Rais
wa Visiwa vya Comoro Mheshimiwa Azali Assouman ameipongeza Serikali ya Tanzania
kwa kufanya uchaguzi huru, amani na haki.
Rais
wa Visiwa vya Comoro ameipongeza Tanzania leo jijini Dar es Salaam wakati
alipokuwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa tayari kuondoka nchini na
kurejea Comoro baada ya kushuhudia hafla ya uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli uliofanyika Novemba 5 Jijini
Dodoma.
Rais
Assouman anasema Tanzania ni nchi ya Amani na utulivu wa kisiasa kwani wakati
wote wa tukio la kuapishwa kwa Dkt Magufuli aliona mambo ambayo yanapaswa
kuigwa na mataifa mengine hususan kwenye nyakati za uchaguzi.
"Kwa
kweli tangu nimefika hapa Tanzania nimeona mambo mazuri na ambayo tunapaswa
kuyaiga sisi viongozi wa mataifa mengine," Amesema Rais Assouman
Mbali
na kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo ya uchaguzi, pia Rais Assouman ameliahidi
ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania katika Nyanja za mbalimbali ikiwemo
diplomasia ya uchumi, biashara, uwekezaji na utalii.
“Najisikia
niko nyumbani kwa sababu uhusiano wetu umeimarishwa zaidi, mahusiano yetu yamekuwa
katika masuala ya kijamii, utamaduni, biashara na mambo mengine mengi”
Amebainisha Rais Assouman.
Kwa
upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Mhe. Sylvester Mabumba amesema
kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na Comoro katika kuhakikisha
kuwa sera ya uchumi wa nchi zote mbili unakua zaidi.
"Sisi
tuatendelea kushirikiana vyema na Comoro kibiashara ili kukuza sera ya 2025 tunaifikia
ipasavyo kwa kuhakikisha kuwa uchumi wetu unafikia kiwango cha juu sana,
naamini kuwa tunapokuwa na masoko ya uhakika Viswa vya Comoro uchumi wetu
utakuwa zaidi," Amesema Balozi Mabumba.
Kwa
Upande wake Balozi wa Visiwa Vya Comoro nchini Tanzania mhe. Dkt. Ahmada El
Badaoui Mohamed amesema kuwa kuna fursa nyingi za kiuchumi ambazo Comoro na
Tanzania zinaweza kushirikiana.
Rais
Assouman aliwasili nchini Novemba 4 kwa ajili ya kuhudhuria hafla ya uapisho wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli uliofanyika
Novemba 5 Jijini Dodoma ambapo baada ya shughuli hiyo alipata fursa ya kutembelea
hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ambapo na kujiona vivutio mbalimbali vya utalii
nchini.
Serikali
ya Tanzania na Visiwa Comoro zimekuwa zikishirikiana katika sekta mbalimbali
ikiwemo, elimu, afya, biashara na uwekezaji.
|
Rais wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Azali Assouman akiongea na waandishi wa habari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA),kabla ya kuondoka nchini na kurejea nchini Comoro. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Mhe.Sylivester Mabunda akifuatiwa na Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Mhe. Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed. |
|
Rais wa Visiwa vya
Comoro, Mhe. Azali Assouman akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
Julius Nyerere (JNIA), baada ya kushuhudia hafla ya Uapisho wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli iliyofanyika Novemba 5, 2020 Jijini Dodoma na Baadaye alitembelea
Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro |
|
Rais wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Azali Assouman, akiangalia kikundi
cha ngoma kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa Julius Nyerere (JNIA), baada ya kushuhudia hafla ya Uapisho wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli iliyofanyika
Novemba 5, 2020, Jijini Dodoma na Baadaye alitembelea Hifadhi ya Taifa ya
Ngorongoro |
|
Kikundi cha Ngoma kikiburudisha katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa Julius Nyerere kabla ya kuondoka kwa Rais wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Azali Assouman |
|
Rais wa Visiwa
vya Comoro, Mhe. Azali Assouman, akiagana na Balozi wa Tanzania nchini
Comoro, Mhe.Sylivester Mabunda katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius
Nyerere (JNIA), Jijini Dar es Salaam |
|
Rais wa Visiwa
vya Comoro, Mhe. Azali Assouman, akiaga tayari kwa kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa Julius Nyerere(JNIA), kwa kutumia Ndege ya Shirika la Ndege la
Tanzania (Air Tanzania) |