Wednesday, August 11, 2021

TANZANIA KUJIPANGA KUNUNUA DOZI MILIONI 17 ZA UVIKO - 19 ILIZOTENGEWA NA UMOJA WA AFRIKA

Umoja wa Afrika umeitengea Tanzania dozi milioni 17 za chanjo za UVIKO- 19 kupitia mpango wa Umoja huo wa kuzisaidia Nchi wanachama kupata chanjo kwa ajili ya Wananchi wake.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameyasema hayo Addis Ababa Nchini Ethiopia alipokutana kwa mazungumzo na Jumuiya ya Watanzania waishio Nchini Ethiopia (Diaspora) waliotaka kufahamu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kupambana na UVIKO -19 ikiwa ni pamoja na suala la chanjo.

 

Aidha Balozi Mulamula amewataka Watanzania wanaofanya kazi katika Mashirika na Taasisi mbalimbali za Kimataifa kusaidia upatikanaji dozi nyingine za chanjo ya UVIKO 19 ili kuwawezesha Watanzania wengi  kupata chanjo hiyo kutokana na  mwamko wa Watanzania kuongezeka mara  baada ya kuzinduliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

 

Katika tukio jingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Ethiopia Mhe Sahle – Work Zewde Addis Ababa nchini Ethiopia ambapo Tanzania na Ethiopia zimekubalina kuendelea kutumia ndege za shirika la Ethiopia kutangaza vivutio na kusafirisha Watalii kutoka mataifa mbalimbali kuja Tanzania.

 

Aidha Balozi Mulamula amemhakikishia Rais Sahle – Work Zewde kuwa Tanzania itaendelea kutekeleza maeneo yote ya ushirikiano ambayo Rais Zewde alikubaliana na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa ziara ya Rais huyo Chato nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na suala la kuwarejesha Nchini Ethiopia wahamiaji wanaoshikiliwa katika magereza mbalimbali.

 

Kwa upande wake Rais wa Ethiopia  Mhe. Sahle – Work Zewde amesisitiza kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Nchi hiyo hususani katika kutatua changamoto zinazozuia maendeleo miongoni mwa Mataifa hayo.

RAIS WA ETHIOPIA MHE. SAHLE - WORK ZEWDE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI MULAMULA ADDIS ABABA - ETHIOPIA

Rais wa Ethiopia Mhe. Sahle – Work Zewde akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula(Mb).

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Rais Zewde, Addis Ababa, Ethiopia 11 Agosti,2021.


Rais wa Ethiopia Mhe. Sahle – Work Zewde akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula(Mb) mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi za Rais Zewde, Addis Ababa, Ethiopia 11 Agosti,2021.

Rais wa Ethiopia Mhe. Sahle – Work Zewde akiwa katika ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula(Mb) mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi za Rais Zewde, Addis Ababa, Ethiopia. 11 Agosti,2021. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Naimi Azizi na Kushoto kwa Rais Zewde ni Kaimu Balozi wa Ethiopia Bi Elizabeth.
 

Tuesday, August 10, 2021

TANZANIA YASAINI MKATABA WA UANZISHWAJI WA TAASISI YA UDHIBITI WA DAWA YA UMOJA WA AFRIKA (AMA)


