Na
Mwandishi wetu,
Kampuni
ya Alrifai inayojihusisha na biashara ya mazao mchanganyiko iko nchini kwa
lengo la kuangalia fursa za uwekezaji hususani kununua zao la korosho na kahawa
na kuangalia uwezekano wa kujenga kiwanda cha kuchakata zao la korosho nchini.
Ujumbe
wa watu watatu (3) ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo ya Alrifai,
Bwn. Abdellah Foaud, Meneja Viwango Bwn. Ahmed Mohamed Bahie pamoja na Meneja
wa Manunuzi Bwn. M. K Hussin uko nchini tangu tarehe 13 Januari, 2020 kwa lengo
kuu la kuangalia uwezekano wa Kununua korosho zilizokwisha chakatwa pamoja na
kahawa zilizokobolewa na pia kuona maeneo ambayo wanaweza kuwekeza katika
kiwanda cha kuchakata korosho.
Ujumbe
huo ulifanya kikako na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bodi ya Kahawa
(TCB), Mamlaka ya Maendeieo ya Biashara Tanzania (TanTrade) pamoja na Bodi ya Mazao
Mchanganyiko na kuweza kupata fursa ya kufahamu kwa undani juu ya taratibu za
ununuzi wa mazao hayo pamoja na taratibu za uwekezaji wa kiwanda cha kuchakata
korosho hapa nchini.
Akitoa
maelezo juu ya uzalishwaji wa zao la Korosho nchini, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma
za Biashara wa TanTrade, Bi. Twilumba Mlelwa alisema kuwa korosho ghafi kwa
mwaka huzalishwa kati ya tani 250,000 na tani 300,000 ambapo kiasi kikubwa
huzalishwa Mtwara, Lindi, Ruvuma (Tunduru), Pwani (Mkuranga na Kibaha) pamoja
na Tanga.
"Naomba
niwatoe shaka juu ya zao la korosho kwani kwa sasa viwanda vya korosho ni 18
ambapo vinauwezo wa huhifadhi tani 63,000 za korosho lakini kwa sasa
vinavyofanya kazi ni 13 na vina uwezo wa kubangua tani 43,000" Amesema Bi.
Mlelwa
Kwa
upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo ya Alrifai, Bwn. Abdellah
Foaud,ameushukuru Ubalozi wa Tanzania nchini Kuwait kwa ushirikiano alioupata
kutoka ubalozini hadi kwa viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje kwa kuweza
kuratibu zoezi la kukuagua zao la Korosho, kahawa pamoja na karafuu.
"Binafsi
nashukuru kwa ushirikiano nilioupata kwa viongozi wa Mkoa wa Lindi na Mtwara, Bodi
ya Mazao Mchanganyiko, TIC, TanTrade, Bodi ya Kahawa pamoja na Balozi Mhandisi
Aisha Amour kwa namna alivyolisimamia jambo hili tangu likiwa wazo mpaka sasa
tunapoelekea kwenye utekelezaji niwaahidi tu kuwa utekelezaji wa kununua mazao
haya utaanza mara moja mara tu baada ya kufanya maamuzi na mikataba itasainiwa kwa
mujibu wa sheria," amesema Bwn. Foaud
Aidha,
mbali na maelezo ya uzalishaji wa zao la Korosho nchini, ujumbe huo pia ulipata
fursa ya kuona zao la korosho lililohifadhiwa katika ghala la Serikali eneo la
Kurasini jijini Dar es Salaam na uliridhishwa na zao hilo na kuahidi kuwekeza
nchini kwani korosho zinzazalishwa ni nzuri na bora.
Meneja
Viwango Bwn. Ahmed Mohamed Bahie amesema "tumejionea wenyewe ubora wa
korosho, kahawa na karafuu kwa kweli ni nzuri sana na sote tumeridhika na ubora
huo. Tutajitahidi kukamilisha taratibu zote muhimu na kuanza mara moja uagizaji
wa korosho na baadae kujenga kiwanda cha kuchakata korosho hapa Tanzania,".
Ujumbe
huo ulipata fursa ya kutembelea maeneo kadhaa kwa lengo la kupata maelezo
kuhusu taratibu na fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini, maeneo hayo ni pamoja
na mikoa ya Lindi, Mtwara na Kilimanjaro pamoja na Zanzibar ambapo waliweza
kuona uzalishaji wa Karafuu.
Ujio
wa kampuni hiyo ni matokeo ya juhudi za Ubalozi wa Tanzania nchini Kuwait ambapo
ulifanya mazungumzo na Kampuni ya Alrifai inayojihusisha na biashara ya mazao
mchanganyiko kuhusu nia yao ya kununua zao la korosho na kahawa na kuangalia
uwezekano wa kujenga kiwanda cha kuchakata zao la korosho nchini Tanzania.
Kaimu
Mkurugenzi wa Bodi ya kahawa nchini(TCB),Primus Kimaryo akiwaelezea jambo viongozi
wa Kampuni Alrifai juu ya upatikanaji wa zao la kahawa nchini
|
Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Mazao Mchanganyiko, Dkt. Anselm Moshi akimuonyesha Afisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Alrifai, Bwn. Abdellah Foaud jinsi korosho zinavyohifadhiwa
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Alrifai, Bwn. Abdellah Foaud akiuliza kitu wakati
alipotembelea moja kati ya viwanda vya kubangua korosho Mkoani Mtwara
Ujumbe
wa Kampuni ya Alrifai ukiwa katika moja ya kiwanda cha kubangua korosho mkoani
Mtwara
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bwn.
Gelasius Byakanwa (kulia) akiwa ofisini kwake na Ujumbe wa Kampuni ya Alrifai
ambapo ujumbe huo ulitembelea pia chuo cha utafiti wa Korosho Nariendele na
baadhi ya viwanda vya kubangua korosho
Ujumbe
wa Kampuni ya Alrifai ukiwa katika moja ya duka la kuuza karafuu Mjini
Zanzibar