Monday, February 10, 2020

DKT. NDUMBARO AKUTANA, KUFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WANAOWAKILISHA KUNDI LA UFC

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa nchi tano (5) hapa nchini wanaowakilisha kundi la Uniting for Consensus (UfC) la Mageuzi ya Baraza la Usalama ya Umoja wa Mataifa.

Dkt. Ndumbaro amekutana na mabalozi hao leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam ambapo ujumbe huo umewahusisha, Balozi wa Italia nchini Mhe. Balozi Roberto Mengoni, Balozi wa Hispania nchini Mhe. Balozi Fransisca Pedros, Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O’Donnel, Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Balozi Ali Davutoglu, pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Tae-ick Cho.


Pamoja na mambo mengine, majadiliano hayo yalijikita kujadili masuala mbalimbali yanayohusu ulinzi na usalama wa Umoja wa Mataifa.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), akisalimiana na Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Balozi Ali Davutoglu wakati mabalozi wanaowakilisha kundi la Uniting for Consensus (UfC) la Mageuzi ya Baraza la Usalama ya Umoja wa Mataifa wakati walipomtembelea na kufanya nae mazungumzo leo katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), akiwaeleza jambo mabalozi wanaowakilisha kundi la Uniting for Consensus (UfC) la Mageuzi ya Baraza la Usalama ya Umoja wa Mataifa wakati walipomtembelea na kufanya nae mazungumzo leo 
Balozi wa Italia nchini Mhe. Balozi Roberto Mengoni akimueleza jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), wakati mabalozi hao walipomtembelea Naibu Waziri na kufanya nae mazungumzo

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), akiwa ktk picha ya pamoja na mabalozi wanaowakilisha kundi la Uniting for Consensus (UfC) la Mageuzi ya Baraza la Usalama ya Umoja wa Mataifa 




KATIBU MKUU MPYA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI AKABIDHIWA OFISI RASMI


Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge amekabidhiwa Ofisi rasmi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Faraji K. Mnyepe kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 06 Februari, 2020. Kabla ya uteuzi huo Balozi Kanali Ibuge alikuwa Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocol). 


Aidha, Balozi Ibuge anachukua nafasi ya Dkt. Faraji K. Mnyepe ambaye alihamishwa wizara kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Dkt. Mnyepe amechukua nafasi ya Dkt. Frolens Turuka ambaye amestaafu.

Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akipokea baadhi ya nyaraka za Ofisi kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Faraji K. Mnyepe. Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akimpa mkono aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Faraji K. Mnyepe mara baada ya makabidhiano rasmi ya Ofisi.

Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Ramadhani Mwinyi baada ya kumtembelea ofisini kwake leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas D. Ndumbaro (Mb) akiwa na Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge alipomtembelea Ofisini kwake leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam


Sunday, February 9, 2020

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI MKUTANO WA 33 WA UMOJA WA AFRIKA ADDIS ABABA,ETHIOPIA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akiwa katika Mkutano wa 33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika unaoendelea Addis Ababa,Ethiopia. Nyuma yake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na Balozi wa Tanzania Nchini Ethiopia Mhe. Naimi Aziz.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akipitia baadhi ya nyaraka wakati akishiriki katika Mkutano wa 33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika unaoendelea Addis Ababa,Ethiopia. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete walipokutana katika ukumbi wa mkutano wa Umoja wa Afrika Addis Ababa, Ethiopia.

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika ukumbi wa Mkutano wa Umoja wa Afrika Addis Ababa,Ethiopia. Anayeshuhudia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan 

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika anayemaliza muda wake Mhe. Abdel Fattah el-Sisi ambae pia ni Rais wa Misri akikabidhi Uenyekiti kwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika Mhe. Cyril Ramaphosa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiteta jambo na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni walipokutana katika jengo la Umoja wa Afrika wakati akisubiri kumpokea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan Mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Friday, February 7, 2020

MKUTANO WA 7 WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI WA MAZINGIRA NA USIMAMIZI WA MALIASILI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAFIKIA TAMATI JIJINI DODOMA

