Meli ya mizigo ya MV Umoja iliyobeba mabehewa ya
treni yenye shehena ya mzigo wa Shirika la Programu ya Chakula Duniani (World
Food Program-WFP) kutoka Mwanza kwenda Uganda iliwasili bandari ya Portbell, Uganda
tarehe 31 Julai 2019.
Katika Halfa ya mapokezi ya meli hiyo, Serikali ya
Uganda iliwakilishwa na Waziri wa Nchi-Uchukuzi, Mhe. General Katumba Wamala na
kwa Upande wa Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Dkt. Aziz Mlima alimwakilisha
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Eng. Isack Aloyce Kamwelwe.
Njia hii ya usafiri wa reli kutoka Dar Es Salaam
hadi Port Bell (Kampala) Uganda, inapunguza gharama kwa asilimia zaidi ya 50 na
pia inachukuwa siku 5 tu kwa mzigo kusafiri kutoka bandari ya Dar Es Salaam
hadi Kampala.
Kwa mwaka jana WFP walisafirisha tani 40,000 na kwa
kutumia njia hii wameokoa zaidi ya Dola za Marekani milioni 2.
Ujumbe uliosafiri na meli ya MV Umoja iliyobeba mabehewa hayo yenye
mizigo ya WFP ulijumuisha Mkurugenzi Mtendaji wa TRC, Bw. Masanja Kadogosa; Mkurugenzi
wa Uchukuzi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Johnson
Kisaka ambao waliambatana na Mkurugenzi wa WFP-Tanzania, Bw. Michael
|
Meli ya MV. Umoja iliyobeba shehena ya mzigo, mali ya WFP kutoka Dar Es Salaam ikiwasili katika Bandari ya Port Bell jijini Kampala tarehe 31 Julai 2019. |
|
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz Mlima akitoa neno wakati wa hafla ya mapokezi ya meli ya Mv. Umoja jijini Kampala, Uganda. |
|
Balozi Mlima akiongea na wanahabari kuhusu zoezi hilo. |