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Dkt. Monica Nsanzabaganwa wakionesha mkataba wa Tanzania wa kukubali kuanzishwa kwa Taasisi ya Udhibiti wa Dawa ya Umoja wa Afrika (African Medicines Agency (AMA)) mara baada ya kusaini Mkataba huo tarehe 10 Agosti,2021 katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika  Addis Ababa, Ethiopia.Tanzania inakuwa Nchi ya 22 kusaini Mkataba huo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) panoja na  Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Dkt. Monica Nsanzabaganwa wakionesha Mkataba wa Tanzania wa kukubali kuanzishwa kwa Taasisi ya Udhibiti wa Dawa ya Umoja wa Afrika (African Medicines Agency (AMA)) mara baada ya kusaini Mkataba huo tarehe 10 Agosti,2021 katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika  Addis Ababa, Ethiopia.Tanzania inakuwa Nchi ya 22 kusaini Mkataba huo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Dkt. Monica Nsanzabaganwa wakionesha Mkataba wa Tanzania wa kukubali kuanzishwa kwa Taasisi ya Udhibiti wa Dawa ya Umoja wa Afrika (African Medicines Agency (AMA)) mara baada ya kusaini Mkataba huo tarehe 10 Agosti,2021 katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika  Addis Ababa, Ethiopia.Tanzania inakuwa Nchi ya 22 kusaini Mkataba huo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Dkt. Monica Nsanzabaganwa pamoja na baadhi wajumbe kabla ya kusaini mkataba wa Tanzania wa kukubali kuanzishwa kwa Taasisi ya Udhibiti wa Dawa ya Umoja wa Afrika (African Medicines Agency (AMA)) 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe alioongozana nao katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika zilizopo Addis Ababa nchini Ethiopia mara baada ya kusaini mkataba wa Tanzania wa kukubali kuanzishwa kwa Taasisi ya Udhibiti wa Dawa ya Umoja wa Afrika (African Medicines Agency (AMA)) Tarehe 10 Agosti,2021. Tanzania inakuwa Nchi ya 22 kusaini Mkataba huo

Monday, August 9, 2021

WAZIRI MULAMULA AMUAGA BALOZI WA OMAN

  Na Mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amemuaga Balozi wa Oman nchini, Mhe. Ally Abdallah Almahruqi katika ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini.

Balozi Mulamula amempongeza Balozi Almahruqi kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kudumisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Oman na Tanzania wakati wote wa uwakilishi wake hapa nchini.

“Tanzania tunashukuru zaidi kwa ushirikiano uliotuonesha wakati wote ulipokuwa hapa kama Balozi na tunakuahidi kuudumisha na kuuendeleza ushirikiano huo kwa maslahi ya nchi zetu mbili (Tanzania na Oman)," amesema Balozi Mulamula

Kwa upande wake Balozi wa Oman aliyemaliza muda wake wa uwakili hapa Nchini Mhe. Ally Abdallah Almahruqi ameishukuru Tanzania kwa ushirikiano alioupata wakati wote alipokuwa akitekeleza majukumu yake.

“Nawashukuru sana kwa ushirikiano mlionipatia wakati wote niliokuwa hapa nikitekeleza majukumu yangu kama Balozi, hakika nilifarijika sana……….naahidi kuwa nitakuwa balozi mwema kwa Serikali ya Tanzania,” amesema Balozi Almahruqi  

Pia Balozi ameipongeza Tanzania kwa hatua inazochukua za kupambana na virusi vya korona ikiwemo kuungana na mataifa mengine duniani kuchanja chanjo ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19.

Tanzania na Oman zimekuwa zikishirikiana katika sekta mbalimbali ikiwemo uwekezaji katika madini, mafuta, gesi, kilimo, usafirishaji, utalii pamoja na biashara. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Balozi wa Oman nchini, Mhe. Ally Abdallah Almahruqi katika hafla ya kumuaga mara baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini. Hafla ya kumuaga imefanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Oman aliyemaliza muda wake wa uwakilishi nchini, Mhe. Ally Abdallah Almahruqi akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimkabidhi zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro Balozi wa Oman aliyemaliza muda wake wa uwakilishi nchini, Mhe. Ally Abdallah Almahruqi  


Thursday, August 5, 2021

BALOZI MULAMULA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA QATAR

 Na Mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar nchini Tanzania Mhe. Hussain Ahmad Al Homaid leo Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao walijadili masuala ya kuimraisha uhusiano wa kidiplomasia, kuendeleza biashara na uwekezaji katika sekta za sekta za Madini, Utalii, pamoja na Mafuta na Gesi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Balozi wa Qatar nchini Mhe. Hussain Ahmad Al Homaid leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

   Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Qatar nchini Mhe. Hussain Ahmad Al Homaid yakiendelea

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongea na Balozi wa Qatar nchini Mhe. Hussain Ahmad Al Homaid leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula pamoja na Balozi wa Qatar nchini Mhe. Hussain Ahmad Al Homaid wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara pamoja na Ubalozi wa Qatar


WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA NJE YA NCHI

Na Mwandishi wetu, Dar

Watanzania wamepewa changamoto ya kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana Nje ya Nchi ili waweze kuinua uchumi wao pamoja na uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Changamoto hiyo imetokewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakati alipofanya ziara ya kutembelea Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd leo Jijini Dar es Salaam.

Balozi Mulamula amewasihi watanzania kuchangamkia fursa za masomo, masoko pamoja na biashara na uwekezaji na endapo kuna mtanzania anakwama basi asisite kuwasiliana na Wizara ili asaidiwe kupata ufumbuzi wa changamoto inayomkabili na kumwezesha kupata fursa husika.

“Fursa mbalimbali zimekuwa zikitangazwa katika Mashirika na Asasi za Kimataifa lakini watanzania wamekuwa wazito kiasi flani kuchangamkia fursa hizo, mfano fursa ya kufundisha lugha ya Kiswahili nje ya nchi, fursa ya kuuza bidhaa za kilimo nje ya nchi na nyingine nyingi………rai yangu kwa watanzania tuchangamkie fursa hizi ili tuweze kuinua kipato na uchumi wetu na taifa kwa ujumla,” amesema Balozi Mulamula

Pia Balozi Mulamula amewahakikishia ‘Diaspora’ kuwa serikali inatambua na kuthamini mchango wao na kwa sasa inaendelea kuandaa Sera ya Mambo ya Nje ili kuwawekea mazingira bora na salama ya uwekezaji nchini.

Pamoja na mambo mengine, Balozi Mulamula ameipongeza Kampuni ya Mwananchi kwa kuhabarisha na kuelimisha jamii kwa weledi wa taaluma ambao umekuwa ukiwawezesha wananchi kufahamu mambo mbalimbali yanayoendela nchini.

“Vyombo vya habari vya Mwananchi ni mdau muhimu sana kwani vimekuwa vikihabarisha na kuelimisha wadau mbalimbali mambo mazuri yanayotekelezwa na Serikali ya Tanzania,” amesema Balozi Mulamula

Balozi Mulamula ameongeza kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itaendelea kushirikiana kwa karibu na vyombo vya habari katika kuhakikisha kuwa vinaitambulisha vyema Serikali ya Tanzania vyema katika mataifa mbalimbali.

Balozi Mulamula ametembelea Kampuni ya Mwananchi Communications Limited wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti na kujionea shughuli zinavyofanyika pamoja na kuongea na wahariri wa Magazeti hayo. 

Tarehe 04 Juni, 2021 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula alifanya ziara yake ya kwanza katika vyombo vya habari vya habari vya IPP ambavyo ni ‘The Guardian Ltd’ inayozalisha magazeti ya The Guardian na Nipashe, Radio One, Capital radio, East Africa radio, ITV, Capital TV pamoja na East Africa TV.

1.  Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications Limited Bw. Bakari Machumu akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi za Mwananchi Communications Ltd Jijini Dar es Salaam. Mwingine ni Naibu Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi, Bw. Rashid Kejo 


1.  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwaelezea jambo Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications Limited Bw. Bakari Machumu pamoja na Naibu Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi, Bw. Rashid Kejo 


1.  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiangalia gazeti la Mwananchi wakati wa kikao


1.  Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications Limited Bw. Bakari Machumu akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nakala za Magazeti ya Mwananchi, The Citizen pamoja na Mwanaspoti


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimsikiliza mmoja kati ya wafanyakazi wa mwananchi   

1.  Naibu Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi, Bw. Rashid Kejo akimuonesha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula namna magazeti yanavyohifadhiwa katika jalada maalum


Kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na wahariri wa Mwananchi Communications Limited kikiendelea 