Meza Kuu ikifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea wakati wa Mkutano wa Saba (7) wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Mazingira na Usimamizi wa Maliasili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Dodoma. Mkutano huu uliofanyika kwa kipindi cha siku 5 (tarehe 3-7 Februari, 2020) umefanyika katika ngazi tatu nazo ni; ngazi ya wataalamu, ngazi ya Makatibu Wakuu na ngazi ya Mawaziri. 
Mawaziri kutoka nchi Wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakisaini taarifa kwenye Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Mazingira na Usimamizi wa Maliasili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Dodoma, Ijumaa tarehe 7 Februari, 2020
Mawaziri kutoka nchi Wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakisaini wakiwa katika picha ya pamoja mara baada kusaini taarifa ya Mkutano 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu wakijadili jambo kwenye Mkutano wa 7 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Mazingira na Usimamizi wa Maliasili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma.  
Mawaziri walioiwakilisha Tanzania wakishikishana jambo kwenye Mkutano wa 7 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Mazingira na Usimamizi wa Maliasili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma.

TANZANIA YAISHAURI ETHIOPIA KUTAFUTA KIINI CHA TATIZO LA RAIA WAKE KUONDOKA NCHINI HUMO BILA KUFUATA UTARATIBU

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Dkt Workneh Gebeyehu walipokutana kwa ajili ya mazungumzo Mjini Addis Ababa,Ethiopia Kando ya Mkutano wa 33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika. 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Dkt Workneh Gebeyehu (Katikati) akiwa na ujumbe wake katika mazungumzo baina yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (hayupo pichani).Mazungumzo hayo yamefanyika Mjini Addis Ababa,Ethiopia Kando ya Mkutano wa 33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa na ujumbe wake katika mazungumzo baina yake Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Dkt Workneh Gebeyehu (hayupo pichani) kushoto aliyevaa kilemba ni Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe Naimi Azizi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Dkt Workneh Gebeyehu. Mazungumzo hayo yamefanyika Mjini Addis Ababa,Ethiopia Kando ya Mkutano wa 33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika. 

Tanzania yaibuka mshindi wa kwanza Tuzo ya Utalii nchini India

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Maonesho ya Kimataifa ya Utalii baada ya kupokea Tuzo ya ushindi wa kwanza kwenye kipengele cha Banda Bora la Maonesho lililopambwa kwa unadhifu na kuvutia watu wengi (The Winner of Best Decoration Award) katika maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya mwaka 2020 jijini Mumbai, India tarehe 5 Februari 2020
Balozi Luvanda akiwa na wadau kwenye Banda la Tanzania
Mhe. Balozi Luvanda akiwa na wadau mbalimbali walioshiriki maonesho ya Utalii jijini Mumbai
Wageni wakiwa wamefurika kwenye Banda la Tanzania kwa ajili ya kupata maelezo kuhusu masuala ya utalii
Picha ya pamoja
========================================================


Tanzania yashinda kwa mara ya pili Tuzo ya Maonesho ya Kimataifa ya Utalii, India.
Tanzania imeibuka mshindi wa kwanza wa Banda Bora katika maonesho ya Kimataifa ya Utalii yajulikanayo kama Outbound Travel Mart 2020 (OTM 2020) yaliyofanyika nchini India hivi karibuni.
Ubalozi wa Tanzania, New Delhi, Taasisi za Serikali na kampuni binafsi mbalimbali za utalii nchini zimeshiriki Maonesho hayo kwa lengo la kutangaza na kutafuta fursa mpya za soko la utalii nchini humo.
Maonesho hayo maarufu na makubwa katika ukanda wa Asia na Pasifiki ambayo hufanyika kila mwaka jijini Mumbai na kuzishirikisha taasisi mbalimbali za utalii duniani, yamefanyika kuanzia tarehe 3 hadi 5 Februari, 2020.
Wakati wa maonesho hayo, Banda la Tanzania limeibuka tena Mshindi wa Kwanza kwa upande wa Banda bora lilopambwa kwa unadhifu na kuvutia watu wengi (The winner of Best Decoration Award). Tanzania imeshinda tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo ambapo katika maonesho ya mwaka 2019, Tanzania pia ilishinda tuzo hiyo.
Akizungumzia maonesho hayo, Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Baraka Luvanda amesema kuwa maonesho hayo ni fursa nyingine adhimu kwa nchi kutangaza vivutio vya utalii ambapo wafanyabiashara wapatao 15,000 wanaojishughulisha na masuala ya utalii walishiriki kutoka katika mataifa zaidi ya 50 duniani. Aidha alisema kuwa, Washiriki wamepata fursa ya kupeana taarifa muhimu kuhusu mwelekeo na maendeleo ya biashara ya utalii katika maeneo mbalimbali duniani, vivutio vipya pamoja na kufanya biashara.
Kadhalika, Balozi Luvanda ameeleza kuwa, maonesho yalisaidia washiriki wa Tanzania kukutana na wadau na kuanzisha uhusiano wa kibiashara unaotarajiwa kufungua soko la utalii nchini baada ya wadau hao kupata maelezo ya kutosha kuhusu vivutio vilivyopo nchini na faida zake. 

