Baadhi
ya mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, wamejitokeza kusaini kitabu cha
maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa aliyeaga dunia
Tarehe 24 Julai, 2020 jijini Dar es Salaam 'wakimlila' na kumuelezea kwa mema
mengi aliyoyafanya wakati wa uhai wake.
Mabalozi
hao walianza kuwasili nyumbani kwa Mzee Mkapa kwa nyakati tofauti ambapo mara
baada ya kusaini kitabu cha maombolezo baadhi yao wakaelezea walivyoguswa na
msiba.
Balozi
wa Misri chini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa amemuelezea Mzee Mkapa kuwa
alikuwa mtu makini na aliyependa masuala ya kidiplomasia.
"Nimekuja
hapa kwa niaba ya Serikali ya Misri kuja kutoa pole kwa kuondokewa na Mzee
Mkapa kiongozi mchapakazi kwa taifa la Tanzania na alikuwa kiongozi aliyeinua
uchumi wa taifa ambapo chini ya uongozi wake Tanzania iliingia katika ubinafsishaji
na utandawazi", Amesema Balozi Abulwafa.
Ameoneza
kuwa Mzee Mkapa atakumbukwa na wanadiplomasia wengi duniani kwani alikuwa kiongozi
aliyependa amani ambapo enzi za uhai wake alisuluhisha mauaji ya kimbari katika
nchi za Rwanda na Burundi pamoja na kurejesa amani katika nci za Sudan, Kongo
DRC, Zimbabwe na Kenya.
"Tutamkumbuka
kwa upendo na uchapakazi wake uliokuwa umetukuka na kuonesha matunda ya amani
na mandeleo kwa Tanzania na Afrika Mashariki", Amesema Balozi Abulwafa.
Kwa
upande wake mwakilisi wa Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Adrian Fitzgerald
amemuelezea Rais Mstaafu Mzee Mkapa kuwa alikuwa rafiki mkubwa wa Ireland, na
ambaye aliyeendeleza na kudumisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na
Ireland ambao hadi sasa upo imara.
"Kwetu
sisi kama Serikali ya Ireland tumeguswa sana na msiba huu, kwa kuondokewa na
kiongozi mchapakazi na mpenda amani….daima tutamkumbuka kwa mema yaka na uchapaji
kazi wake ulioiletea Tanzania maendeleo. Tulimfaamu vizuri alikuwa kionozi
mpenda maendeleo na amani……kwetu sisi ni pigo kubwa sana kwa kifo chake" Amesema Fitzgerald.
Baadhi
ya mabalozi waliofika na kusaini kitabu cha maombolezo ni Balozi wa Japan
nchini Tanzania, Mhe. Shinichi Goto, Balozi wa Falme za Kiarabu nchini
Tanzania, Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi, Balozi wa Misri chini
Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa, Balozi
wa Finland chini Tanzania, Mhe. Riitta Swan, Balozi wa Oman hapa Nchini
Mhe. Ally Abdallah Almahruqi.
Balozi wa Misri chini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa nyumbani kwa Marehemu jijini Dar es Salaam |
Balozi wa Finland chini
Tanzania, Mhe. Riitta Swan akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Marehemu
Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa
Balozi wa Oman hapa Nchini Mhe. Ally Abdallah Almahruqi akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa nyumbani kwa marehemu jijini Dar es Salaam |
Mwakilisi wa Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Adrian Fitzgerald akiwaelezea waandishi wa habari jinsi alivyomfahamu Rais Mstaafu Mzee Mkapa wakati alipokuwa nyumbani kwa marehemu jijini Dar es Salaam |