1.  Kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na wahariri wa Mwananchi Communications Limited kikiendelea  



Wednesday, August 4, 2021

BALOZI MULAMULA: ZIARA YA RAIS SAMIA RWANDA IMEIMARISHA UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA

 Na Mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amesema moja ya mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini Rwanda ni kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia, kukuza biashara na uwekezaji pamoja na kuimarisha sekta ya uchukuzi baina ya Tanzania na Rwanda.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Waziri Mulamula amesema kuwa mbali na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, pia ziara ya Mhe. Rais nchini Rwanda nchini Rwanda ziara hiyo imekuwa kielelezo kizuri cha ujirani mwema, na imeweka msingi mzuri wa ushirikiano baina ya nchi zetu mbili katika siku za usoni na walionesha kuridhishwa kwao na hali ya uhusiano uliopo.

Pamoja na mambo mengine, Waheshimiwa Marais walikubaliana kuharakisha majadiliano kuhusu Rwanda kuongeza matumizi yake ya Mkongo wa Taifa wa Tanzania.

“Nchi zetu zilikubaliana kuhakikisha kwamba upembuzi yakinifu unaofanywa kuhusu kuanzisha kiwanda cha maziwa Mkoani Mwanza unakamilika ifikapo mwezi Septemba, 2021. Kukamilika kwa mchakato huo na kuanza kwa uwekezaji kutatoa fursa za ajira kwa vijana wetu, lakini pia kutaongeza soko kwa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa katika Kanda ya Ziwa,” amesema Balozi Mulamula.

Balozi Mulamula ameongeza kuwa Waheshimiwa Marais wamebaini fursa mbalimbali za ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda ambazo zitakuwa na manufaa kwa Serikali na wananchi ikiwemo sekta za biashara na uwekezaji na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.  

“Ziara ya Mhe. Rais Samia nchini Rwanda ililenga pia kuimarisha ushirikiano katika uendelezaji wa miundombinu ya ushoroba wa kati ambapo Serikali ya Tanzania inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuimarisha uchukuzi kupitia ushoroba wa Dar es Salaam chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, ikiwemo uboreshaji wa Bandari za Dar es Salaam na Tanga na ujenzi wa miundombinu ya reli. Jitihada hizo zinalenga kurahisisha na kupunguza muda na gharama za usafirishaji. Hivyo, Mhe. Rais aliwakaribisha wafanyabiashara na wasafirishaji kutoka Rwanda kuendelea kutumia Bandari za Tanzania, ameongeza Balozi Mulamula.

Balozi Mulamula pamoja na Mambo mengine amesema kuwa katika ziara hiyo, Mhe. Samia akiwa na mwenyeji wake Mhe. Paul Kagame walishuhudia utiaji saini wa Hati za Makubaliano ya Ushirikiano nne (4) ambazo ni ati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika sekta ya Elimu, Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika sekta ya TEHAMA, Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika sekta ya Uhamiaji pamoja na Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika sekta ya Usimamizi wa Bidhaa za Dawa.

“Waheshimiwa Marais walishuhudia pia uwekaji saini wa Tamko la Pamoja la Ziara (Joint Communique) linaloainisha maeneo ya ushirikiano yaliyokubaliwa na kutoa mwongozo wa utekelezaji,” amesema Balozi Mulamula.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mulamula ameongeza kuwa, Rais Samia alitembelea kiwanda cha kutengeneza maji, maziwa na juisi cha Inyange, kutembelea eneo la Makumbusho la Mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda Mwaka 1994 ambapo aliweka Shada la Maua kama ishara ya kumbukumbu kwawote waliopoteza maisha.

Katika ziara hiyo, Mhe. Rais Paul Kagame alielezea utayari wa Rwanda kuanza kufundisha lugha ya Kiswahili katika shule zake na hivyo watahitaji walimu wa lugha ya kiswahili.  

Katika Tukio jingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Nam Tien.

