu mtauona mlima mrefu kuliko yote Afrika ambao unapatikana Tanzania tu, Mlima Kilimanjaro. Ukitaka kuuzunguka mlima huu lazima uje Tanzania, ukitaka kuuona vizuri njoo Tanzania na ukitaka kuupanda tembelea Tanzania” alisisitiza Mhe. Waziri Mkuu.

Aidha, Mhe. Waziri Mkuu alitumia nafasi hiyo kuwashukuru na kuwapongeza wote waliofanikisha ziara ya watalii hao akiwemo Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na kuwaomba Watalii hao kuwa mabalozi wazuri wa vivutio vya utalii vya Tanzania wanaporudi nchini kwao.

Awali akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi, alisema kuwa ziara ya watalii hao imedhihirisha namna Wizara kupitia Balozi zake na kwa kushirikiana na wadau wengine inavyotekeleza Diplomasia ya Uchumi ambayo imejikita katika kuvutia watalii na wawekezaji pamoja na kukuza biashara nchini.

Vilevile aliongeza kuwa, Serikali kwa sasa ina mpango mkubwa wa kutangaza utalii kwenye nchi mbalimbali kupitia mpango uliopewa jina la “New Horizon, Tour Africa” na kuwataka Watanzania kuchangamkia fursa hii ya watalii wanaoendelea kuja nchini makundi kwa makundi ili wanufaike na uwepo wao.

Kwa upande wake, Waziri wa Maliasilia na Utalii, Mhe. Hamis Kigwangala alieleza kwamba, sekta ya utalii nchini imepiga hatua kubwa katika kipindi kifupi cha Serikali ya Awamu ya Tano na kwamba ni ndoto yake kuendelea kukuza sekta hiyo muhimu kwa uchumi wan chi. “Hii ni hatua kubwa kwenye sekta ya utalii nchini kuona makundi ya watalii yakija nchini mfululizo. Tumeamua kuwekeza katika nchi tano za kipaumbele cha pili kwa maana ya China kama mdau wetu namba moja, Israel, Oman na nchi zingine za mashariki ya kati, Australia na Urusi, alifafanua Mhe. Kigwangala.

Naye Mwenyekiti wa Kampuni ya TouchRoad International Holding Group ya China, Bw. Liehui He ambayo ndiye mratibu mkuu wa ziara za watalii hao, alisema kuwa amefurahishwa na mapokezi makubwa na kwamba kampuni yake itaendelea kushirikiana na Serikali kwenye sekta ya utalii kama walivyoahidi kwenye makubaliano waliyosaini kati yao na TTB.

Wakiwa nchini, Watalii hao watatembelea maeneo mbalimbali ya utalii ikiwa ni pamoja na Hifadhi ya Wanyama ya Manyara, Ngorongoro, Serengeti, Olduvai Gorge pamoja na kutembelea Maboma ya wamaasai. Aidha, sehemu ya watalii hao ambao ni wawekezaji 57 kutoka kampuni 26 za China wanatarajiwa kushiriki Kongamano la Uwekezaji litakalofanyika jijini Arusha tarehe 13 Mei 2019.

Kutokana na jitihada za Ubalozi wa Tanzania nchini China za kutangaza utalii, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ilisaini makubaliano na Kampuni ya TouchRoad International Holding Group ya China kwa ajili ya kusafirisha watalii 10,000 kutoka China watakaotembelea nchini kwa kutumia ndege maalum ikiwemo Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL). Makubaliano hayo pia ni kwa kampuni hiyo kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania kwenye soko la China.

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Arusha
12 Mei 2019

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akizungumza kwenye hafla maalum ya kuwapokea watalii 336 kati ya watalii 10,000 watakaotembelea nchini mwaka huu wa 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na Mawaziri na Viongozi mbalimbali kutoka Serikalini na Sekta binafsi.Watalii hao watafanya ziara kwenye vivutio mbalimbali vya utalii kwa muda wa siku nne kuanzia tarehe 13 hadi 16 Mei, 2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Palamagamba John Kabudi akizungumza wakati wa hafla ya kuwakaribisha nchini watalii kutoka China.
Sehemu ya Watalii hao wakifuatilia hotuba zilizotolewa
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akiwa kwenye hafla ya kuwakaribisha watalii kutoka China ambao ameongozana nao.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Caesar Waitara pamoja na mdau kutoka Bodi ya Utalii wakiwa kwenye hafla hiyo. 