“Nachukua fursa hii kwa dhati kuwapongeza sana Maafisa wote walioshiriki katika Banda letu la Tanzania la Maonesho kwa kazi nzuri ya kutangaza vivutio vya utalii nchini iliyowezesha tupate ushindi mwingine katika maonesho haya kwa mara ya pili kwa upande wa Banda bora lilopambwa kwa unadhifu na kuvutia watu wengi (The winner of Best Decoration Award)”, alisema Balozi Luvanda.

Kwa ujumla, India ina soko kubwa la utalii. Idadi ya watalii kutoka India wanaokwenda Tanzania sasa imeongezeka mara dufu baada ya kuanza kwa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) moja kwa moja kutoka Tanzania kuja India na katika hilo alitoa wito kwa wafanyabiashara hao kuendelea kutumia fursa hiyo kuongeza idadi ya watalii wa India kutembelea Tanzania.

Taasisi za Serikali ya Tanzania zilizoshiriki ni pamoja na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania). Kampuni binafsi zilizoshiriki ni pamoja na Zara Tours, Mount Meru Hotel na Nature’s Land Safaris & Rentals.




Wednesday, February 5, 2020

BENKI YA DUNIA, SERIKALI YA TANZANIA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia hapa nchini Tanzania, Bi. Mara Marwick ameihakikishia Serikali ya Tanzania ushirikiano katika sekta mbalimbali ili kufikia maendeleo yaliyokusudiwa.


Bi. Marwick ameyasema hayo  leo tarehe 5 Februari 2020 alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi katika Ofisi Ndogo za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam.

 Bi. Marwick amesema uhususiano baina ya benki hiyo na Tanzania ni mzuri na kwamba Benki ya Dunia inathamini uhusiano huo wa tangu miaka ya 1960 hadi leo na iko tayari kuendelea kuunga mkono kwa njia ya ufadhili au mikopo miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.

"Tuna uhusiano mzuri katika miradi na uwekezaji ambapo tunaiwezesha serikali katika maeneo mbalimbali. Pia tunafanya kazi pamoja katika masuala muhimu kama vile uchambuzi wa sera za maendeleo hii inaashiria kuwa Benki ya Dunia itaendeleza ushirikiano huu katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na mahusiano imara pamoja na maendeleo endelevu," Amesema Bi. Marwick.

Ameongeza kuwa katika mazungumzo hayo, wamejadili masuala muhimu kuhusu maendeleo ya Tanzania hususani elimu, miradi ya miundombinu, uchumi wa viwanda, pamoja na maendeleo ya wananchi. 

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema Tanzania itaendeleza mahusiano na Benki ya Dunia na kuwataka watanzania kupuuza uzushi na uvumi unaosambazwa katika mitandao ya kijamii kuhusu mahusiano baina ya Tanzania na Benki hiyo na badala yake wasubiri taarifa rasmi kutoka kwa Serikali na Benki ya dunia.

"Uhusiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia ni imara na unaendelea vizuri, na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia ametuhakikishia kwamba katika kipindi hiki ambacho yeye ni mkurugenzi hapa atauendeleza uhusiano huo huo. Mengi yanasemwa lakini mengi hayana ukweli na wakati mwingine si busara kwa kila yanayosemwa kuyajibu kwasababu yanaweza kuwaondoa kwenye shughuli za msingi na mkajikuta kila siku mnajibu uvumi au uzushi katika mitandao ya kijamii na mambo mengine," Amesema Prof. Kabudi.

Prof. Kabudi ameongeza kuwa katika mazungumzo hayo pia wamegusia miradi ya kimkakati ambayo Tanzania inaitekeleza, mingine kwa fedha za ndani au kwa kupata mkopo kutoka Benki ya Dunia.

"Tumezungumza kwa kirefu kuhusu mashirikiano katika elimu hasa elimu ya wasichana na kukuza rasilimali watu na kutaja maeneo mengine ya mashirikiano ambayo ni pamoja na  sekta za miundombinu, afya, maji na nishati," Ameongeza Prof. Kabudi.

Prof. Kabudi ameongeza kuwa Tanzania inakopesheka kwenye benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Afrika Mashariki ya Maendeleo na taasisi nyingi sana za kifedha na daima Serikali huhakikisha kuwa vigezo vyote vinavyotakiwa vinasimamiwa lakini kikubwa hulipa madeni iliyokopa na ndiyo maana inaaminiwa na kukopeshwa zaidi na fedha yote inayokopwa hupelekwa kwenye miradi ya msingi ya kulifanya taifa kujitegemea lenyewe katika miaka michache ijayo.

Katika tukio jingiene, Waziri kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. Stegomena Taxi na kujalidiana nae mambo mbalimbali kuhusu SADC.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongea na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bi. Mara Marwick wakati Bi. Marwack alipomtembelea Waziri katika ofisi ndogo za Wizara leo jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bi. Mara Marwick  akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati walipokuwa na mazungumzo katika ofisi ndogo za Wizara leo jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bi. Mara Marwick  akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo za Wizara leo jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongea na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. Stegomena Taxi leo katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam





UZINDUZI WA KITABU CHA KUVUTIA WATALII ‘A TASTE OF TANZANIA”


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Uzinduzi wa Kitabu cha ‘A TASTE OF TANZANIA”

Dodoma, 5 Februari 2020
Ubalozi wa Tanzania nchini Uholanzi umeshiriki katika hafla ya uzinduzi wa kitabu kinachoitwa “A Taste of Tanzania” kilichosheheni picha zinazoonesha vivutio vya utalii pamoja na utamaduni wa Mtanzania. Uzinduzi wa Kitabu hicho chenye kurasa 343 ulifanyika wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha za utalii uliofanyika The Hague, Uholanzi tarehe 30 Januari 2020.

Maeneo ya utalii yanayooneshwa kwa kina ndani ya Kitabu hicho ni pamoja na; Mji wa kimataifa wa Arusha; Mlima Kilimanjaro; Hifadhi za Taifa za Manyara, Ngorongoro, Serengeti, Tarangire na Ruaha; Mlima Ol Donyo Lengai na Ziwa Natron. Maeneo mengine ni Olduvai Gorge; umaarufu wa Ziwa Eyasi na Bonde la Ufa; Utalii wa mkoa wa Iringa; aina mbalimbali za mapishi pamoja na viungo vyenye ladha nzuri vinavyoleta upekee katika mapishi hayo.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa sherehe ya Uzinduzi wa Kitabu na Maonyesho hayo, Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju aliwashukuru waandaji wa Kitabu hicho kwa uwasilishaji sahihi kuhusu Tanzania, hali itakayowezesha watalii kuongezeka zaidi nchini, Balozi Kasyanju alitumia fursa hiyo pia kutoa wito kwa Waholanzi na Jumuiya ya Kimataifa kuja kuwekeza Tanzania kufuatia maboresho makubwa yaliyofanyika katika miundombinu na taratibu za uwekezaji.