Pamoja na mambo mengine, mazungumzo ya viongozi hao yalilenga kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia uliopo baina ya Tanzania na Vietnam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam. kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz.  


 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz.  


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Nam Tien katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

 


Kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Nam Tien kikiendelea


BALOZI MULAMULA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE MAREKANI

 Na Mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anaeshughulikia masuala ya Siasa Mhe. Victoria Nuland Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, mazungumzo ya viongozi hao yalilenga kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia uliopo baina ya Tanzania na Marekani.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anaeshughulikia masuala ya Siasa Mhe. Victoria Nuland akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anaeshughulikia masuala ya Siasa Mhe. Victoria Nuland katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Kikao baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anaeshughulikia masuala ya Siasa Mhe. Victoria Nuland kikiendelea   


Kikao baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anaeshughulikia masuala ya Siasa Mhe. Victoria Nuland kikiendelea   



Saturday, July 31, 2021

SERIKALI YA ZANZIBAR YAAPA KUULINDA MUUNGANO

 Na Mwandishi wetu, Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuulinda Muungano kwa kuwa ndio tunu kubwa ambayo imeachwa na waasisi wa Muungano huo na kwamba Serikali haitotumia nguvu kwa baadhi ya wananchi wenye maoni taofauti bali itawaelimisha.

Ahadi hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla wakati alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ulioongozwa na Waziri wa Wizara hiyo Balozi Liberata Mulamula (Mb) na kuongeza kuwa Zanzibar inatambua umuhimu wa Muungano uliopo pamoja na manufaa yake huku akitolea mfano kwa baadhi ya Wazanzibar wanaoishi Bara ambao ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameongeza kuwa kwa sasa Serikali imeweka kipaumbele katika masuala ya kuimarisha uchumi na kuwaletea Wazanzibar maendeleo kutokana na umoja, amani na mshikamano uliopo tangu uwepo wa muafaka wa Serikali ya Kitaifa na kuwataka wafanyabiashara na wawekezaji kujitokeza kuwekeza visiwani humo katika sekta mbalimbali ikiwemo eneo la Uchumi wa Buluu.

Akizungumza wakati wa kujitambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano uliopo katika utendaji kazi na kwamba kwa sasa Wizara inaendelea na maandalizi ili kuwawezesha Viongozi wakuu wa pande zote mbili kushiriki kikamilifu katika mikutano ya Kimataifa.

Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukiongozwa na Balozi Liberata Mulamula ambaye ameambatana na Naibu Waziri Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine pamoja na Naibu Katibu Mkuu Balozi Fatma Mohammed Rajab na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara hiyo uko visiwani Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha kwa viongozi wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiongea na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati uongozi huo ulipomtembelea Ofisini kwake Zanzibar. Uongozi wa Wizara umeongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, Naibu Waziri Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk, Katibu Mkuu, Balozi Joseph Sokoine, Naibu Katibu Mkuu, Balozi Fatma Mohammed Rajab pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa Idara na vitengo vya Wizara.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje ulipomtembelea Ofisini Kwake Zanzibar   


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akisisitiza jambo kwa Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati uongozi huo ulipomtembelea Ofisini kwake Zanzibar. Uongozi wa Wizara umeongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, Naibu Waziri Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk, Katibu Mkuu, Balozi Joseph Sokoine, Naibu Katibu Mkuu, Balozi Fatma Mohammed Rajab pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa Idara na vitengo vya Wizara.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na  Naibu Waziri Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk




Thursday, July 29, 2021

DKT MWINYI ATOA MAELEKEZO KWA WIZARA YA MAMBO YA NJE

Na Mwandishi wetu, Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kipaumbele cha Serikali yake hususani katika sekta ya mafuta na gesi,Utalii,Uvuvi Biashara na Uwekezaji ni katika Uchumi wa Buluu ambao utamsaidia Mzazibar katika kuimarisha kipato pamoja na kuondoa kodi za kero kwa Wanzazibar.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ulioongozwa na Waziri wa Wizara hiyo Balozi Liberata Mulamula (Mb) kwa lengo la kujitambulisha na kupokea maelekezo ya kutekeleza  vipaumbele vya Serikali ya mapinduzi Zanzibar.