Mhe. Waziri Mkuu akisalimiana na Mkuu wa Msafara wa watalii kutoka China mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro katikati ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Touch Road na mratibu wa ziara ya watalii hao.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) akisalimiana na mmoja wa watalii kutoka China.
Mhe. Waziri Mkuu akimsikiliza Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi alipokuwa akimweleza jambo kabla ya kuwasili kwa watalii kutoka China. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mgwira.

Friday, May 10, 2019

Waziri wa Mambo ya Nje akutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi wa Afrika kutoka Norway

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Kusini mwa Afrika kwenye Wizara ya Mambo ya Nje  ya Norway, Bw. Germund Saether. Katika mazungumzo hayo, walijadili umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Norway hususan katika sekta za kukuza uchumi kwa maendeleo ya mataifa haya mawili.  Mazungumzo hayo yamefanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam tarehe 10 Mei 2019
 Kulia ni Balozi wa Norway hapa nchini,  Mhe. Elisabeth Jacobsen pamoja na maafisa kutoka ubalozi huo wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi na mgeni wake (hawapo pichani). 
Mazunguzmzo kati ya Mhe. Prof. Kabudi na Bw. Saether yakiendelea huku wajumbe wengine wakifuatilia. Pembeni kwa Mhe. Prof. Kabudi ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Jestas Nyamanga  pamoja na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo 
Picha ya pamoja
Prof. Palamagamba John Kabudi akiagana na Mgeni wake.




Waziri Kabudi aongoza maadhimisho ya miaka 25 ya uhuru wa Afrika Kusini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.)akihutubia kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 25 ya Uhuru wa Taifa la Afrika Kusini iliyofanyika kwenye Hoteli ya Coral Beach jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2019. 
Juu na Chini ni sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo

Prof. Palamagamba John Kabudi akiendelea kuzungumza kwenye hafla hiyo huku Balozi wa Afrika Kusini nchini, Mhe. Thamsanga Dennis Msekelu (aliyeketi) akimsikiliza.
Sehemu nyingine ya wageni wakimsikiliza Prof. Kabudi hayupo pichani.
Juu na chini ni sehemu nyingine ya wageni waalikwa aliohudhuria maadhimisho hayo wakisikiliza hotuba hiyo ya Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Hayupo pichani).
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (wa pili kutoka kushoto) pamoja na Balozi wa Afrika Kusini nchini, Mhe. Thamsanga Dennis Msekelu pamoja na Balozi wa Algeria Mhe. Saad Belabed wakikata keki iliyoandaliwa kwenye hafla hiyo.







TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU FURSA ZA MASOMO



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO KWA WATANZANIA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea nafasi za masomo ya muda mrefu katika fani ya Sayansi kutoka Serikali ya Misri.

Masomo hayo ambayo ni  kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili na Uzamivu yatatolewa kwenye Chuo Kikuu cha Alexandria kilichopo nchini Misri chini ya udhamini wa Mpango wa Bonde la Mto Nile (Nile Basin Initiative).

Mwisho wa kuomba nafasi hizo ni tarehe 30 Mei 2019. Kwa maelezo zaidi kuhusu kozi hizo na namna ya kuomba, tafadhali tembelea tovuti ifuatayo: www.nbs.alexu.edu.eg
  

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
10 Mei 2019


Thursday, May 9, 2019

Prof. Kabudi akutana kwa mazungumzo na Balozi wa Vietnam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Vietnam hapa nchini Mhe. Nguyen Doanh (kushoto), mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Kitengo cha mawasiliano serikalini wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Emmanuel Buhohela (katikati), wa kwanza kulia ni Katibu wa Waziri Bw. Magabilo Murobi na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Luangisha. E.F.L wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi na  Balozi Doanh (hawapo pichani)
Mazungumzo yakiendelea
Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Doanh wakiwa katika picha ya pamoja.




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika hapa nchini mwezi August 2019,ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anatarajia kupokea nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya hiyo na kutoa rai kwa Makampuni,taasisi za serikali na binafsi na wajasiriamali mbalimbali kuchangamkia fursa zitakazojitokeza wakati wa mkutano huo wa SADC.Mkutano huo wa waandishi wa habari umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakinukuu mazungumzo ya Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi kuhusu Mkutano wa 39 wa SADC utakaofanyika hapa Nchini mwezi August 2019 (hayupo pichani).
Sehemu ya wajumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na taasisi mbalimbali wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi na Waandishi wa Habari Kuhusu mkutano wa SADC utakaofanyika hapa Nchini mwezi August 2019.(hawapo pichani.)
Wapiga Picha wa Vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi na waandishi wa Habari kuhusu mkutano wa 39 wa SADC kufanyika hapa Nchini mwezi August 2019.