“A Taste of Tanzania” ni kitabu kilichoandaliwa na mwandishi Bw. Stephen Walckiers kwa kushirikiana na mpiga picha maarufu, Bw. Wim Demessemaekers, wote wakazi wa Uholanzi waliowahi pia kuishi Tanzania. Uzinduzi rasmi wa kitabu hicho kinachopatikana kwenye mitandao na maduka ya vitabu nchini unatarajiwa kufanyika nchini Tanzania tarehe 05 Februari 2020.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.

=======================================================================


Baadhi ya picha zilizotumika kuutangaza utalii wa Tanzania katika kitabu cha "A Taste of Tanzania." 


Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju akiteta jambo na mpiga picha aliyeshiriki katika maandalizi ya uandishi na uchapishaji wa kitabu hicho, Bw. Wim Demessemaekers.

Mhe. Balozi kasanju akipokea ufafanuzi wa tafsiri za picha mbalimbali kutoka kwa Bw. Wim

Balozi wa Yemen nchini Uholanzi, Mhe. Sahar Ghanem akimsalimia na kumpongeza Bw. Wim kwa umahiri wake wa kupiga picha. Mhe. Ghanem alielezea nia yake ya dhati ya kutembelea Tanzania.

Sehemu ya Wanadiplomasia, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa na wadau wengine walioshiriki kwenye sherehe ya uzinduzi wa Kitabu na ufunguzi wa maonesho ya picha za utalii wa Tanzania.

Baadhi ya vyakula vya kitanzania vilivyoandaliwa kwa ajili ya hafla ya uzinduzi wa kitabu na ufunguzi wa maonesho.

TANZANIA, JAPAN ZAAHIDI KUENDELEZA UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA NA UCHUMI

Tanzania na Japan zimeahidiana kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia pamoja na  kushirikiana katika kuhakikisha maendeleo katika sekta za biashara, uwekezaji na viwanda baina ya nchi hizo mbili. 

Akihutubia sherehe ya kumbukizi ya miaka 60 kuzaliwa Mfalme Naruhito wa Japan na Siku ya Taifa la Japan kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Mkuu wa Itifaki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge alisema kuwa Tanzania na Japan zimekuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia ambapo kutoka na uhusiano, Japan imekuwa ikisaidia ujenzi wa miradi mbalimbali kama vile ujenzi wa miradi ya maendeleo kama vile daraja la juu lililopo eneo la Tazara (Mfugale flyover) na mradi wa umeme wa Kinyerezi II.

"Kutokana na Uhusiano mzuri baina ya Tanzania na Japan serikali ya Japan imefadhili miradi mingine mbalimbali hpa nchini ikiepo ujenzi wa barabara ya Iringa - Dodoma, Dodoma - Babati, Tunduru - Namtumbo, pamoja na upanuzi wa barabara ya Bagamoyo eneo la kuanzia Morocco hadi Mwenge," Amesema Balozi Kanali Ibuge. 

Balozi Kanali Ibuge aliongeza kuwa, mbali na sekta ya ujenzi, pia Japan imefadhili miradi mbalimbali katika sekta muhimu nchini kama vile elimu, afya, maji na michezo.

"Serikali ya Japan imechangia sana sula la elimu ambapo watanzania (wanafunzi) wengi wamekuwa wakipata ufadhili wa kusomeshwa Japan mafunzo ya muda mrefu nay ale ya muda mfupi na yamechangia kwa kiasi kikubwa ufanisi wa rasilimali watu," Amesema Balozi Kabudi Ibuge

Kwa upande wake, Balozi wa Japan chini Tanzania, Mhe. Balozi Shinichi Goto amesema kuwa Japan inatambua Tanzania mara baada ya ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa umoja na mshikamano ambao imekuwa ikionesha kwa Japan na kusema kuwa umoja huo umekuwa ni chachu ya maendeleo kwa Tanzania na Serikali ya Japan.

Japan imekuwa ikifurahia uhusiano wa kirafiki na mzuri na Tanzania kwa muda mrefu sasa, ambapo pamoja na mambo mengine Mhe. Balozi, Goto ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa umoja na mshikamano ambao imekuwa ikionesha kwa Japan tangu wakati huo na kusema kuwa umoja huo umekuwa ni chachu ya maendeleo baina ya mataifa hayo mawili.

