Na mwandishi wetu, Dar
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb) amemuaga Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Sanjiv Kohli ambaye amemaliza
muda wake wa uwakilishi nchini.
Akiongea
katika hafla ya kumuaga balozi wa India iliyofanyika leo katika Ofisi Ndogo za
Wizara Jijini Dar es Salaam, Waziri Mulamula amempongeza Balozi Kohli kwa kazi
nzuri aliyoifanya ya kudumisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya India na Tanzania.
Pamoja
na mambo mengine, Balozi Mulamula amemuahidi Balozi Kohli kuwa Tanzania
itaendelea kushirikiana na India katika sekta za elimu, afya, maji, kilimo, tehama
na utalii kwa maslahi mapana ya nchi zote mbili.
"Kwa
niaba ya Serikali ya Tanzania nakuahidi ushirikiano kutoka kwetu, nakutakia
kila la kheri katika maisha yako nje ya Tanzania na ni imani yangu kuwa utakuwa
balozi mzuri wa Tanzania duniani," Amesema Balozi Mulamula
Kwa
upande wake Balozi Kohli ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kumpa ushirikiano
wa kutosha wakati wa kipindi chake cha uwakilishi hapa nchini.
Balozi
Kohli ameelezea kufurahishwa na uhusiano mzuri uliopo baina ya India na
Tanzania na amepongeza hatua mbalimbali ambazo Serikali ya Tanzania imeendelea
kuzichukua katika kuimarisha diplomasia ya uchumi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Balozi wa India aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini, Mhe. Sanjiv Kohli katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi
wa India aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini, Mhe. Sanjiv Kohli akiongea
na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata
Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Libarata
Mulamula akimueleza jambo Balozi wa India aliyemaliza muda wake wa uwakilishi
hapa nchini, Mhe. Sanjiv Kohli
Maongezi
baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Libarata Mulamula na Balozi wa India aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa
nchini, Mhe. Sanjiv Kohli yakiendelea
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula
akimkabidhi zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro Balozi wa India anayemaliza
muda wa uwakilishi nchini, Mhe. Sanjiv Kohli