Dkt. Mwinyi ameilekeza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutilia mkazo katika uwekezaji wa maeneo ya Uchumi wa Buluu katika mazungumzo na Mashirika ya fedha duniani ikiwemo IMF na Benki ya dunia ikiwa ni pamoja na wawekezaji na wafadhili mbalimbali kwa kuwa Serikali yake ina imani kuwa bahari ikitumiwa vizuri itainufaisha Zanzibar kiuchumi kuliko maeneo mengine.

Pia Dkt. Mwinyi ameitaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuwasaidia wafanyabiashara kutoka Zanzibar kwa kuwaunganisha na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nje ili Zanzibar nayo iweze kusafirisha bidhaa zake za ndani kwenda nje badala ya kupokea bidhaa kutoka mataifa mengine kama ilivyo sasa.

Dkt. Mwinyi amezitaja bidhaa kutoka Zanzibar zinazoweza kusafirishwa Nje ya Zanzibar kuwa ni pamoja na karafuu,samaki na nyama ambazo zina soko kubwa nje ya nchi hususani katika nchi za Kiarabu.

Mbali na hilo Dkt. Mwinyi ametaka kupitiwa upya kwa Sera ya Mambo ya Nje ya Nchi hususani katika suala Wazanzibar wanaoishi nje maarufu kama Diaspora ikiwemo kupatiwa hadhi maalum itakayowawezesha kushiriki katika uchumi wa nchi ikiwemo kuwekeza,kubadilishana uzoefu wa kitaaluma na masuala mengine ya maendeleo.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amesema Wizara imeyapokea maelekezo ya Rais Dkt Hussein na kwamba tayari kuna mkakati na maelekezo maalum kwa Mabalozi wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mataifa mbalimbali duniani ili kuhakikisha mahusiano ya Tanzania na Nchi hizo yanakuwa ya manufaa katika uchumi wa pande zote za Jamuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika tukio jingine Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake wamekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa kwanza wa Rais Mhe. Othman Masoud Othman ambaye kwa upande wake ameeleza nia ya Ofisi yake katika kupambana kudhibiti biashara na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na suala la mazingira ambayo kwa kiasi kikubwa yameathirika kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi jambo ambalo linatishia uhai wa Visiwa mbalimbali duniani ikiwemo Zanzibar.

Katika tiara hiyo Balozi Mulamula ameambatana na Naibu Waziri Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb), Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine, Naibu Katibu Mkuu Balozi Fatma Mohammed Rajab pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Idara na Vitengo vya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula alipokuwa Ikulu - Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiongea na uongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ulioongozwa na Waziri wake Mhe. Balozi Liberata Mulamula walipokuwa Ikulu - Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Katibu wa baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi - Zanzibar na Uongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukiongozwa na Waziri wake Mhe. Balozi Liberata Mulamula. wengine ni Naibu Waziri, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb), Katibu Mkuu, Balozi Joseph Sokoine pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Fatma Mohammed Rajab

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Uongozi wa Wizara umeongozwa na Mhe. Waziri, Balozi Liberata Mulamula (Mb) na kuwataka kuandaa mpango maalumu wa kushirikiana na Zanzibar kwa lengo la kuendelea kuitangaza na kuboresha uhusiano wake na nchi mbalimbali duniani

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, akizungumza na viongozi wakuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Uongozi wa Wizara umeongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula (Mb), Naibu Waziri, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb), Katibu Mkuu, Balozi Joseph Sokoine pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Fatma Mohammed Rajab katika ziara rasmi ya kujitambulisha kwa Viongozi Waandamizi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.  


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman katika picha ya pamoja na  viongozi wakuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Uongozi wa Wizara umeongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula (Mb), Naibu Waziri, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb), Katibu Mkuu, Balozi Joseph Sokoine pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Fatma Mohammed Rajab.