"Urafiki wa kiuchumi kati ya Tanzania na Japan kwa sasa ni imara, na ni matumaini yetu kuwa katika siku za usoni uhusiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Japan utafikia hatua mpya ya ushirikiano," Amesema Balozi Goto.


Mkuu wa Itifaki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiwasilisha hotuba kwa niaba ya Waziri wa Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati wa sherehe ya kumbukizi ya miaka 60 kuzaliwa Mfalme Naruhito wa Japan na Siku ya Taifa la Japan iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Japan chini Tanzania, Mhe. Balozi Shinichi Goto

 Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia hutuba ya mgeni rasmi wakati wa sherehe ya kumbukizi ya miaka 60 kuzaliwa Mfalme Naruhito wa Japan na Siku ya Taifa la Japan iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam 

Mkuu wa Itifaki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Japan chini Tanzania, Mhe. Balozi Shinichi Goto

Wanakwaya wa kwaya ya Dar es Salaam wakiimba wimbo wa Taifa wa Tanzania pamoja na wa Japan wakati wa sherehe ya kumbukizi ya miaka 60 kuzaliwa Mfalme Naruhito wa Japan na Siku ya Taifa la Japan iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam 



Tuesday, February 4, 2020

ZIARA YA MABALAOZI WASTAAFU WA TANZANIA JIJINI DODOMA YAFANA

Mabalozi Wastaafu wa Tanzania 34 walifanya ziara ya siku 2 jijini Dodoma tarehe 3 na 4 Februari 2020 kwa mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi.

Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kuendelea kutambua mchango mkubwa wa Mabalozi hao kwa nchi katika medani za kimataifa na masuala ya ukuzaji Diplomasia ya Uchumi kwa ujumla. Pia kuendelea kutoa uzoefu wao kwenye masuala ya Diplomasia kwa makundi mbalimbali ikiwemo Wabunge, Wanafunzi na Watumishi wa Wizara.

Wakiwa jijini Dodoma Mabalozi hao Wastaafu walipata fursa ya kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Chuo Kikuu cha Dodoma na Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahriki zilizopo Mtumba.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati alipowakaribisha Bungeni Mabalozi Wastaafu wa Tanzania (hawapo pichani) walipotembelea Bungeni tarehe 3 Februari 2020  kwa ajili ya kujionea shughuli za Bunge.
Waheshimiwa Mabalozi Wastaafu wakifuatilia vikao vya Bunge wakiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe (wa kwanza kulia)
Mhe. Spika Ndugai, Mhe. Ndumbaro  na Dkt. Mnyepe wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi Wastaafu mara baada ya kukamilisha ziara yao Bungeni hapo
Balozi Mstaafu,  Mhe. Getrude Mongella akizungumza na Wanafunzi wa  Kozi ya Mahusiano ya Kimataifa na Diplomasia (hawapo pichani)  katika Chuo Kikuu cha Dodoma wakati wa ziara ya Mabalozi Wastaafu Chuoni hapo tarehe 3 Februari 2020. Pamoja na mambo mengine Mhe. Balozi Mongella aliwaasa kuzingatia uzalendo, kusoma kwa bidii  na kujiongezea maarifa kwa kujifunza mambo mbalimbali yanayoendelea duniani. Pia aliwashirikisha falsafa yake ya kutokata tamaa na kujiamini kwani hakuna lisilowezekana.

Sehemu ya Mabozi Wastaafu na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakimsikiliza Balozi Mongella (hayupo pichani)

Picha ya pamoja kati ya Mabalozi Wastaafu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma 
Waheshimiwa Mabalozi Wastaafu wakipata maelezo kuhusu Mji wa Serikali kutoka kwa  Bw. Meshack Bandawe, Mratibu wa Ujenzi wa Mji huo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu. Mabalozi hao walipata maelezo hayo walipotembelea Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo Mtumba jijini Dodoma.

Waheshimiwa Mabalozi Wastaafu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo Mtumba jijini Dodoma